SILAHA
NANE ZA KUFUNGUA MILANGO NA MALANGO YALIYOFUNGWA MBELE YAKO;
SILAHA YA NANE
UWE MVUMILIVU;
“Uvumilivu” (Greek makrothumia) means patience without reaction (by
implication without reaction, long suffering) ikiwa na maana ya ustahimivu; si
mwepesi wa hasira wala kukata tamaa. Maandiko matakatifu yanatuelekeza
tumwendee BWANA kwa wito wetu. Tukiwa tumejivika uvumulivu. “Kwa
unyenyekevu wote na upole, kwa uvumulivu, mkichukuliana katika upendo.”
Waefeso 4:2
Maisha
ya mwanadamu yana mapito mengi sharti avumilie katika BWANA. Pasipo Uvumilivu,
hauwezi kupokea jibu toka kwa BWANA kwa kuwa yeye hachelewi wala hawai
isipokuwa anajibu kwa wakati wake. Hivyo maisha ya Imani yanahitaji Uvumilivu. “Kwa
hiyo ndugu, vumilieni hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya
nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya
kwanza naya mwisho. Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja
kwake BWANA kunakaribia. Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni,
mwamuzi amesimama mbele ya milango. Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina
la BWANA, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. Angalieni,
twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona
mwisho wa BWANA ya kwamba BWANA ni mwingi wa rehema, mwenye huruma. Lakini
zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape wala kwa mbingu wala kwa nchi, wala kwa kiapo kinginecho chote, bali ndiyo yenu
iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.” Yakobo 5:7-12
Mmesikia
habari ya uvumulivu wa Ayubu, inasemekana zaidi ya miaka kumi na saba Ayubu
alikuwa kwenye hali ya dhiki nzito yenye msiba na magonjwa lakini katika mambo
yote hakumkufulu Mungu wala kuwaza kwa upumbavu. Maandiko yanathibitisha; “Katika
mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.”
Ayubu 1:22
Kutokana
na uvumilivu basi hivyo BWANA akaubarikia mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake.
Akawa na mali mengi kondoo kumi na nne elfu, ngamia elfu sita na jozi ya
ng’ombe elfu na punda wake elfu pia BWANA alimbariki Ayubu kwa kumwinulia uzao
tena akawa wana waume saba na binti watatu. Wana wa Mungu yatupasa tusizimie
roho bali tumtumaini BWANA kwa uvumilivu, “Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki
bali njia ya wasio haki itapotea.” Zaburi 1:6
Eliya
alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe
na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. Akaomba
tena mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake. Maombi ni lazima
yaambatane na Uvumilivu. Bwana anaposema atatenda ni lazima atende kwa wakati. “Na
mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni
mwaminifu.” Waebrania 10:23
Hivyo
Mungu wetu hana kigeugeu, yeye akisema itakuwa lazima iwe tu. Ibrahimu
alivumilia miaka ishirini na mitano kabla ya kumpata Isaka kwa Sara mkewe. “Bwana
akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema. Sara akapata
mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa
na Mungu. Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye
Sara alimzalia. Ibrahimu akamtahiri Isaka mwanawe alipokuwa mwenye siku nane,
kama Mungu alivyomwamuru. Naye
Ibrahimu alikuwa mtu wa miaka mia, alipozaliwa mwana wake Isaka. Sara akasema,
Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami. akasema,
n’nani angemwambia Ibrahimu, Sara
atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.” Mwanzo 21:1-7
BWANA
alimpa ahadi lakini ilipita miaka ishirini na mitano ya uvumilivu wa Kiimani. BWANA
akageuza huzuni ya Sara kuwa kicheko, akazaliwa Isaka. Nawe Vumilia katika
BWANA, Isaka wako atazaliwa pale lango lako
litakapo funguliwa. “BWANA
ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwahiyo nafsi imtafutayo.” Maombolezo 3:25
Umkabidhi
BWANA njia zako pia umtumaini yeye naye atafanya. Ukae kimya mbele za BWANA
nawe umngojee kwa saburi naye atakutendea pale usipozimia roho.
ISAKA naye alivumilia katika BWANA miaka ishirini akiomba kwa
ajili ya mke wake Rebeka alikuwa tasa, mwisho wakazaliwa watoto mapacha.
Isaka alioa Rebeka akiwa na umri wa miaka arobaini na mke wake alizaa Isaka
alipokuwa ametimiza miaka sitini. “Na hivi ndivyo vizazi vya Isaka, mwana wa
Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka. Isaka akawa mwenye miaka arobaini alipomtwaa
Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa
mke wake. Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye
BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba, watoto wakashindana
tumboni mwake. Naye akasema, ikiwa ni
hivi, kuishi kwa nifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA. BWANA akamwambia, Mataifa
mawili yako tumboni mwako, na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni
mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko
la
pili,
na mkubwa atamtumikia mdogo. Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo
tumboni mwake. Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la
nywele. Wakamwita jina lake Esau. Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake
unamshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka
sitini mkewe alipowazaa.” Mwanzo 25:19-26
Yusufu alivumilia mbele za BWANA muda wa miaka kumi na mitatu
kabla ya ndoto zake zikatimizwa. “Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu,
aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu
zake, naye alikuwa kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa
baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari mbaya.” Mwanzo 37:2
Yusufu
aliyekuwa na miaka kumi na saba alikuwa akichunga kondoo, akaota ndoto
akawajulisha ndugu zake, wakazidi kumchukia wakasema tumuue tuone ndoto zake
zitakuwaje. Lengo la ndugu zake Yusufu ilikuwa ni kuua maono na ndoto
zisitimie, maadamu mbeba hayo maono alikuwa ni Yusufu ilibidi wapange kumuua na
hayo maono. Maandiko yanathibitisha yakisema; “Wakamwona toka mbali na kabla
hajawakaribia wakafanya shauri juu yake ili wamwue. Wakasemezana wao kwa wao,
tazama, Yule bwana ndoto anakuja. Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika
birika mojawapo, nasi tutasema mnyama mkali amemla; KISHA TUTONA ZITAKUWAJE
NDOTO ZAKE.” Mwanzo 37:18-19
Atukuzwe
Mungu asiyeshindwa na jambo lolote, anayetuwazia mema, anayetamka mwisho wetu
kabla ya mwanzo. Maana yake kwa imani lazima uuone mwisho wako kabla ya mwanzo
ndipo utaweza kuvumilia. Maana; “Mungu si mtu aseme uongo; wala si
mwanadamu, ajute; iwapo amesema hatalitenda? Iwapo amenena hatafikiliza?”
Hesabu 23:19
Sifa
ya Mungu ni thabiti katika kauli zake. Mungu si yule ambaye haaminiki, mwenye
kigeugeu au mwenye kubadilika lakini kwa asili yake ni mwaminifu katika ahadi
zake na kauli zake. Pamoja na kuuzwa ili ndoto za Yusufu zisitimie, Mungu alimfungulia
Milango na Malango baada ya kukaa ndani ya gereza miaka miwili mizima ikiwa
inahitimisha miaka kumi na tatu ya kusubilia jibu na wakati wa Mungu kuyatimiza
aliyosema kwake. Tunajifunza uvumilivu wa Yusufu na mapito yake maana kila
alikopita BWANA alikuwa pamoja naye, ndio maana hata kwa mke wa Potifa
alionyesha kumjali Mungu na kumtumainia kuliko ahadi za muda kitambo tu.
Akasema; “Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu
chochote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe NIFANYEJE UBAYA HUU MKUBWA NIMKOSE
MUNGU?” Mwanzo 39:9
Uaminifu
wa Yusufu kwa Mungu ulimfanya ashinde jaribu la kuanguka katika tanzi ya uzinzi
na uasherati. Tunajifunza kwa Yusufu alivyokimbia dhambi hii nasi yatupasa
kuiga mfano huu kwa kukimbia dhambi ya uzinzi. Dhambi hii imewaangusha wengi na
wamepoteza mwelekeo wa kiimani na uwepo wa Mungu. Vijana kwa wazee wanaanguka
katika dhambi hii. Na wengi wao wameponzwa na ushawishi wa wenye dhambi kama
mke wa Potifa, badala ya kukimbia kama
Yusufu wameingia katika majadiliano mwisho wake wameanguka. “Mwanangu,
wenye dhambi wakikushawishi, wewe usikubali. Mwanangu, usiende njiani pamoja
nao; uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.” Mithali 1:10, 15
Baada
ya uvumilivu na ushindi wa Yusufu, BWANA alimwinua, tunaona katika maandiko
matakatifu jinsi Mungu alivyomkamata Farao kukawa ndio mwanzo wa kuinuliwa
Yusufu na wana wa Israeli. “Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka
juu ya nchi yote ya Misri. Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake,
akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa
dhahabu shingoni mwake. Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo.
Na watu wakapiga kelele mbele yake,
pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri. Farao akamwambia
Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika
nchi yote ya Misri. Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi,
binti Potifera, kuhani wa Oni, kuwa mkewe Yusufu akaenda huko na huko katika
nchi yote ya Misri. Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama
mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akapita
katika nchi nyote ya Misri.” Mwanzo 41:41-46
Pia
tunajifunza kwa Musa alipokataa kuitwa mtoto
wa binti Farao, alikuwa na umri wa miaka AROBAINI. Lakini alivumilia
miaka arobaini akichunga mifugo ya Yethro na akavumilia safari ya miaka
arobaini jangwani na wana wa Israeli kuelekea Kanani. Maandiko matakatifu
yanathibitisha; “Umri wake ulipopata kama miaka arobaini akaazimu moyoni mwake kwenda
kuwatazama ndugu zake Waisraeli. Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamtetea,
akamlipia kisasi yule aliyekuwa akionewa, akampiga huyo Mmisri. Alidhani kwamba
ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokovu kwa mkono wake, lakini
hawakufahamu. Siku ya pili yake akawatokea walipokuwa wakishindana, akataka
kuwapatanisha, akasema, Enyi bwana zangu, ninyi ni ndugu. Mbona mnadhulumiana?
Lakini yeye aliyemdhulumu mwenziwe akamsukumia mbali, akisema, ni nani
aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama
ulivyomwua yule Mmisri jana? Musa akakimbia kwa neno hilo, akakaa hali ya ugeni
katika nchi ya Midiani, akazaa wana wawili huko. Hata miaka arobaini
ilipotimia, malaika wa Bwana akamtokea katika jangwa la mlima wa Sinai katika
mwali wa moto, kijitini. Musa alipouona akastaajabia maono yale, na
alipokaribia ili atazame, sauti ya Bwana ikamjia, Mimi ni Mungu wa baba zako,
Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akatetemka
asithubutu kutazama. Bwana akamwambia, vua viatu miguuni mwako, kwa maana
mahali hapa unaposimama ni nchi takatifu. Yakini nimeona mateso ya watu wangu
waliomo Misri, nimesikia kuugua kwao, nami nimeshuka niwatoe. Basi sasa,
nitakutuma mpaka Misri. Musa huyo waliyemkataa, wakisema, Ni nani aliyekuweka
kuwa mkuu na mwamuzi? Ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mkuu na mkombozi, kwa
mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kijiti. Huyo ndiye aliyewatoa,
akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika bahari ya Shamu, na
katika jangwa muda wa miaka arobaini. Musa huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli,
Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi, msikieni
yeye. Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika
aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye
aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi. Mtu huyo baba zetu hawakutaka kumtii, bali
wakamsukumia mbali, na kwa mioyo yao wakarejea Misri, wakamwambia Haruni,
Tufanyie miungu, watakaotutangulia; maana huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya
Misri, hatujui lililompata. Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa
sanamu ile, wakafurahia kazi za mikono yao. Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili
waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, je!
Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka, Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya
Israeli? Nanyi mlichukua hema ya Moleki, na nyota za mungu wenu Refani, Sanamu mlizozifanya
ili kuziabudu; nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli.” Matendo
1:23-43
Pasipo
Uvumilivu tutapishana na kalenda ya Mungu, lakini tukivumilia katika BWANA
tutavuna mema. “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kishinda, kwa
yeye aliyetupenda.” Warumi 8:37
Tutashinda
yote tusipovunjika moyo; bali tujinyenyekeze kwa Mungu atatukweza kwa wakati
wake. “Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki
aondoshwe milele.” Zaburi 55:22
DAUDI alivumilia miaka kumi na tatu. Na wakati ulipofika alipokuwa
na umri wa miaka thelathini akawa mfalme wa Israeli. Amenusulika kuuawa na
Sauli mfalme mara ishirini na tano; lakini Daudi daima aliomba akisema; “Ee
Mungu, uniokoe, Ee BWANA, unisaidie hima. Warudishwe nyuma , watahayarishwe,
wapendezwao na shari yangu. Warudi nyuma na iwe aibu yao, wanaosema Ewe! Ewe!
Washangilie, wakufurahie, wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako waseme daima,
Atukuzwe Mungu. Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka.
Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee BWANA, usikawie.” Zaburi 70:1-5
Maombi
haya yanafungua Malango na Milango ndani mwa Uvumilivu wa Kiimani. Mtu mwenye Imani sharti avumilie
akidumu katika maombi, maana yuko Jehova aliye hai atasimama. Maandiko
matakatifu yanasema; “Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu
hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.” Ayubu 19:25
Mtetezi
wetu hatimaye atasimama juu ya nchi atafuta kila chozi.
“Heri
wakaao nyumbani mwako, Wanakuhimidi daima. Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako,
Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake. Wakipita kati ya bonde la Vilio,
hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulivika Baraka.” Zaburi 84:4-6
Yesu
atawalipa watu wake wala hatawaacha bali katika taabu atawatoa. Mateso
ya mwenye haki ni mengi sana lakini BWANA humponya nayo yote.