SILAHA NANE ZA KUFUNGUA MILANGO NA MALANGO YALIYOFUNGWA MBELE YAKO;
SILAHA YA TATU
USIKATE TAMAA
Usikate tamaa
katika yale unayo yaamini BWANA atakufanyia, kwakuwa Mungu wetu hachelewi wala
hawai isipokuwa anajibu kwa wakati wake. Maisha ya imani yanahitaji mtu mwenye
moyo imara katika Kristo Yesu asiye yumba wala kutetemeshwa. Pia yatupasa
tufahamu kipo kipindi ambacho imani inaweza kutindika, panahitajika maombi
yenye kuinua imani. Maombi haya aliyafanya Yesu kwa Petro ili imani ya Petro
isitindike; “Akasema, Simon, Simon, tazama, shetani amewataka nyinyi apate
kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike;
nawe utakapoongoka uwaimarishe ndugu zako.” Luka 22:31-32
Malango na
Milango yatafunguka pale Mhitaji au Mwombaji atakapo mwomba Mungu aliye hai
pasipo kukata tamaa. Maana maombi endelevu uleta ushindi na baraka endelevu.
Silaha hii ya tatu ni ya muhimu sana kwa mtu wa Mungu. Bwana Yesu kristo
anathibitisha; “Akawaambia mfano ya kwamba imewapasa kumuomba Mungu siku zote, wala
msikate tamaa. Akasema palikua na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala
hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa
akimwendea-endea, akisema, nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda alikataa,
halafu akasema moyoni mwake, ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, lakini
kwakuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa
kunijia daima. Bwana akasema, sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu. Na Mungu
je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni
mvumilivu kwao? Nawaambia atawapatia haki upesi; walakiniatakapokuja mwana wa
Adamu, je! Ataiona imani duniani?” Luka 18:1-8
Na Mungu je!
Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku naye ni mvumilivu
kwao. Nawaambia atawapatia haki upesi lakini atakapokuja mwana wa Adamu je
ataiona Imani duniani? Bwana Yesu Kristo aliuliza swali hili kwa lengo la
kuwajenga wanafunzi wake wasikate tamaa kamwe, wakati wa kuinuliwa ukifika
watainuliwa tu. Maana nyakati za kuburudishwa zimewadia sharti upate
kuburudishwa katika BWANA. Sawasawa na Neno la Mungu lililonenwa katika kinywa
cha nabii Isaya; “Nyakati zako zitakua ni nyakati za kukaa imara; za Wokovu tele na
Hekima na Maarifa. Kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba.” Isaya 33:6
Ndani mwa
Maombi haya; ukiomba na kumsihi Mungu pasipo kukata tamaa, yeye atakuinua na
atazifanya nyakati zako kuwa nyakati za kukaa imara Kiroho na Kimwili. Maana
Malango yako ya Kiuchumi yatakuwa Imara, Kazi ya Mikono yako haitazaa kufakufa
wala kuzaa mapooza. “Watu wa mjini wakamwambia Elisha, angalia, twakusihi, mahali pa mji
huu ni pazuri, kama BWANA wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi
huzaa mapooza. Akasema, nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake.
Wakamletea. Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo
ndani, akasema, BWANA asema hivi, nimeyaponya maji haya, hakutatoka huko tana
kufa wala kuzaa mapooza. Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la
Elisha alilolinena.” 2
Wafalme 2:19-22
Kukata tamaa
kulimfanya Musa apishane na uponyaji wake. Mungu alikusudia kumponya Musa
kigugumizi lakini Musa akawa mkata tamaa maana aliona amezaliwa hivyo, hivyo
hawezi kupona. Maandiko matakatifu yanathibitisha; “Musa akamwambia BWANA, Ee Bwana,
mimi si msemaji tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako, maana
mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito. BWANA akamwambia, Ni nani
aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi,
au mwenye kuona au kuwa kipofu? Si mimi BWANA? Basi sasa enenda nitakuwa pamoja
na kinywa chako, kukufundisha utakalolinena. Akasema, Ee Bwana nakuomba, tuma
kwa mkono wake huyo utakayemtuma. Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Musa, akasema
je! Hayuko Haruni ndugu yako, Mlawi? Najua ya kuwa yeye aweza kusema vizuri.
Pamoja na hayo tazama, anakuja kukulaki naye atakapokuona atafurahi moyoni
mwake. Nawe utasema naye, nakuyatia maneno kinywani mwake, nami nitakuwa pamoja
na kinywa chako na pamoja na kinywa chake na kuwafundisheni mtakayofanya. Naye
atakuwa msemaji wako kwa watu, hata yeye atakuwa mfano wa kinywa kwako, nawe
utakuwa mfano wa Mungu kwake. Nawe utatwaa fimbo hii mkononi mwako, na kwa hiyo utazifanya zile ishara.”
Kutoka 4:10-17
Bwana
anamwambia Musa; Je aliyeumba kinywa cha binadamu ni nani?, Je ni nani
aliyemfanya mtu kuwa bubu?, Ni nani aliyemfanya mtu kuwa kiziwi? Na ni nani
aliyemfanya mtu awe mwenye kuona? Bwana anamwambia Musa nenda, ntakuwa na
kinywa chako, nitakufanya upate kusema vema lakini Musa akasema; Mungu, tuma
mtu mwingine, HASIRA YA BWANA ikawaka juu ya Musa ndipo akamuacha akamtuma
Haruni. Mahali hapa tumejifunza jambo la msingi ambalo Mungu halipendi ni
kukata tamaa. Milango na Malango yatafunguliwa kwa Imani thabiti sio kwa Imani
ya kukata tamaa.
Kwa Imani,
Malango yote yaliyofungwa sharti yafunguliwe. Kristo amekusudia kututendea mema
katika maisha yetu, hakuna atakayezuia maana hakuna awezaye kulizuia kusudi la
Mungu kwako. Simama Imara usikate tamaa wala usife moyo. BWANA anasema katika
kinywa cha nabii Isaya: “Maana BWANA wa Majeshi amekusudia naye ni
nani atakayelibatilisha? Na Mkono wake ulionyoshwa ni nani atakayegeuza nyuma?”
Isaya 14:27
GIDION alikata
tamaa kutokana na ugumu wa maisha waliokuwa wanapitia kama Taifa, Lakini
Israeli alipomlilia BWANA, akamuinua Gidion katika hali ile ya kukata tamaa,
akainuliwa roho yake na kufanyika mlango wa ukombozi kwa wana wa Israeli dhidi
ya majeshi ya Wamidiani. Japo yeye alijiona maskini asiyeweza kutokana na udogo
wa kabila lake lakini kwa imani katika Mungu, aliwapiga Wamidiani kama mtu
mmoja. Maandiko yanathibitisha; “Kisha
wana wa Israel walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA; BWANA akawatia
mikononi mwa Midiani muda wa miaka saba, mkono wa Midiani ulikuwa na nguvu juu
ya Israeli; tena kwa sababu ya Midiani wana wa Israeli walijifanyia hayo
mashimo yaliyo milimani, na hayo mapango, na hizo ngome. Basi ikawa hapo
Israeli walipokuwa wamepanda mashamba, Wamidiani wakakwea, na Waamaleki, na hao
wana wa mashariki wakakwea juu yao, na kuyaharibu hayo maongeo ya nchi hata
ufikapo Gaza, wala hawakuacha katika Israeli riziki ziwazo zote; kondoo wala
ng’ombe, wala punda. Kwa maana walikwea na ng’ombe zao na hema zao, wakaja
mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu nao
waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu. Israeli walitwezwa sana kwa sababu ya
Wamidiani, nao wana wa Israeli wakamlilia BWANA. Kisha ikawa, hapo wana wa Israeli
walipomlilia BWANA kwa sababu ya Midiani, BWANA akamtuma nabii aende kwa hao
wana wa Israeli, naye akawaambia, BWANA yeye Mungu wa Israeli asema hivi, Mimi
niliwaleta ninyi mkwee kutoka Misri, nikawatoa katika nyumba ya utumwa; nami
niliwaokoa na mikono ya Wamisri na mikono ya wote waliokuwa wakiwaonea, nami
niliwafukuza watoke mbele zenu, nami niliwapa ninyi nchi yao kisha niliwaambia,
Mimi ndimi BWANA Mungu wenu, msiiche miungu ya Waamori, ambayo mwaketi katika
nchi yao lakini hamkuitii sauti yangu. Malaika wa BWANA akaenda akaketi
chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri na
mwana wa Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo ili kuificha
machoni pa Wamidiani. Malaika wa BWANA akamtokea, akamwambia, BWANA yu pamoja
nawe, Ee shujaa, Gideoni akamwambia Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi,
mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyo
tuhadithia baba zetu, wakisema, je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri?
Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani. BWANA akamtazama,
akasema, enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli kwa mkono wa Midiani. Je!
Si mimi ninaye kutuma? Akamwambia, Ee Bwana nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani?
Tazama jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye
mdogo katika nyumba ya baba yangu. BWANA akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja
nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja.” Waamuzi 6:1-16
Yako mambo
mengi ya kukatisha tamaa lakini katika Kristo Yesu upo mlango wa kutokea. Usife
moyo bali jitie nguvu katika BWANA. Maombi ya wana wa Israeli yalifungua
Malango na Milango wakainuka tena. Nawe waweza kuinuka tena maana ni tabia ya
Mungu isiyobadilika kuwainua watu wake wanaomlilia mchana na usiku. Maana
maandiko yanathibitisha katika kitabu cha 1Samweli 1:6-9 “BWANA huua, naye hufanya kuwa
hai; hushusha hata kuzimu, tena huleta juu. BWANA hufukarisha mtu, naye
hutajirisha; hushusha chini, tena huinua juu. Humwinua mnyonge kutoka
mavumbini, humpandisha mwitaji kutoka jaani, ili awaketishe pamoja na wakuu,
wakirithi kiti cha enzi cha utukufu. Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, naye
ameuweka ulimwengu juu yake. Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; bali
waovu watanyamazishwa gizani, maana kwa nguvu hakuna atakaye shinda.”
Angalia
Bathromayo mwana wa Timayo, yule kipofu wa kuzaliwa; Alikatishwa tama wakati
alipokuwa anamwita Yesu lakini yeye hakukata tamaa bali aliendelea Kuomba,
akapaza sauti yake kwa nguvu naye Yesu akamwitikia na kumfungua. “Wakafika
Yeriko, hata alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake,
na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa
ameketi kando ya njia. Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza
kupaza sauti yake na kusema, mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu. Na wengi
wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, mwana wa Daudi,
unirehemu. Yesu akasimama akasema mwiteni. Wakamwita Yule kipofu,
wakamwambia, jipe moyo, inuka, anakuita. Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea
Yesu. Yesu akamjibu, akamwambia, wataka nikufanyie nini? Yule kipofu
akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona. Yesu akamwambia, Enenda zako,
imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.” Marko 10:46-52
Naipenda imani
ya
Bartimayo kwa kuwa hakujidharau japo watu walimdharau, walimwona hafai
(rejected man). Mwana wa Mungu katika maisha yako utakutana na watu wenye
dharau, kebehi, viburi, waliojaa masimango na vinywa vya ukaidi. Wataipepeta
imani yako kwa maneno yao ili utindikiwe kiimani, lakini nakutia moyo, vuka mipaka
utakayowekewa mbele yako (GO BEYOND YOUR LIMITATIONS). Wengi;
Watakubeza, Watakusemasema, Watakudharau; Wewe simama katika Imani yako wala
usikate tamaa, Mlango wa Uzima utafunguliwa na Lango la Baraka litafunguliwa.
Mkuu wa Sinagogi alipokea
ufufuo wa mtoto wake aliyekuwa amekufa wakati amemfuata Yesu aje amponye huku
nyuma mtoto akafariki na taarifa ikaja ikisema, usimsumbue mwalimu mtoto
amekwisha kufa.
“Hata Yesu
alipokwisha kuvuka kurudia ng’ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano
mkuu; naye alikuwa kando ya bahari. Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi,
jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake akimsihi sana,
akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu
yake, apate kupona, na kuishi. Akaenda pamoja naye, mkutano mkuu wakamfuata,
wakamsonga-songa… hata alipokuwa katika kunena wakaja watu kutoka kwa yule mkuu
wa sinagogi, wakisema, binti yako amekwishakufa; kwani kuzidi kumsumbua
mwalimu? Lakini Yesu, aliposikia lile neon likinenwa akamwambia mkuu wa
sinagogi, usiogope, amini tu… wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi,
akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu. Alipokwisha kuingia
akawaambia, mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu.
WAKAMCHEKA SANA. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote akamtwaa babaye Yule kijana
na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana.
Akamshika mkono kijana, akamwambia, thalita, kumi; tafsiri yake, mschana,
nakwambia inuka. Mara akasimama yule kijana, akaenda maana alikuwa amepata umri
wa miaka kumi na miwili. MARA WAKAMSHANGAA MSHANGAO MKUU. Akawaonya sana mtu
asijue habari ile; akaamuru apewe chakula.” Marko 5:21-24, 35-43
Pata picha hapa
ya kutokukata tamaa; Huyu mkuu wa sinagogi amemuacha mtoto anaumwa nyumbani
kwake, anamfuata Yesu aje amponye, anakwenda kwenye maombi ghafla analetewa
habari mbaya na ngumu yakuwa mtoto wake amekwisha kufa achana na maombi. Lakini
hata aliporudi nyumbani mwake na Kristo Yesu, alipokelewa na msiba na maombolezo
makuu, bado maombolezo makuu hayakugeuza imani yake kwa Kristo, aliendelea
kuamini Neno la Kristo Yesu. Neno la BWANA linasema; “Msiyakumbuke mambo kwanza, wala
msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama nitatenda neno jipya; sasa litachipuka;
je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito nyikani.” Isaya
43:18-19
Waombolezaji hawakuhitaji
imani ili kuomboleza bali Yairo mkuu wa sinagogi alihitaji imani thabiti ili
binti yake afufuliwe. Yesu Kristo anasema binti amelala wakati waombolezaji wao wanasema
kafa, ndio maana walimcheka sana kwa kuwa aliongea kitu kilichozidi ufahamu na
akili za waombolezaji. Ili mtu wa Mungu asikate tamaa anahitaji kuwa na imani
iliyo juu zaidi ya akili za wanadamu, maana njia za Mungu hazichunguziki na
makusudi yake hayawezi kuzuilika.
“Hata
zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, mahali
hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa, uwaage watu hawa ili waende zao
mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula. Akajibu, akawaambia, Wapeni
ninyi chakula. Wakamwambia je! Twende tukanunue mikate ya dinari mia mbili ili
tuwape kula? Akawaambia mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame. Walipokwisha
kujua wakasema, mitano na samaki wawili. Akawaagiza wawaketishe wote, vikao
vikao, penye majani mabichi. Wakaketi safusafu, hapa mia hapa hamsini. Akaitwaa
ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru,
akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandikie na wale samaki wawili
akawagawia wote. Wakala wote wakashiba. Wakaokota vipande vilivyomegwa vya
kuweza kujaza vikapu kumi na viwili na vipande vya samaki pia.” Marko 35-43
Inawezekana
nawe umezoea kupokelewa na Misiba mwaka kwa mwaka nyumbani mwako. Unapokelewa
na Magonjwa mwaka kwa mwaka uzao hadi uzao, Unapokelewa mwaka kwa mwaka na
Kufeli katika Masomo. Usiogope, Amini tu katika Kristo kwani yote
yanawezekana kwake yeye aaminiye tu na si vinginevyo. “yote yawezekana kwake
aaminiye.” Marko 9:23
Maandiko
matakatifu yanatujenga kiimani yakuwa tusiogope habari mbaya zijapo bali
tujithibitishe katika imani mpaka tutakapoona watesi wetu wameshindwa na
kuwekwa chini ya miguu yetu, sawasawa na Neno la Mungu katika Zaburi 112:7-8
“Hataogopa habari mbaya, moyo wake u Imara ukimtumaini BWANA; Moyo wake
umethibitika hataogopa, HATA AWAONE WATESI WAKE WAMESHINDWA.”
“MJANE WA
SEREPTA”
Angalia Mjane
huyu wa Sarepta akiwa katika hali ya kukata tamaa, hana kitu lakini alipotii
Neno la Mungu, hakika Mungu aligeuza Masikitiko yake kuwa Furaha. Mjane huyu
akiwa anaomba katika hali ngumu, BWANA akamtuma Nabii Eliya alete jibu; “Neno
la Bwana likamjia, kusema, Ondoka, uende Sarepta ulio mji wa Sidoni, ukae huko.
Tazama nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe. Basi akaondoka, akaenda
Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako
akiokota kuni; akamwita, akamwambia, niletee nakuomba, maji kidogo chomboni
nipate kunywa. Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, niletee nakuomba
kipande cha mkate mkononi mwako. Naye akasema, Kama Bwana Mungu wako aiishivyo,
sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa na mafuta kidogo katika chupa; nami
ninaokata kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule
tukafe. Elia akamwambia, usiogope, enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini
unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee, kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao.
Kwakuwa BWANA, Mungu wa Israel, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka,
wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile BWANA atakapoleta mvua juu ya
nchi. Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; nayeye mwenyewe, na Eliya,
na nyumba yake, wakala siku nyingi. Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile
chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa kinywa cha
Eliya.” 1Wafalme 17:8-16
Mjane, anaombwa
atengeneze mkate kwa ajili ya Nabii naye akasema; “Kama BWANA Mungu aishivyo, sina
mkate ila konzi ya unga katika pipa na mafuta kidogo katika chupa nami naokota
kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tule tukafe.”
Imani ya Mama huyu mjane ilikuwa imefika
mwisho, alikuwa hana matumaini tena ya kuishi kutokana na hali halisi
ilivyokuwa katika nchi yake na katika mazingira aliyokuwemo. Ndivyo wakristo
wengi walivyo leo, japo wanasali lakini hawana matumaini tena kutokana na
mapito yao wanayopitia. Na wengi wamepishana na Miujiza yao na Malango yao ya
Baraka yameendelea kufungwa kwa sababu ya kukata tamaa.
Wakristo wengi
wanataka kuona miujiza ikitendeka pasipo wao kuamini kwanza ndipo miujiza
itendeke. Wengi wanashindwa kutoa zaka kamili mbele za Mungu aliye hai
kwasababu ya ugumu wa maisha. Bwana anasema lete zaka kamili, wewe unatoa nusu
au hutoi kabisa, Malango yako na Milango itaendelea kufungwa tu mpaka
utakapolitii Neno la Mungu. Ndiyo maana nabii Eliya mtishibi alitaka mjane huyu
atii agizo la Mungu kwanza la kutengeneza mkate bila kujali kitakachobakia
kwenye pipa lake la unga na kwenye chupa yake ya mafuta. Lakini jambo la ajabu
la ki-Mungu kila alipochota unga haukwisha na kila alivyomimina mafuta
hayakuisha mpaka njaa ilipokoma. Hivyo mtumishi mwaminifu atastawi daima katika
nyua za BWANA. Fahamuni ndugu zangu Mungu hana kigeugeu akisema iwe inakuwa,
akisema ndiyo ni ndiyo. “Kwa kuwa mimi BWANA, sina kigeugeu, ndiyo
maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo. Tokea siku za baba zenu
mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi,
name nitawarudia ninyi, asema BWANA wa Majeshi. Lakini ninyi mwasema turudi kwa
namna gani? Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini
ninyi mwasema, tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu, ninyi
mmelaaniwa kwa laana kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu
kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya
mbinguni, na kuwamwagieni Baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami
kwaajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala
mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba,
asema BWANA wa majeshi. Na mataifa yote watawiteni heri; maana mtakuwa nchi ya
kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.” Malaki 3:6-12
Pili, Acha
kujidharau wala usidharau ulichonacho, Mungu aliye hai yeye atafanya njia
mahali pasipo kuwa na njia, ndiyo kazi yake. Eliya Nabii akamwambia
Mjane, Usiogope, nenda uakanifanyie mkate, kwanza ukaniletee nile ndipo
ujifanyie wewe na mwanao.
“Kwa kuwa Bwana
Mungu wa Israeli asema hivi lile pipa la unga halitapunguka wala ile chupa ya
mafuta haitaisha hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi.” Mjane
yule akafanya kama mtumishi wa Mungu Eliya alivyosema; Maana yake aliamini na
kukata tamaa kukaondoka, hakika aliona maajabu. Usikate tamaa, Yesu Kristo yupo
atakufungulia Malango na Milango yako; Amesema, atatenda tu maana kwa kusudi
hili amedhihirishwa ili azivunje kazi za Ibilisi. Piga mbio katika Maombi,
majibu yako yapo.
Dada huyu
aliambiwa Hospital kuwa hatazaa kwasababu tumbo lake limejaa mauvimbe makubwa
ambalo lazima afanyiwe upasuaji atolewe kizazi; lakini tarehe 04/08/2013,
aliponijia akanieleza yaliyompata ndipo nikamwambia “Usiogope, Kuzaa utazaa maana Kristo atafanya njia mahali pasipo kuwa
na njia” Nikampa andiko;
“Akajibu
akasema, kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbunguni, litang’olewa.” Mathayo 15:13
Baada ya hapo,
nikamfanyia Maombi, mwezi uliofuata akapata mimba, akaendelea kuja kwenye
maombi maana nilimueleza mfano wa kuku wa kienyeji, anapotaka kutotoa vifaranga
utamkuta masaa yote amelala juu ya mayai yake mpaka siku ile anapototoa
vifaranga vyake. Nawe kaa kwenye Maombi, naye kweli alikaa kwenye maombi; Mpaka
anakwenda kujifungua, anasema Mchungaji Niombee maombi, sasa amepata mtoto wa
kike anaitwa Sarah na tarehe 25/05/2013 tulimbariki huyu mtoto akiwa na
siku 14 tu tangu azaliwe; Jina la Bwana Libarikiwe.
Amina mtumishi wa Bwana umeniponya na malango na milango imefunguka sasa
ReplyDeleteAmina mtumishi wa Bwana umeniponya na malango na milango imefunguka sasa
ReplyDelete