SILAHA NANE ZA KUFUNGUA MILANGO NA MALANGO YALIYOFUNGWA MBELE YAKO;
SILAHA YA PILI
(ii) UWE HODARI TU
Silaha hii ni ya muhimu sana katika maombi yetu ya kufungua milango
na malango maana mwenye imani itendayo kazi sharti awe hodari katika BWANA hata
kama kuna magumu mbele yako unayapitia. Njia ya kuyashinda hayo ni kuwa hodari
tu maana uhodari ndio unao fungua Milango na Malango. Hatukupewa roho ya woga
bali ya uweza na nguvu katika Kristo Yesu. “Uwe hodari tu na ushujaa mwingi uangalie
kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiache
kwenda mkono wa kuume au wa kushoto upate kubarikiwa sana kila uendako.” Yoshua
1:7
Tunajifunza kwa
mtume Petro alizama kwa kukosa imani thabiti, alipoona hofu moyoni mwake,
akapoteza mwelekeo wa kiimani, akazama. Hofu ikiwa ndani mwa mkristo
utapoteza uwezo wa kumiliki na kutawala. Maana hatuwezi kumiliki pasipo imani
thabiti katika Mungu. “…Petro akajibu akasema, Bwana, ikiwa ni
wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema njoo. Petro akashuka chomboni,
akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona upepo
akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu
akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona
uliona shaka?...” Mathayo 14:22-32
Milango na
Malango vitafunguliwa pale tunapokuwa na moyo wa ushujaa na uhodari. Watu wa
Imani sharti watoke waombe kwa nguvu
zenye kuangusha ngome. Ukiwa na hofu na mashaka uwezi kusimama mbele ya maadui
zako ukawashinda. “Bwana Mungu ndiye atakayevuka mbele yako; atawaangamiza mataifa haya
mbele yako nawe utamiliki.” Kumbukumbu 31:3
Mbele yetu yuko
Kristo Yesu, naye anasema atatufungulia milango na malango, na hao adui zetu
wataangamizwa. Walio inuka juu yako watatiwa mkononi mwako na utayamiliki
Malango na Milango ya adui zako. “Iweni hodari na moyo wa ushujaa; msiogope
wala msihofu kwa maana Bwana Mungu wako yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe
hatakupungukia wala kukuacha.” Kumbukumbu 31:6
“Bwana ni nuru
yangu na wokovu wangu nimuogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu nimuhofu
nani? Watenda mabaya waliponikaribia wanile nyama yangu; watesi wangu na adui
zangu walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami, moyo wangu
hautaogopa vita vijaponitokea; hata hapo nitatumaini.” Zaburi 27:1-3
Imani pasipo
shaka ndiyo inayofungua malango na milango hivyo mwombaji sharti uwe na imani isiyo
na shaka. “Yesu akajibu akawaambia, amini nawaambia; mkiwa na Imani, msipokuwa na
shaka, mtafanya si hilo la mtini tu lakini hata mkiuambia mlima huu ng’oka
ukatupwe baharini itatendeka. Na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini,
mtapokea.” Mathayo 21:21-22
Milango na
Malango yaliyofungwa yatafunguliwa kwa kuwa na moyo mkuu wa Imani isiyokuwa na
shaka ndani mwake. Nasi tukiomba pasipo shaka yoyote hakika tutashinda. “Ila
aombe kwa Imani pasipo shaka yoyote moyoni maana mwenye shaka nikama wimbi la
bahari lililochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama
yule asidhani atapokea kitu kwa Bwana. Mtu wa nia mbili husitasita katika njia
zake zote.” Yakobo 1:6-8
Mtu mwenye
mashaka, Mwenye hofu, Mtu mwoga na Mtu wa wasiwasi, ASIDHANI ATAPOKEA KITU
KUTOKA KWA BWANA. Malango ya wengi yamefungwa mpaka sasa kwa sababu sio Hodari.
Lazima mtu wa Mungu uwe Hodari tunajifunza kwa mfano wa Daudi alimshinda
Goliathi sio kwa ujuzi wa vita bali kwa
Uhodari katika Mungu aliye hai. Hata mfalme Sauli alipomwambia Daudi huwezi
kupigana na Mfilisti huyu maana amekuwa mtu wa vita tangu utotoni mwake. Lakini
Daudi kwa imani alisema naweza kumpiga mfilisti huyu.
“Daudi akamwambia Sauli, asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi
mtumishimwako nitakwenda kupigana na mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi
uwezi kumwendea mfilisti huyu upigane naye maana wewe u kijana tu; na huyu ni
mtu wa vita tangu ujana wake. 1Samweli 17:32-33
Angalia Gidion
ilibidi Mungu amwambie apunguze katika jeshi lake watu wote wenye hofu na
wasiwasi, toka jeshi la askari thelathini na mbili elfu (32,000) mpaka askari
mia tatu (300) walio Hodari tu. ”Kisha Yerubaali yaani Gidion na watu wote
waliokuwa pamoja nae wakaondoka na mapema wakapiga kambi yao karibu na kijito
cha Harod na kambi ya midiani ilikua upande wao wa kaskazini karibu na milima
wa more bondeni. Bwana akamwambia Gidion, watu hawa walio pamoja nawe ni wengi
mno hata nikawatie kwa Wamidiani katika mikono yao wasije Israeli wakajivuna
juu yangu wakisema mkono wangu mwenyewe ndio ulioniokoa. Basi sasa enda tangaza
habari masikioni mwa watu hawa na kusema, mtu awaye yeyote anayeogopa na
kutetemeka na arudi aondoke katika mlima wa Gidon Gileadi, ndipo watu ishirini
na mbili elfu wakarudi katika watu hao wakabaki watu elfu kumi. Bwana
akamwambia Gidion hata sasa watu hawa ni wengi mno, uwalete chini majini name
nitawajaribu huko kwaajili yako kasha itakuwa ya kwamba yule nitakaye kuambia
huyu atakwenda pamoja nawe, ndipo atakwenda pamoja nawe na mtu yule
nitakayekuambia huyu hatakwenda pamoja nawe basi mtu huyo hatakwenda. Basi
akawaleta watu chini majini, Bwana akamwambia Gidion kila mtu atakaye yalamba
maji kwa ulimi wake kama vile alambavyo mbwa huyo utamuweka kando kadhalika
kila mtu apigaye mago ti kunywa na hesabu ya hao waliokunywa kwa kulambalamba
wakipeleka mkono kinywani ilikua watu mia tatu bali watu wengine wote walipiga
magoti kunywa maji. Bwana akamwambia Gidion kwa watu hawa mia tatu walioyalamba
maji nitawaokoa name nitawatia wamidiani katika mikono yao, lakini watu hawa
wote wengine na waende zao kila mtu mahali pake.” Waamuzi 7:1-7
Malango yako
yatafunguliwa kwa Imani thabiti sio kwa wingi wa maneno, Yesu akamwambia Petro,
Mbona umeona shaka moyoni mwako? Kikwazo na kizuizi kikuu ni mashaka
hivyo ondoa mashaka na uwe hodari katika BWANA. “Si kwa uwezo wala si kwa nguvu
bali kwa roho yangu asema BWANA. Nani wewe ee mlima mkubwa mbele ya Zerubabeli
utakua nchi tambarare naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na
vigelegele vya neeme ilikalie.”
Zekaria 4:6-7
Casino in New York - Mapyro
ReplyDeleteCasino 김포 출장마사지 is 화성 출장샵 a non-smoking casino 시흥 출장안마 located in Yonkers, NY. The casino is a non-smoking hotel and not a full-service casino. In the 고양 출장안마 photo, you can 양산 출장안마 see