Kama ambavyo mtumishi wa Mungu Ayubu alivyosema hivyo ndivyo wana EAGT CITY CENTRE TUNASEMA LEO!!!
Ama kwa hakika tumemuona Mungu akifanya na ataendelea kufanya maana tulikotoka ni mbali kuliko tunakokwenda...!!!
Kwa takribani miaka mitano sasa tumekuwa tukiabudu katika Viwanja vya Maonesho vya Mwl Julius Kambarage Nyerere ( Sabababa) huku tukiwa na shauku ya kutaka kumiliki eneo letu ambapo tutajenga nyumba ya kumuabudu Mungu wetu pasipo bughudha.
Hakika Mungu amejibu maombi yetu kwa kutupa eneo katika eneo la MTONI MTONGANII karibu kabisa na Daraja la Reli ya Tazara .....
Eneo hili jipya lina uwezo wa kuchukua takriban waumini 2,500 , na kuna mpango endelevu ambao utawezesha upanuzi wa eneo hili hata kuweza kuchukua jumla ya waumini 7,200. Na hapo ndipo EAGT City Centre itadumu.
![]() |
Kikosi cha Bendi ya Jeshi la Polisi Tanzania kikiongoza maandamano kuelekea katika kanisa jipya .. |
![]() |
Umati mkubwa wa waumini wa kanisa la EAGT CITY CENTER ukiongozwa na Mchungaji Florian Katunzi. |
![]() |
MChungaji Katunzi akiongoza msafara kuelekea lilipo kanisa jipya eneo la MTONI MTONGANI jirani na reli ya Tazara. |
![]() |
Mwandishi na mtangazaji wa Radio WAPO Angelina Lukindo akifanya kazi yake wakati wa masafara.. |
![]() |
Viongozi wa kanisa wakiwa wametangulia mbele ili kuhakikisha mambo yanakwenda kwa utaratibu. |
![]() |
Waumini wakiwa wamebeba viti ambavyo watatumia katika kanisa hili jipya. |
![]() |
Mbeba maono na Mchungaji wa kanisa hili akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kanisa hili. |
![]() |
Viongozi mbalimbali waliokuwepo katika zoezi hilo |
![]() |
Umati wa waumini wakiwa ndani ya kanisa. |
Ni kweli Mungu wetu hujibu maombi kwa wakati wake na wakati ukifika hakuna wa kuzuia....halleluyaaa!!
ReplyDeleteNdio Bishop Katunzi,Mungu atukuzwe sana,na awape nguvu ya kufanikiwa zaiidi ya hapo mulipo sasa.
DeleteNinayabariki MAONO ya Mungu uliyoyabeba. EAGT CITY CENTRE idumu melele
AMEN,AMEN,AMEN.
Ubarikiwe sana Mchungaji! Mungu hamtupi mjaliwa wake
ReplyDelete