Imeelezwa kuwa katika kongamano la siku tisini watu
mbalimbali waliokuwa na matatizo na shida mbalimbali wamefunguliwa na kuwekwa
huru na wengi wameshuhudia jinsi Mungu alivyo wafungua katika taabu zao.
Akifundisha katika kongamano hilo mchungaji kiongozi wa
kanisa la EAGT City Center Mchungaji Florian Katunzi alisema kuwa katika
kongamano hilo kuna maombi ndani mwa maombi ambao kuna vipengele mbalimbali na kwa wiki hiii
inahitimika na kiengele cha kumiliki na kutawala.