Mpendwa msomaji bado naendelea na somo hili la maombi ya
kufungua malango na milango, ambalo pia utaweza jipatia nakala ya kitabu chako
hivi punde.
Toleo lilipita nilikugusia juu ya ufunguo wa pili wa
kufungua milango na malango ambapo nilikufundusha juu ya imani. Bado
tunaendelea na aina hizi tano za funguo na leo nitakufundisha juu ya ufunguo wa
tatu…..Endelea.
UFUNGUO WA TATU;
TOBA
Toba ni tendo la kiimani la kuungama dhambi na maovu yote
yaliyokwisha kufanyika kwa nia ya kujenga upya mahusiano na Mungu aliye hai
sawasawa na Neno lake. Maana dhambi ni uasi hivyo atendaye dhambi hujitenga na
rehema za Mungu. “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha
atapata rehema.” Mithali 28:13
Yako malango na milango iliyofungwa kwa watu wa Mungu kwa
sababu ya dhambi. Maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa
Mungu. Palipo dhambi na makosa panahitaji toba si vinginevyo. Watu wengi wameruka
ufunguo huu matokeo yake wamefunga na kuomba hawakupata majibu kwa kuwa Mungu
hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho atakacho vuna. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni
mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”
Warumi 6:23
Tunajifunza kwa mtumishi wa Mungu Danieli baada ya kuvisoma
vitabu vyenye maneno ya Mungu alipata ufahamu utokanao na Neno, akaamini
sawasawa na Neno la Mungu jambo la tatu akachukua hatua ya kutubia maovu na
dhambi zake na za Taifa lake. Ili kwa njia ya toba BWANA awafungulie milango na
malango yaliyokuwa yamefungwa kwa nguvu za miungu ya Babeli.
“Katika mwaka wa
kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme
juu ya milki ya Wakaldayo; katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi
Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA
lilimjia Yeremia nabii, yaani, miaka sabini. Nikamwelekezea Bwana Mungu uso
wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za
magunia na majivu. Nikamwomba BWANA, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee
Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao,
na kuzishika amri zake; tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu,
tumeasi, naam, kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako; wala hatukuwasikiliza
watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu
wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi. Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu
sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa
Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi
zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa. Ee Bwana, kwetu sisi
kuna haya ya uso, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu tumekutenda
dhambi. Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi, wala
hatukuitii sauti ya BWANA, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake,
alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii. Naam, Israeli
wote wameihalifu sheria yako, kwa kugeuka upande, wasiisikilize sauti yako;
basi kwa hiyo laana imemwagwa juu yetu, na uapo ule ulioandikwa katika sheria
ya Musa, mtumishi wa Mungu; kwa sababu tumemtenda dhambi. Na ye ameyathibitisha
maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuziwetu waliotuamua, kwa
kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama
hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu. Kama ilivyoandikwa katika sheria ya
Musa, mabaya haya yote yametupata lakini hata hivyo hatukumwomba BWANA, Mungu
wetu, atupe fadhili zake, ili tugeuke na kuyaacha maovu yetu, na kuitambua
kweli yake. Basi BWANA ameyavizia mabaya hayo, akatuletea; maana BWANA, Mungu
wetu ni mwenye haki katika kazi zake zote azitendazo; na sisi hatukuitii sauti
yake. Na sasa, Ee Bwana Mungu wetu, uliyewatoa watu wako hawa katika nchi ya
Misri kwa mkono hodari, ukajipatia sifa, kamailivyo leo; tumefanya dhambi,
tumetenda maovu. Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na
ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu;
maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako
wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka. Basi sasa, Ee Mungu wetu,
yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya
patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana. Ee Mungu wangu, tega sikio
lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa
kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini
kwa sababu ya rehema zako nyingi. Ee Bwana, usikilize, ukatende, usikawie; kwa
ajili yako wewe, Ee Mungu wangu; kwa sababu ya mji wako na watu wako wanaitwa
kwa jina lako. Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi
yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za BWANA,
Mungu wangu, kwa ajili yam lima mtakatifu wa Mungu wangu; naam, nilipokuwa
nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo
kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.
Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe
akili upate kufahamu. Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja
kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na
kuyafahamu maono haya. Muda wa majuma sabini umuamuriwa juu ya watu wako, na
juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na
kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na akuleta haki ya milele, na kutia
muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu. Basi ujue na
kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu
hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba, na katika majuma
sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam,
katika nyakati za taabu. Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi
atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja
watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika , na
hata mmwisho ule vita vitakuwepo; ukiwa umekwisha kukusudiwa. Naye atafanya
agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo
ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu;
na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye
kuharibu.”
Danieli 9:1-27
Danieli anaanza kwa Kuungama ili apate kufungua Malango na
Milango iliyofungwa.
Unapotubu dhambi na kuziacha ni Mlango wa kuinuliwa, Hata
kama umetupwa chini, Maandiko yanasema wazi Mtu mwaminifu atakuwa na Baraka tele
na Malango yake yatafunguliwa daima.
“Haya njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa
nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theruji, zijapokuwa nyekundu kama bendera
zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi, bali
kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga maana kinywa cha BWANA kimenena
haya.” Isaya 1:18-19
Angalia pia watu wa Ninawi, walivyofungua Malango yao kwa
nguvu ya TOBA, maana Walilisikia Neno, Wakaliamini na Kutubu, Naye Yehova
akawafungua. Walibatilisha lango la mauti kwa njia ya toba. Hivyo toba ina
nguvu katika Mungu hata kuangusha ngome za mauti na kuzimu. Mfalme wa Ninawi
aligeuza hasira ya Mungu juu yake na watu wake pale alipoomba rehema za Mungu
kwa njia ya toba. Nasi tukiomba rehema kwa ajili yetu na watoto wetu hakika
BWANA ni mwingi wa rehema si mwepesi wa hasira, yeye husamehe wote wanao
jinyenyekeza kwake.
“Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye
akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za
magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu akatangaza habari katika
mji wa Ninawi kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema mwanadamu asionje kitu,
wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo, wasile wala
wasinywe maji bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao
wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya,
na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na
kughairi na kuiacha hasira yake kali ili msiangamizwe? Mungu akaona matendo yao
ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akaghairi neno lile baya ambalo
alisema atawatenda, asilitende.” Yona
3:6-10
TOBA ilirejesha upya uhai kwa watu wa Ninawi.
Nasi Kanisa hatuwezi kufunguliwa Malango na Milango pasipo
kufanya TOBA ya kweli.
“Tazama mkono wa BWANA haukupunguka, hata
usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu
yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake
msiuone, hata hataki kusikia.” Isaya 59:1-2
Lazima uiondoe dhambi katikati yako kwa Kutubu na Kuungama
mbele za Mungu. Ufunguo huo wa TOBA ndio unaotupa Uwezo na Ujasiri wa kupaingia
Patakatifu pake Mungu aliye hai kwa jinsi ya Imani. Ni lazima MKRISTO
UZAE MATUNDA YAPASAYO TOBA.
“Basi zaeni matunda yapasayo toba.”
Mathayo 3:8”
Wokovu maana yake ni Kutengwa mbali na dhambi.
Hatuwezi kufunguliwa Milango ya Baraka
na Ustawi kama hatutajitenga na maovu.
“Ndipo Yona akamwomba BWANA Mungu wake,
katika tumbo la yule samaki, akasema, Nalimlilia BWANA kwa sababu ya shida
yangu, naye akaniitikia; katika tumbo la kuzimu naliomba. Nawe ukaisikia sauti
yangu. Maana ulinitupa vilindini, ndani ya moyo wa bahari, gharika ya maji
ikanizunguka pande zote, Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu
yangu. Nami nikasema nimetupwa mbali na macho yako, lakini nitatazama tena
kukabili hekalu lako takatifu. Maji yalinizunguka hata nafsini mwangu, Vilindi
vilinizunguka, mwani ulikizinga kichwa
changu, Nalishuka hata pande za chini za milima, Huyo nchi na mapingo yake
yalinifunga hata milele. Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee
BWANA, Mungu wangu, Roho yangu ilipozimia ndani yangu, nalimkumbuka BWANA;
maombi yangu yakakuwasilia katika hekalu lako takatifu. Watu waangaliao mambo
ya ubatili na uongo, Hujitenga na rehema zao wenyewe; lakini mimi nitakutolea
sadaka kwa sauti ya shukurani, nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa
BWANA. BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.”
Yona
2:1-10
Nabii Yona alipo Omba toba na Rehema akiwa ndani ya tumbo la
nyangumi, BWANA akamwinua tena, akamfungulia Milango na Malango ya Utumishi.
Angalia pia Samsoni pamoja na kumkosea Mungu kwa kiwango kikubwa kwa uzinzi
mpaka akatobolewa macho, Lakini alipo Omba TOBA, Jehova Elshadai, Mungu
anayetenda zaidi ya tarajio akamwinua tena.
“Samsoni akaenda
Gaza, akaona huko mwanamke kahaba, akaingia kwake. Watu wa Gaza wakaambiwa
yakwamba, huyo Samsoni amekuja huku, wakamzingira wakamvizia usiku kucha penye
lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, na tungoje mpaka
mapambazuko, ndipo tutamwua. Basi Samsoni akalala hata usiku wa manane,
akaondoka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji na miimo yake
miwili, akaing’oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hata
kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni. Ikawa baada ya hayo akampenda mwanamke
mmoja katika bonde la Soreki, jina lake akiitwa Delila. Nao wakuu wa Wafilisti
wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi,
na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa
kila mtu fedha elfu na mia moja. Delila akamwambia Samsoni, Tafadhali uniambie
asili ya nguvy zako nyingi, na jinsi uwezavyo kufungwa, ili uteswe. Samsoni
akamwambia, wakinifunga kwa kamba mbichi saba ambazo hazija kauka bado, hapo
ndipo nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Ndipo wakuu wa
Wafilisti wakamletea kamba mbichi saba zisizokauka, naye akamfunga nazo. Na
yule mwanamke alikuwa na watu katika chumba cha ndani, wakimwotea. Basi
akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakuja. Ndipo akazikata zile kamba kama vile
uzi wa pamba ukatwavyo ukiguswa na moto. Basi hiyo asili ya nguvu zake
haikujulikana. Delila akamwambia Samsoni, Tazama, umenidhihaki na kuniambia
uongo; sasa tafadhali, niambie, wawezwa kufungwa kwa kitu gani? Akamwambia
wakinifunga tu kwa kamba mpya ambazo mtu hakufanya kazi nazo, hapo ndipo
nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Basi Delila akatwaa kamba
mpya akamfunga nazo, akamwambia, Wafilisti wanakuji, Samsoni, na wale wenye
kuotea walikuwa katika chumba cha ndani. Naye akazikata, akazitupa kutoka
mikononi mwake kama uzi. Delila akamwambia Samsoni, hata sasa umenidhihaki,
umeniambia maneno ya uongo; niambie sasa, waweza kufungwa kwa kitu gani?
Akamwambia, ukivifuma hivi vishungi saba vya nywele za kichwa changu katika
mtande wa nguo. Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti
wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung’oa ule msumari, na ule mtande. Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema,
Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala
hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi. Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa
maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa. Ndipo
alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, wembe haukupita juu ya
kichwa change kamwe; maana mimi nimekuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa
mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu,
nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote
yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema,
Njoni huku nmara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo
wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao. Naye
akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi
saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka. Kisha
akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema,
nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA
amemwacha. Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakatelemka naye mpaka
Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika
gereza. Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa
kwake. Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu
wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi
mwetu. Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu
wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua
watu wengi miongoni mwetu. Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, mwiteni
Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze
mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili. Samsoni akamwambia yule kijana
aliyemshika mkono, niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate
kuzitegemea. Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote
wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume
kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza. Samsoni akamwita
BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba,
mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili
ya macho yangu mawili. Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo
nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja
kwa mkono wake wa kushoto. Samsoni akasema; na nife pamoja na hawa Wafilisti.
Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote
waliokuwa ndani yake. Basi wale watu waliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa
wengi kuliko wale waliowaua wakati wa uhai wake. Ndipo ndugu zake, na watu wote
wa nyumba ya baba yake wakatelemka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya
Sora na Eshtaoli, katika kiwanja cha
kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka
ishirini.” Waamuzi
16:1-31
TOBA ilimfanya Samsoni ahesabiwe kuwa miongoni mwa Mashujaa
wa Imani maana wokovu aliouleta siku ya kufa kwake ulikomesha ufalme wa
Wafilisti kwa kuwa aliwaangamiza kuanzia mdogo mpaka mfalme wao. “Nami
niseme nini tena? Maana wakati usingetosha kuleta habari za Gidioni na Baraka
na Samsoni na Yefta na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani
walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa
vya samba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga, walitiwa
nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya
wageni.” Waebrania 11:32-34
Israeli wakafanya dhambi kwa kukosa uaminifu katika kitu
kilichowekwa wakfu. Walipokwisha kuangusha mji wa Yeriko na kuta zake na
wakauingia mji wa Ai. Akani mwana wa Zabdi mwana wa Zera wa kabila la Yuda,
alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu, hasira ya BWANA ikawaka juu ya wana
wa Israeli kutokana na kutokuwa waaminifu katika maagizo ya Mungu aliye hai.
“Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu
kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera,
wa kabila ya Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya BWANA
ikawaka juu ya wana wa Israeli. Kisha Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko mpaka
mji wa Ai, ulio karibu na Bethaveni, upande wa mashariki wa Betheli,
akawaambia, akisema, pandeni juu mkaipeleleze nchi, basi wakapanda juu
wakaupeleleza Ai. Wakarejea kwa Yoshua wakamwambia, wasiende watu wote, ila
waende watu kama elfu mbili, tatu, wakupige Ai; usiwataabishe watu wote kwa
kuwaendesha huko; maana watu hao ni wachache tu. Basi watu wakaenda huko wapata
elfu tatu tu; nao wakakimbia mbele ya watu Ai. Watu wa ai wakawapiga watu kama
thelathini na sita; wakawafuatia kutoka mbele ya mlango mpaka Shebarimu,
wakawapiga huko kwenye matelemko; mioyo ya watu ikayeyuka, ikawa kama maji.
Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA
hata jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao. Yoshua
akasema, Ee Bwana MUNGU, kwa nini umewavusha watu hawa mto wa Yordani, ili
kututia katika mikono ya Waamori, na kutuangamiza? Laiti tungelikuwa radhi
kukaa ng’ambo ya Yordani Ee Bwana, niseme nini baada ya Israeli kuwapa visogo
adui zao? Maana Wanaani na wenyeji wote wan chi hii watasikia habari hii,
naowatatuzingira, na kulifuta jina letu katika nchi. Nawe utafanya nini kwa
ajili ya jina lako kuu? BWANA akamwambia Yoshua, Haya! Inuka, mbona umeanguka
kifudifudi hivi? Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu
nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu, tena wameiba,
tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe. Ndiposa wana wa Israeli
hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu
wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho
nacho kilichowekwa wakfu. Haya! Inuka, uwatakase watu, ukaseme, Jitakaseni, mwe
tayari kesho; maana BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; kitu kilichowekwa
wakfu kiko katikati yako, Ee, Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata
mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu. Basi asubuhi mtaletwa
karibu nami kabila kwa kabila; kisha itakuwa ya kwamba kabila ile atakayoitwaa
BWANA itakaribia jamaa kwa jamaa; na jamaa ile atakayoitwaa BWANA itakaribia
nyumba kwa nyumba; na nyumba ile atakayoitwaa BWANA itakaribia mtu kwa mtu. tena
itakuwa ya kwamba yeye atakayetwaliwa, naye anacho kitu kile kilichowekwa
wakfu, akateketezwa kwa moto, yeye na vitu vyote alivyo navyo; kwa sababu
amelivunja agano la BWANA, na kwa sababu ametenda upumbavu katika Israeli. Basi
Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, akawasogeza Israeli kabila kwa kabila;
kabila ya Yuda ikatwaliwa. Akazisogeza jamaa za Yuda, akitwaa jamaa ya Wazera;
akaisogeza jamaa ya Wazera mtu kwa mtu; Zabdi akatwaliwa. Akawasogeza watu wa
nyumba yake mmoja mmoja; na Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa
Zera, wa kabila ya Yuda akatwaliwa. Yoshua akamwambia Akani, mwanangu,
nakusihi, umtukuze BWANA, Mungu wa Israeli, ukaungame kwake; uniambie sasa
ulilolitenda; usinifiche. Akani akamjibu Yoshua, akasema, kweli nimefanya
dhambi juu ya BWANA, Mungu wa Israeli, nami nimefanya mambo haya na haya.
Nilipoona nyara katika joho nzuri ya Babeli, na shekel mia mbili za fedha, na
kabari ya dhahabu, uzani wake shekel hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa;
tazama vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake.
Basi Yoshua akatuma wajumbe wakapiga mbio mpaka hemani; na tazama, vile vitu
vilikuwa vimefichwa hemani mwake, na ile fedha chini yake. Wakavitoa kutoka
hapo katikati ya hema, wakavileta kwa Yoshua, na kwa wana wa Israeli wote, nao
wakaviweka chini mbele za BWANA. Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye,
wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na lile joho, na ile kabari ya
dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo
zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde
la Akori. Yoshua akasema, mbona umetufadhaisha hivi? BWANA atakufadhaisha wewe
leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na
kuwapiga kwa mawe. Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa yam awe hata leo;
naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale
likaitwa, Bonde la Akori hata hivi leo.” Yoshua 7:1-26
Kitu kilichowekwa wakfu maana yake ni cha Mungu.
Mfano:
ZAKA ni sehemu ya kumi ya mali, mazao, mifugo, fedha n.k
BWANA ametoa maagizo na sheria maalumu katika vitu
vitakatifu, nayatupasa kupambanua kati ya vitu vitakatifu (wakfu) na vya siku
zote. Maandiko matakatifu yanasema;
“Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya
mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.” Kumbukumbu 14:22
Inasisitizwa kuwa makini na kuvitenga vitu vitakatifu kwa
Mungu visiwe au kuliwa katika malango ya nyumba zetu maana kufanya kinyume na
maagizo ya neno la Mungu ni kukaribisha laana na ukaufu katika kazi zetu za
mikono. Maandiko matakatifu yanasema;
“Usile ndani ya malango yako zaka ya nafaka zako, wala divai
yako, wala mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng’ombe
wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zo zote, wala sadaka zako za hiari,
wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako;” Kumbukumbu 12:17
Jilinde nafsi yako usile zaka siku zote za maisha yako;
maana ukila zaka umekula kitu kilichowekwa wakfu ni dhambi. “Kwa
kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio
maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo. Tokea siku za baba zenu
mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi,
name nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi
kwa namna gani? Je! Mwanadamu atamwambia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi.
Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa nanmna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. Leteni
zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa
njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya
mbinguni, nakuwamwagieni Baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami
kwa ajili yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati
wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi. Na mataifa yote watawiteni heri;
maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.” Malaki
3:6-12
Kutokutoa zaka ni kwenda kinyume na maagizo ya Mungu hivyo
mtu uliyeokoka ukila zaka utapigwa mbele ya adui zako;
·
Biashara yako itapigwa.
·
Ndoa yako itapigwa.
·
Elimu ya watoto wako itapigwa.
·
Ustawi wako utapigwa.
“Je mwanadamu utamwibia Mungu? Lakini ninyi; mnaniibia mimi
lakini ninyi mwasema tumekuibia kwa namna gani”
Kutokutoa zaka ni kumpora Mungu haki yake katika kazi zako
za mikono (sehemu ya kumi ya mapato yako) ni sehemu takatifu kwa Mungu. BWANA
anasema;
“Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni
matunda ya nchi, NI YA BWANA; NA KAMA MTU AKITAKA kukomboa cho chote cha zaka
yake, ATAONGEZA SEHEMU YAKE YA TANO juu yake.” Mambo ya Walawi 27:30-31
Sehemu ya kumi ni takatifu kwa Mungu. Hivyo kutoa zaka sio swala la hiari bali ni
lazima kama kulivyo kuokoka ni lazima, nje ya hapo utatupwa Jehanamu. Kumwacha
Mungu siyo lazima unywe pombe au ufanye uzinzi lakini kwa tendo la kukosa
uaminifu ni dhambi na Kristo anasema TUBUNI NA MREJEE, tafuteni ufalme wa Mungu
na haki yake na mengine yote mtazidishiwa. BWANA Yesu Kristo akasema;
“Ole wenu waandishi na mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa
mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria,
yaani, adili, na rehema, na imani; hayo IMEWAPASA KUYAFANYA, WALA YALE mengine
msiyaache.” Mathayo
23:23
Yesu Kristo aliunga mkono utoaji wa fungu la kumi
alipowakemea Mafalisayo waliotilia mkazo fungu la kumi tu huku wakiwa wamesahau
mambo ya adili na sheria. Wengine hudhani alipinga utoaji wa fungu la kumi,
lakini sivyo, yeye alikuwa anaweka uwiano.
Wako wanaodhani kuwa fungu la kumi sio lazima wakidai ni
kwaajili ya waumini wa agano la kale. Wao hudhani fungu la kumi ni agizo la
torati. Lakini sivyo. Fungu la kumi liliamriwa kabla ya torati unaweza kusoma “Abramu
aliporudi kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa
Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni bonde la mfalme. Na
Melkizedek mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa
Mungu aliye juu sana… Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.”
Mwanzo 14:17-20
Kwa kuwa Imani tu pasipo matendo ya haki ya kiimani, ufalme
wa Mungu hauwezi kuwa kwako. Ili malango na milango ifunguke sharti kuwa
mwaminifu. Maana BWANA ameahidi kwa ajili yetu atamkemea yeye alaye:
·
Asile tena Kazi zetu.
·
Asile tena Ndoa zetu.
·
Asile tena Familia zetu.
Maana Kristo Yesu “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana,
huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika dogo, huwa
dhalimu katika lililo kubwa pia.”
Luka 16:10
Ukishindwa kutoa zaka ya hicho kidogo unachopata, huwezi
kupewa kikubwa. BWANA anasema angamiza vyote lakini wewe kwa tamaa unaficha,
matokeo yake unaleta mauti katika familia yako badala ya Baraka na ustawi.
BWANA Yesu Kristo anasema “Akawaambia, Ninyi ndinyi
mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu awajua mioyo yenu; kwa
kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu. Luka 16:15
Maana vyote vitapita lakini Neno la Mungu halitapita kamwe
katika maisha yetu. Ufalme wa Mungu umo ndani yetu pale tunaposhika Neno lake
kwa uaminifu.
AKANI kwa tamaa ya joho tu na shekeli mia mbili za fedha
(Akani anasema NALITAMANI MKAVITWAA katika hema yangu na ile fedha. Akani na
familia yake waliangamizwa “Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye,
wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na lile joho, na ile kabari ya
dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo
zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde
la Akori. Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? BWANA atakufadhaisha wewe
leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakateketeza kwa moto, na
kuwapiga kwa mawe. Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa yam awe hata leo;
naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale
likaitwa, Bonde ka Akori, hata hivi leo.” Yoshua 7:24-26
Baada ya TOBA ya wana wa Israeli BWANA akasema “…Inukeni
mwende Ai; angalia mimi nimeutia Ai na watu wake; mji wake na nchi yake
mikononi mwenu na hawatasimama tena mbele yenu.”
Ushindi wetu wa ki-Mungu hutoka kwa Mungu hivyo afichaye
dhambi zake HATAFANIKIWA bali yeye aziungamaye atapata rehema mbele za Mungu.
Ufunguo huu ni wa muhimu sana katika maisha yetu “Afichaye
dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema”
Mithali 28:13
Kukosa uaminifu huleta kupigwa. Lazima tuchunguze mwenendo
wetu na tuyatubie matendo yetu mafu.
“[Ikiwa siku zile Wafilisti walikusanyika ili kupigana na
Israeli], nao Waisraeli wakatoka juu ya
Wafilisti kwenda vitani; wakatua karibu na Ebenezeri, nao Wafilisti wakajipanga
juu ya Israeli wakapigwa mbele ya Wafilisti; wakauawa watu wa jeshi lao
lililokuwa uwandani wapata watu elfu nne. Hata watu walipofika kambini, wazee
wa Israeli wakasema, mbona BWANA ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende
tukalilete sanduku la agano la BWANA toka Shilo hata huku, lije kati yetu, na
kutuokoa katika mikono ya adui zetu. Basi wakatuma watu kwenda Shilo, nao
wakalileta toka huko sanduku la agano la BWANA wa majeshi, akaaye juu ya
makerubi; na Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwako huko pamoja na
sanduku la agano la Mungu. Na sanduku la agano la BWANA lilipoingia Kambini,
Israeli wote wakapiga kelele kwa sauti kuu, hata nchi ikavuma. Nao Wafilisti
waliposikia mshindo wa zile kelele, walisema, Maana yake nini mshindo wa kelele
hizi kubwa katika kambi ya Waebrania? Wakatambua ya kuwa sanduku la BWANA
limefika kambini. Wafilisti wakaogopa, maana walisema, Mungu ameingia kambini.
Wakasema, Ole wetu! Kwani halijawa jambo kama hili tangu hapo. Ole wetu! Ni
nani atakayetuokoa na mkono wa miungu hawa walio hodari? Hawa ndio miungu
waliowapiga Wamisri kwa mapigo ya kila namna jangwani. Iweni hodari, na kufanya
kiume enyi Wafilisti, msije mkawa watumwa wa Waebrania, kama wao walivyokuwa
watumwa wenu; fanyeni kiume, mkapigane nao. Wafilisti wakapigana nao, Israeli
wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana
katika Israeli walianguka watu thelathini elfu wenye kwenda vitani kwa miguu.
Hilo sanduku la Mungu likatwaliwa; na Hofni na Finehasi, wale wana wawili wa
Eli, wakauawa. Basi, mtu mmoja wa Benyamini akapiga mbio kutoka mle jeshini
akafika Shilo siku ile ile, hali nguo zake zimeraruliwa, na mavumbi kichwani
mwake. Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia,
akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule
mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia. Naye Eli aliposikia
kelele za kile kilio, akasema, maana yake nini kelele za kishindo hiki? Yule
mtu akafanya haraka, akaenda, akamwambia Eli. Basi Eli umri wake umepata miaka
tisini na minane; na macho yake yamepofuka hata asiweze kuona. Yule mtu
akamwambia Eli, Mimi ndimi niliyetoka jeshini, nami leo hivi nimekimbia toka
jeshini. Naye akasema, Yalikwendaje, mwanangu? Yeye aliyeleta habari akajibu,
akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa,
hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu
limetwaliwa. Ikawa walipotaja sanduku la Mungu, Eli akaanguka kitini pake kwa
nyuma, kando ya mlango, shingo yake ikavunjika, akafa; maana alikuwa mzee, tena
mzito. Naye alikuwa amewaamua Israeli miaka arobaini. Tena mkwewe, mke wa huyo
Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya
kutwaliwa sanduku la Mungu, nay a kwamba mkwewe na mumewe wamekufa,
akijiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia. Hata alipokuwa katika
kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana
umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama. Akamwita mtoto,
Ikabodi, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la
Mungulilikuwa liketwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe.” 1Samweli 4:1-21
Israeli walipopigwa hawakuangalia kwa makini sababu ya
kupigwa kwao matokeo yake badala ya kufanya toba wakaanza kusaka vitu vya upako
viwasaidie katika vita vyao, matokeo yake wakapigwa navyo, wakafa watu wengi
sana na sanduku la BWANA Mungu wa majeshi likatekwa.
Ndivyo walivyo wakristo wengi siku za leo, milango na
malango yao yanapofungwa badala yakutengeneza njia zao mbele za Mungu, matokeo
yake wanasaka vitu vya upako, kama vile maji, mafuta chumvi, vipande vya sabuni
matokeo yake wamefarakana na Mungu kwa kufuata ibada ziliotungwa kwa namna ya
wanadamu. Maana Mungu ni Roho na wale wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu
katika roho na kweli, kwa mantiki hiyo mtu wa Mungu zingatia kweli ya Mungu
ndani ya Neno lake si vinginevyo, mahali pa toba fanya toba. BWANA anasema; “Basi,
kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa uungu ni mfano wa
dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu.
Basi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni bali sasa amewaagiza
watu wote wa kila mahali watubu.” Matendo17:29-30
Nasi yatupasa tutengeneze mienendo yetu maana pasipo kuwa na
matendo ya haki tukakimbilia kulitaja jina la Kristo Yesu tu, malango na
milango havitafunguka.
“Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe
kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako? Maana wewe
umechukia maonyo, na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. Ulipomwona mwivi ulikuwa
radhi naye, ukashirikiana na wazinzi. Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, na
ulimi wako watunga hila. Umekaa na kumsengenya ndugu yako, na mwana wa mama
yako umemsingizia. Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza; ukadhani ya kuwa Mimi
ni kama wewe. Walakini nitakukemea; nitayapanga hayo mbele ya macho yako.” Zaburi 50:16-21
Dhabihu ya Mungu ni Roho iliyopondeka na kutubu.
“Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na
kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.” Zaburi 51:17
Anania na mkewe Safira walikufa kwa sababu ya kutokuwa
waaminifu katika kitu kilichowekwa wakfu mbele za Mungu.
“Lakini mtu mmoja jina lake Anania pamoja na
Safira mkewe, aliuza mali, akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye
akijua haya akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. Petro akasema,
Anania, kwanini shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na
kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali
yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani haikuwa katika uwezo wako?
Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu bali
Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa.ofu nyingi ikawapata watu
wote walioyasikia haya. Vijana wakamchukua nje, wakamzika. Hata muda wa saa
tatu baadaye mkewe akaingia naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Petro
akamjibu, niambie mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani
hiyo. Petro akamwambia imekuaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia
miguu yao ya waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.
Mara akaanguka miguuni pake akafa. Wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa,
wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mume wake.”
Matendo
5:1-10
Usituppe neno la Mungu nyuma yako, maana mshahara wa Dhambi
ni Mauti.
“Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi
ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawata urithi ufalme wa Mungu, wala
waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala
watamanio, wala walevi wala watukanaji, wala wanyang’anyi. Na baadhi yenu
mlikuwa watu wa namna hii lakini MLIOSHWA, LAKINI MLITAKASWA, lakini
mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu
wetu.” 1
Wakorintho 6:9-11
Lazima kuoshwa kwa Damu ya Yesu Kristo kwa njia ya TOBA,
hapo ndipo Malango na Milango yako itakapofunguliwa mbele yako.
Lazima Kristo amiliki na kutawala maisha yako, hivyo
hatulegei bali tunapiga mbio katika Maombi; ijapokuwa Utu wetu wa nje unachakaa
lakini Utu wetu wa ndani sharti ufanywe upya siku kwa siku.
Lazima tuyavue matendo yote maovu na Tumvae Kristo.
“Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye
kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika
wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.” 1Petro 1:17
Kwa hiyo tujifunge viuno vya nia zetu tukitumainia kwa
utimilifu ile neema inayoletwa katika ufunuo wake Yesu Kristo. Kama watoto wa
kutii tusijifananishe na tamaa zetu za kwanza za ujinga wetu, bali kama yeye
aliyetuita alivyo mtakatifu, sisi
nasi yatupasa tuwe watakatifu katika mienendo yetu wote. Kwa maana imeandikwa mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Itaendelea.........
Asante Mtumishi wa BWANA wa kutufunulia sili hii ya ufalme wa MUNGU.
ReplyDeleteNEEMA YA YESU KRISTO HIZIDI KUKUFUNIKA KUZIDI KUFANYA KAZI YAKE
ReplyDeleteAmina.
ReplyDelete