Friday, 28 November 2014

Unaweza jiuliza ni kwa nini namuita mwanamke wa shoka.....



Endelea kufuatilia blogu hii pendwa na utakubaliana na mimi siku nitakayokupa sababu zisizopungua KUMI zitakazokufanya ukubaliane na mimi.

Picha mbalimbali za Mama Mchungaji Rachel Katunzi akiwa katika huduma.






WANAWAKE wa injili (WWI) wa kanisa la EAGT City Centre lililopo
chini ya Mtumishi wa Mungu Mchungaji Florian Katunzi na mama yetu mlezi Rachel Katunzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jimbo la Temeke, katika kutimiza makusudi matano ya mwanawake ndani ya       kanisa,tumejipanga kumtegemeza Mchungaji wa kanisa hili FLORIAN KATUNZI  kwa kununua GARI aina ya LANDCRUZER V8 pamoja na kuandaa chakula cha hisani ambacho kinalenga kutumika kukusanya fedha ambazo zitatumika katika ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Mungu.

Tukio hili la kihistoria na lililojaa baraka ndani yake linatarajiwa kufanyika siku  tarehe 7 Desemba Mwaka huu  katika viwanja vya maonesho sabasaba na mgeni rasmi atakuwa Mh. Tunu Pinda.

Wazo hili limetokana na makubaliano ya wanawake wapatao 360 ambao ni wanachama wa kurugenzi ya ndani ya kanisa letu

Unaweza jiuliza wanawezaje kufanikisha hili!

Ukweli ni kwamba wanawake hawa walishirikiana katika kutoa ahadi mbalimbali pamoja na kadi za michango  ambazo zililenga ukusanyaji wa fedha ambazo ndizo zitakazotumika kununua gari hii, pia kuandaa chakula hiki cha hisani.

Lakini wanawake hawa hawakutaka kuchukua baraka hii peke yao bali walishirikisha kanisa kwa ujumla na michango hii bado inaendelea kukusanywa na tutazidi kujulishana kadri siku zinavyokwenda…

Najua unatamani kujua makudi haya matano ya mwanamke ndani ya kanisa ambayo yanatoa msingi na wazo madhubuti la kumtegemeza mtumishi wa Mungu.

KUSUDI LA KWANZA.
 -  KULETEA NYUMBA BARAKA.

* Kuombea Mungu aibariki na wote waliomo waokoke na wale waliokoka waendelee kukua kiroho.
* Kuwa mfano mzuri nyumbani.
* Kuwaleta wote na jamaa zake kwa Yesu
* Kuhudhuria ibada na mikutano yote ya WWI ili ajifunze.
* Kutekeleza nyumbani yote aliyojifunza kwemye ibada na mikutano ya WWI
* Kusimamia ibada za nyumbani.

KUSUDI LA PILI.
  -   KULILETEA KANISA BARAKA.

*Kuombea likue kiroho na mafanikio katika mahitaji yake.
* Kulitegemeza kwa sadaka zetu za pesa na uhusika katika shughuli za kanisa na kueneza injili.
*  Kulisaidia kununua viti, mikeka,meza n.k. kuwa walimu wa shule za Jumapili na kushuhudia.
* Kuhudhuria kwa uaminifu tutakuwa tunaliletea Baraka kanisa letu.

KUSUDI LA TATU
 - KUMLETEA MCHUNGAJI BARAKA.

* Kumwombea mchungaji na mke wake katika huduma
* Kuombea familia ya mchungaji kwa ajili ya mahitaji.
* KUMTEGEMEZA
- KWA CHAKULA AMBACHO HAKIJAPIKWA NA VITU MBALIMBALI       WALAO MARA MOJA KWA MWEZI
-KWA MAVAZI YA MCHUNGAJI NA FAMILIA YAKE WATOTO NA MKE
-KWA KUTOA FUNGU LA KUMI KWA UAMINIFU KANISANI.
* KUMSAIDIA
- KWA KUMPA NAULI ANAPIKWENDA KWENYE MIKUTANO YA  WACHUNGAJI INAPOWEZEKANA NA MAHITAJI MENGINE.

-KUMHESHIMU
-  kumheshimu mchungaji kama mtumishi wa Mungu anayesimamia kundi. Wathesalonike 5:12-13

KUSUDI LA NNE

*Kuuletea mji Baraka
* kuwaombea watu wa mji ili waokolewe
*Kuishi maisha matakatifu ambayo kwayo watu wanaweza kuvutwa kwa Yesu Kristo  bila hata neon au bila kuhubiriwa.
* Kwa kuwashuhudia watu na kuwakaribisha kanisani.

KUSUDI LA TANO

*Kukiletea chuo cha biblia Baraka
* Kwa kukiombea kwa ajili ya mahitaji yake
*kuwaombea walimu na wanafunzi
*Kukitegemeza kwa chakula na vitu vingine kama vyombo n.k
*Kukisaidia au kumsaidia mwanafunzi wa chuo cha Biblia kama ada na nauli yake.

Mpenzi wa blog hii, ni matumaini yangu ya kuwa mara baada ya kusoma makusudi hayo utatambua wanawake hawa wapo makini na wanafuata matakwa na makudi yao katika kanisa.

Lakini napenda utambue ya kuwa chama hiki cha WWI ni chama huru ambacho kinakaribisha wanawake wote waliompokea Yesu kuwa BWANA  na mwokozi wa maisha yao sanjari na kuabudu katika kanisa la mahala pamoja.

Naamini ya kuwa umeelewa chanzo na dhima halisi la wazo hili  na tunaamini utaungana nasi katika kufanikisha hili kwa fedha na maombi pia.

Mwisho napenda uwajue viongozi wetu ambao pia kama utaguswa unaweza kutuma mchango wako kupitia mitandao ya simu.

M/KITI- CHRISTINA MGAYA
MAKAMU M/KITI- GRACE MASEBO- 0717 332922
KATIBU- IMANI MBAGA
MTUNZA HAZINA- ESTER MPEPO

Je! Utapenda kujua ni gharama kiasi gani zitatumika katika ununuzi wa gari sanjari na ujenzi wa nyumba????????????

ENDELEA KUFUATA NAMI KATIKA BLOGU YETU PENDWA.
MUNGU AWABARIKI.



.



Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu unayefuatilia kwa ukaribu makala haya. Nakusalimu katika jina la BWANA wetu Yesu Kristo.

Bado tunaendea na mfululizo wa makala haya ambayo yanakujia kila wiki na usisite kuuliza maswali endapo hutaelewa kipengele chochote katika mfululizo huu.


Wiki jana nilikufundisha juu ya aina za funguo za kufungua malango na milango, ambapo nilikwambia zipo aina tano na nikakufundisha funguo mbili kati ya hizo. Funguo ya kwanza ilikuwa ni Neno la Mungu na ya pili ilikuwa ni Imani.

Nilikwambia ya kuwa neno la Mungu ni kauli ya Mungu yenye Mamlaka, Uweza na Nguvu za ki-Mungu zenye kuleta mageuzi ya kiroho na kimwili. Pia nilikuonesha maandiko ambayo yanathibitisha hilo.

Katika kipengele cha imani ambacho ndicho tunachoendela nacho siku ya leo, nilikufundisha maana halisi ya imani na nilisema  Imani ni tendo la utii katika kuitikia kile Mungu alichokisema katika Neno lake.

Nilizama zaidi  na kukuonesha msingi wa kuwa na imani kwa Mungu ambao uko katika kweli tatu zilizobebwa na maana halisi ya Asili ya Mungu wetu. Kweli hizo ni  Hawezi Kubadilika, Hawezi Kushindwa na Hawezi Kudanganywa.

Endelea……….

Malango na Milango ni sharti ifunguliwe kwa Imani; sawasawa na Neno la Mungu. Kwa Imani tunalegeza viuno vya wafalme, Kwa Imani tunalegeza mafungo na vifungo vilivyowafunga watu wa Mungu. Kwa Imani tunafungua Malango na Milango iliyofungwa mbele yetu.

 “Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.” Isaya 10:27

Kila mzigo uliotwishwa katika nafsi yako unaondolewa begani mwako maana uwezo wake Kristo Yesu sasa umedhihirishwa ili kazi zote za yule mwovu shetani zivunjwe ndani mwa imani.

“Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo, nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji.” Zekaria 10:2

Imani ni Ufunguo wa kufungua Malango na  Milango, tunaona Senakeribu analeta majeshi yake akiwa ameazimia kupiga watu wa Mungu na kuwatawala. Mfalme Hezekia  akasema na watu wake ili apate wakuwajenga Kiimani.

 “Iweni hodari, na wa moyo mkuu, msiogope, wala msifadhaike kwa sababu ya mfalme wa Ashuru, wala kwa majeshi yote walio pamoja naye; kwa maana yupo mkuu pamoja nasi kuliko aliye pamoja naye, kwake upo mkono wa mwili, ila kwetu yupo BWANA, Mungu wetu, kutusaidia, na kutupigania mapigano yetu. Na watu wakayategemea maneno ya Hezekia mfalme wa Ashuru.” 2Mambo ya Nyakati 32:7-8

Adui anakuja na neno lenye kuogofya ili kuifisha Imani yako, Senekarabu anatuma watu wenye kuhubiri hofu kwa kueleza historia ya Hezekia ya udhaifu.
Senekerebu anatuma watu wake wageuze neno la Mfalme Hezekia ili apate kuifisha Imani yao apate kuwapiga. Hezekia anataka kuonyesha waziwazi tofauti kati ya mkono wa mfalme wa Ashuru na mkono wa BWANA.

Nasi kanisa lazima tutambue ya kuwa kwetu upo mkono wa BWANA wenye nguvu ya Kuokoa na Kuponya hivyo lazima tusimame kwa Imani ndipo tupate kufungua Malango na Milango iliyofungwa mbele zetu, Maana pasipo IMANI haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa imani yote yanawezekana katika Kristo.

Imani ni chanzo kikuu cha kupokea kutoka kwa Mungu maana hakuna neno lolote lililo gumu la kumshinda Mungu aliye hai.

Mwanamke huyu aliteseka pamoja na kuteswa na mengi lakini kwa IMANI alipata kupokea Uponyaji baada ya kusikia Neno la Yesu Kristo lenye nguvu ya Kuponya. Hivyo kwa imani Wagonjwa wataponywa na kupata afya tena.

Wakati mwanamke yule anashika pindo la vazi la Yesu Kristo, nguvu zilizomtoka Yesu Kristo, ndizo zilizokwenda kufanya uponyaji kwa mwanamke huyu kwa Imani, hivyo ni dhahiri pasipo Imani hakuna nguvu ya Mungu kuingia na kuponya. Unaweza kuguswa na Watu au Watumishi wa Mungu na usipone lakini ukiamini kabisa na usione shaka moyoni mwako hapo ndipo utakapo pokea.“Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kkwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”  Warumi 10:9-10

Imani yetu katika Yesu Kristo Yesu sharti ivuke mipaka iliyowekwa mbele yetu, maana kwa Imani BWANA anasema,
“Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza, nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma.” Isaya 45:2

WATU WANAWEZA KUKUCHEKA KWASABABU YA IMANI YAKO KATIKA MUNGU, usiogope vicheko vyao bali kaza roho kwa Imani maana lipo Jibu kwa kuwa Mungu hufungua njia mahali pasipo kuwa na njia. Angalia mfano huu wa ufunguo wa imani; “

 “Hata alipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa yule mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu? Lakini Yesu, aliposikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu. Wala hakumruhusu mtu afuatane naye, ila Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye Yakobo. Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu. Alipokwisha kuingia, akawaambia, mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu. Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, wakamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwambo yule kijana. Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi, tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka. Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu. Akawaonya sana, mtu asijue habari ile, akaamuru apewe chakula.” Marko 5:35-43

Katika msiba Yesu anaangalia imani ya yule mkuu wa Sinagogi ili apate kutenda muujiza. Kwa maana Imani ahitaji ushabiki wa watu bali Imani inahitaji mtu mwenye kujua Neno la Mungu na kuliamini. Watu walimcheka Yesu Kristo pale aliposema mtoto hajafa bali amelala, Yesu akamwamsha, akamwambia kijana amka naye akawa mzima. Vivyo hivyo inawezekana upo kwenye ndoa miaka mingi hujapata mtoto, Kwa Imani tumbo lako lifunguliwe milango yake na upate watoto wa kiume na wakike.

 “Kwa Imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba, alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.” Waebrania 11:11

SARA alipoambiwa atabeba mimba na kuzaa aliona ni kichekesho kwake maana alikuwa mzee. Hali halisi ya mwili wa Sara ilimfanya apoteze imani ya kuzaa. Wako watu wengi wa Mungu wanaopishana na Baraka zao toka kwa BWANA kwa sababu ya kuhesabu miaka ya mapito yao na kuona Mungu amechelewa na kinachozaliwa ni kukata tamaa kwa mfano wa Sara. “Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee? BWANA akamwambia Ibrahimu, mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee? Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.” Mwanzo 18:11-14

Katika mambo yote Mungu hufanya kazi na wenye Imani ili apate kuwapatia Mema kwani ndio wale walioitwa kwa kusudi lake, Sisi tu watoto wa Mungu basi sasa tu warithi wa Baraka na Ustawi wa Kimungu, turithio kwa Imani pamoja na Kristo Yesu. Imani ni kutarajia yasiyowezekana kutarajiwa.

SARA alimpokea Isaka katika hali ya kutokutarajiwa kwani alikuwa mkongwe wa miaka mingi. Tangu Mungu atamke Ahadi ya uzao wa Sara, miaka ishirini na tano ilipita. “Nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani, na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. Basi Abrahamu akenda kama BWANA alivyomwamuru, Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abrahamu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.” Mwanzo 12:3-4

IBRAHIMU alishakata tama juu ya ahadi ya Mungu ya kupata mtoto kupitia SARA, maana kimwili Sara alikuwa ni mzee asingeweza tena kuzaa. (biologically)
“Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara. Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme za kabila za watu watatoka kwake. Ndipo Ibrahimu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, je! Mtu wa umri wa miaka mia, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa? Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.”  Mwanzo 17:15-18

 Kwa imani kila mlango uliofungwa utafunguliwa, hatuhitaji kuangalia historia uliyopitia au hali ya mwili wako bali unachopaswa kuangalia ni Uweza na Nguvu za Mungu aliyehai ambaye yeye hashindwi na jambo lolote.

 “…lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.” Habakuki 2:4

“BWANA ametukumbuka, naye atatubariki sisi. Ataubariki mlango wa Israeli, Ataubariki mlango wa Haruni, Atawabariki wamchao BWANA, wadogo kwa wakubwa.” Zaburi 115:12-13

Ushindi wetu katika ulimwengu wa Roho na mwili hutegemea Ufunguo wa Imani.

Itaendelea……..



Friday, 21 November 2014

Mch. Florian . J. Katunzi.
Bwana asifiwe mtu wa Mungu, bado naendelea na mtiririko wa somo hili ambaloninaamini litafanyika msaada kwako na hata kwajirani yako. Pia napenda kukumbusha ya kuwa kitabu hiki kitatoka  siku chache zijazo hivyo jiandae kukipokea.

Katika utangulizi wa somo hili tuliangalia juu ya habari za Mfalme Nebukadreza aliyekuwa kiongozi wa dola yenye nguvu sana ya Ukaldayo na pia alikuwa muabudu miungu. Mara  baada ya kifo chake Mungu alimuinua Mfalme Koreshi ambaye alikuwa mpakwa mafut wa BWANA na alifanya akusudi yote ambayo Mungu aliyaweka.

 Leo tutakwenda kuangalia juu ya aina tano za funguo za kufungua                                               malango na   milango. 


 AINA TANO ZA FUNGUO ZA KUFUNGUA MALANGO NA MILANGO;


 UFUNGUO WA KWANZA 

 NENO LA MUNGU   


 Neno ni kauli ya Mungu yenye Mamlaka, Uweza na Nguvu za ki-Mungu zenye kuleta mageuzi ya kiroho na kimwili. Yesu Kristo alithibitisha yakuwa Neno la Mungu lina mamlaka na nguvu pale alipolitumia kufungua mafungo yaliyofunga watu wa Mungu sawasawa na injili ya Luka 4:36 Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, ni Neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.” 


Tunajifunza pia kwa Neno vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana viliumbwa maana Mungu aliziumba mbingu na nchi kwa Neno lake. Alisema iwe na ikawa. “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.” Yohana 1:1-5


 Tukitaka kufungua malango na milango iliyofungwambele yetu sharti kwanza tuwe na ufunguo wa Neno la Mungu. Maana Neno ni taa na nuru ya maisha yetu. Aliye na Neno haendi gizani kwa sababu kwa Neno la Mungu hakuna lisilowezekana.Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.” Luka 1:37


 Neno la Mungu kamwe halipiti hivyo tukilishika Neno kila lango na malango hakika yatafunguka. “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe” Mathayo 24:35Neno lake husimama katika kweli daima. Neno la Mungu huja kwetu likiwa hai, likifungulia imani yetu.Ndipo BWANA akaniambia… naliangalia neno langu, ili nilitimize” Yeremia 1:12
 

 UFUNGUO WA PILI

IMANI


Imani sikuzote imekuwa ndiyo alama ya wanafunzi wa Yesu. Wanafunzi wa kwanza walijulikana kama WAAMINI. Yesu alisema “… Yote yawezekana kwake aaminiye Mark 9:23


Imani humaanisha kumtegemea Mungu kwa hali zote. Wakati Adamu alipofanya dhambi, alijitoa katika kumtegemea Mungu na kujitegemea (ambako ni kutokuamini). Hii ndiyo sababu Mungu ameweka kipaumbele kwenye imani. Imani ni njia ya kuturudishia uhusiano na Mungu (kumtegemea Mungu). Basi Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Warumi 10:17  


Tunajifunza yakuwa pasipo Neno la Mungu hakuna imani ya ki-Mungu. Maana yake ufunguo wa kwanza ndiyo unaotupeleka kwenye ufunguo wa pili. Kumtegemea Mungu ndiko kunakoitwa imani. Kwa imani unatoka kwenye kutokuweza hadi kuweza. Kwa imani hakuna lisilowezekana.


 A: IMANI NI NINI?  


Imani ni tendo la utii katika kuitikia kile Mungu alichokisema katika Neno lake.Imani ya kweli inaelezewa katika Utii na Kutenda kulingana na  Neno la Mungu.Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana” Waebrania 11:1


Hivyo pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu; kwa maana kila mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, naye huwapa thawabu wale wamtafutao sawasawa na Neno lake. Ni lazima tumtafute Mungu kwa juhudi na kutamani kwa bidii uwepo wa neema yake.


Imani na utii haviwezi kutengana kama vile ambavyo kutokuamini na kutokutii kusivyoweza kutengana.Kwa imani Musa, alipozaliwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; hawakuigopa amri ya mfalme. Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima akakataa kuitwa mwana wa binti Farao; akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo; akihesabiwa ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo. Kwa  imani akatoka Misri asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.”  Waebrania 11:23-27 


B: KWELI TATU ZA IMANI    


 Msingi wa kuwa na imani kwa Mungu uko katika kweli tatu muhimu: Asili ya Mungu; 

 a.     Hawezi Kubadilika.
“Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu..” Malaki 3:6
 b.     Hawezi Kushindwa“Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na yakuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika” Ayubu 42:2
 c.      Hawezi Kudanganywa“Mungu si mtu, aseme uongo; wala si mwanadamu ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?” Hesabu 23:19
Kristo amefanyika chanzo cha imani yetu kwa Mungu. Ukweli kuhusu kifo chake na ufufuko hutoa msingi wa kuamini kwetu.Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi” 1Wakorintho 1:30


Ili imani itende kazi ya kufungua malango na milango katika maisha yetu, ni lazima kutii Neno la Mungu. Imani HUTENDA KAZI pale mtu aliyeamini anapofanya sehemu yake kwa imani, hiyo humfanya Mungu naye kutenda sawasawa na kuamini kwa mtu. 


Angalia mfano wa mwanamke aliyekuwa na msiba wa kutokwa damu muda wa miaka kumi na miwili, aliposikia Neno la uponyaji kupitia Kristo Yesu aliamini na kuadhimia moyoni mwake kumwendea Yesu Kristo kwa imani ili apate kufunguliwa. “Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi namiwili alikuja kwa nyuma, akagusa upindo wa vazi lake. Kwa maana alisema moyoni mwake, nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, jipe moyo mkuu, binti yangu, imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile. Mathayo 9:20-21


Matokeo ya imani sikuzote mwisho wake ni ushindi kwake yeye aaminiye na kumletea utukufu wa Mungu katika maisha yake ya kiroho na kimwili. “… kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu” 1Yohana 5:4


Malango na Milango ni sharti ifunguliwe kwa Imani; sawasawa na Neno la Mungu. Kwa Imani tunalegeza viuno vya wafalme, Kwa Imani tunalegeza mafungo na vifungo vilivyowafunga watu wa Mungu. Kwa Imani tunafungua Malango na Milango iliyofungwa mbele yetu.  “Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.” Isaya 10:27


 Kila mzigo uliotwishwa katika nafsi yako unaondolewa begani mwako maana uwezo wake Kristo Yesu sasa umedhihirishwa ili kazi zote za yule mwovu shetani zivunjwe ndani mwa imani. “Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo, nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji.” Zekaria 10:2


Imani ni Ufunguo wa kufungua Malango na  Milango, tunaona Senakeribu analeta majeshi yake akiwa ameazimia kupiga watu wa Mungu na kuwatawala. Mfalme Hezekia  akasema na watu wake ili apate wakuwajenga Kiimani.  “Iweni hodari, na wa moyo mkuu, msiogope, wala msifadhaike kwa sababu ya mfalme wa Ashuru, wala kwa majeshi yote walio pamoja naye; kwa maana yupo mkuu pamoja nasi kuliko aliye pamoja naye, kwake upo mkono wa mwili, ila kwetu yupo BWANA, Mungu wetu, kutusaidia, na kutupigania mapigano yetu. Na watu wakayategemea maneno ya Hezekia mfalme wa Ashuru.”   2 Mambo ya Nyakati 32:7-8


 Adui anakuja na neno lenye kuogofya ili kuifisha Imani yako, Senekarabu anatuma watu wenye kuhubiri hofu kwa kueleza historia ya Hezekia ya udhaifu.Senekerebu anatuma watu wake wageuze neno la Mfalme Hezekia ili apate kuifisha Imani yao apate kuwapiga. Hezekia anataka kuonyesha waziwazi tofauti kati ya mkono wa mfalme wa Ashuru na mkono wa BWANA. 


Nasi kanisa lazima tutambue ya kuwa kwetu upo mkono wa BWANA wenye nguvu ya Kuokoa na Kuponya hivyo lazima tusimame kwa Imani ndipo tupate kufungua Malango na Milango iliyofungwa mbele zetu, Maana pasipo IMANI haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa imani yote yanawezekana katika Kristo.


 Imani ni chanzo kikuu cha kupokea kutoka kwa Mungu maana hakuna neno lolote lililo gumu la kumshinda Mungu aliye hai. Mwanamke huyu aliteseka pamoja na kuteswa na mengi lakini kwa IMANI alipata kupokea Uponyaji baada ya kusikia Neno la Yesu Kristo lenye nguvu ya Kuponya. Hivyo kwa imani Wagonjwa wataponywa na kupata afya tena.


Wakati mwanamke yule anashika pindo la vazi la Yesu Kristo, nguvu zilizomtoka Yesu Kristo, ndizo zilizokwenda kufanya uponyaji kwa mwanamke huyu kwa Imani, hivyo ni dhahiri pasipo Imani hakuna nguvu ya Mungu kuingia na kuponya. Unaweza kuguswa na Watu au Watumishi wa Mungu na usipone lakini ukiamini kabisa na usione shaka moyoni mwako hapo ndipo utakapo pokea.Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kkwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”  Warumi 10:9-10


Imani yetu katika Yesu Kristo Yesu sharti ivuke mipaka iliyowekwa mbele yetu, maana kwa Imani BWANA anasema,Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza, nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma.” Isaya 45:2


 WATU WANAWEZA KUKUCHEKA KWASABABU YA IMANI YAKO KATIKA MUNGU, usiogope vicheko vyao bali kaza roho kwa Imani maana lipo Jibu kwa kuwa Mungu hufungua njia mahali pasipo kuwa na njia. Angalia mfano huu wa ufunguo wa imani; “  “Hata alipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa yule mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu? Lakini Yesu, aliposikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu. Wala hakumruhusu mtu afuatane naye, ila Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye Yakobo. Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu. Alipokwisha kuingia, akawaambia, mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu. Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, wakamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwambo yule kijana. Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi, tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka. Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu. Akawaonya sana, mtu asijue habari ile, akaamuru apewe chakula.” Marko 5:35-43


 Katika msiba Yesu anaangalia imani ya yule mkuu wa Sinagogi ili apate kutenda muujiza. Kwa maana Imani ahitaji ushabiki wa watu bali Imani inahitaji mtu mwenye kujua Neno la Mungu na kuliamini. Watu walimcheka Yesu Kristo pale aliposema mtoto hajafa bali amelala, Yesu akamwamsha, akamwambia kijana amka naye akawa mzima. Vivyo hivyo inawezekana upo kwenye ndoa miaka mingi hujapata mtoto, Kwa Imani tumbo lako lifunguliwe milango yake na upate watoto wa kiume na wakike.  “Kwa Imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba, alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.” Waebrania 11:11


SARA alipoambiwa atabeba mimba na kuzaa aliona ni kichekesho kwake maana alikuwa mzee. Hali halisi ya mwili wa Sara ilimfanya apoteze imani ya kuzaa. Wako watu wengi wa Mungu wanaopishana na Baraka zao toka kwa BWANA kwa sababu ya kuhesabu miaka ya mapito yao na kuona Mungu amechelewa na kinachozaliwa ni kukata tamaa kwa mfano wa Sara. Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee? BWANA akamwambia Ibrahimu, mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee? Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.” Mwanzo 18:11-14


Katika mambo yote Mungu hufanya kazi na wenye Imani ili apate kuwapatia Mema kwani ndio wale walioitwa kwa kusudi lake, Sisi tu watoto wa Mungu basi sasa tu warithi wa Baraka na Ustawi wa Kimungu, turithio kwa Imani pamoja na Kristo Yesu. Imani ni kutarajia yasiyowezekana kutarajiwa. SARA alimpokea Isaka katika hali ya kutokutarajiwa kwani alikuwa mkongwe wa miaka mingi. Tangu Mungu atamke Ahadi ya uzao wa Sara, miaka ishirini na tano ilipita. Nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani, na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. Basi Abrahamu akenda kama BWANA alivyomwamuru, Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abrahamu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.” Mwanzo 12:3-4 


IBRAHIMU alishakata tama juu ya ahadi ya Mungu ya kupata mtoto kupitia SARA, maana kimwili Sara alikuwa ni mzee asingeweza tena kuzaa. (biologically)Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara. Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme za kabila za watu watatoka kwake. Ndipo Ibrahimu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, je! Mtu wa umri wa miaka mia, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa? Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.”  Mwanzo 17:15-18


Kwa imani kila mlango uliofungwa utafunguliwa, hatuhitaji kuangalia historia uliyopitia au hali ya mwili wako bali unachopaswa kuangalia ni Uweza na Nguvu za Mungu aliye hai ambaye yeye hashindwi na jambo lolote.  “…lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.” Habakuki 2:4


BWANA ametukumbuka, naye atatubariki sisi. Ataubariki mlango wa Israeli, Ataubariki mlango wa Haruni, Atawabariki wamchao BWANA, wadogo kwa wakubwa.” Zaburi 115:12-13


 Ushindi wetu katika ulimwengu wa Roho na mwili hutegemea Ufunguo wa Imani.

Itaendelea……………………..

Friday, 14 November 2014


BWANA asifiwe mtu wa Mungu, ni matumaini u mzima wa afya na unaendelea vema na shughuli zako za kila siku.

Ni jambo la baraka mbele zangu na mbele za Mungu kwa kuwa umepata nafasi ya kuweza kupitia habari mbalimbali katika blog hii.


Hivyo basi napenda nikukumbushe jambo moja la msingi sana katika maisha hasa wakati huu ambao tunajiandaa na safari ya kwenda mbinguni.


Jambo hilo ni juu ya maombi ya Utakaso, ni wazi kuwa wengi wetu tunajisahau sana au kujiona ni WAKAMILIFU mbele za Mungu na kusahau ya kuwa yapo mambo madogo madogo ambayo huwa yanatufarakanisha na Mungu wetu.


Ebu chukua hatua na kutafakari ni sehemu zipi au maeneo mangapi ambayo huwa unamkosea Mungu na yawezekana ikiwa ni kwa mawazo, matendo,maneno hata kutazama.


Bado hujachelewa Mungu wetu ni wa neema na huruma, na fanya wiki hii ikawe ni wiki yako ya kutengeneza na Mungu katika kila nyanja na eneo la maisha yako maana  Mungu wetu anasema, “Tazama mkono wa Bwana haukupunguka hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”Isaya 59:1-2


Je! unajisikia faraja gani kukosana na Mungu akupaye pumzi ya uhai kila inapoitwa LEO na ahangalii ni kwa namna gani umemkosea??


Lakini kumbuka, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Warumi 6:23


Hivyo, “Msidanganyike Mungu hadhihakiwi kwa kuwa cho chote apandacho mtu ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake katika mwili wake atavuna uharibifu bali yeye apandaye kwa Roho katika Roho atavuna uzima wa milele.” Wagalatia 6:7-8


Sasa basi huu ni wakati muafaka wa kuamua kwa dhati kabisa kuachana na yale yote mabaya na kulitii NENO la Mungu maana hata yeye anasema,“Kwa maana atakaye kupenda maisha na kuona siku njema auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila. Na aache mabaya atende mema  atafute amani, aifuate sana. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.” 1Petro 3:10-12


Ni matumaini yangu  vifungu hivi vya maneno vitakupeka katika tafakari ya juu ya njia zako maana Mungu anasema wazi ya kuwa, “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.” Mithali 28:13.


Basi chukua hatua ya kuingia katika maombi ya utakaso sasa,  TUBU kwa kila dhambi unayoikumbuka na usiyoikumbuka, achilia moyo wako mbele za Mungu., mimina machozi yako madhabahuni pake na kwa kuwa Mungu wetu ni wa rehema hakika atakusamehe.


Endapo utahitaji msaada zaidi basi wasiliana nami kupitia mawaaliano ambayo yanapatikana katika blog hii.


MUNGU WA MBINGUNI NA AKUBARIKI.

Wednesday, 12 November 2014

Mch. Florian  J. Katunzi

Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu na mpenzi wa Blog hii. Ni matumaini yangu u mzima wa afya.

Napenda kuchukua nafasi hii kukaribisha  katika mfululizo wa somo hili jipya ambalo naamini ukilifuatilia kwa makini hautatoka kama ulivyo. 

Pia jiandae kukipokea kitabu hiki ambacho bado kipo jikoni na kitakuwepo mtaani si muda mrefu kutoka sasa.



Utangulizi

Zipo aina nyingi za maombi yanayotajwa kwenye Biblia takatifu, na yenye matokeo dhahiri yenye kudhihirisha uweza wa ki-Mungu wenye nguvu za kuangusha ngome zote za giza.  Katika kitabu hiki nitafundisha aina ya maombi ya kufungua  malango na milango.

KUOMBA maana yake ni Kumwita Mungu. “Katika shida yangu nalimwita BWANA, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.” Zaburi  18:6

Ndani mwa maombi haya  BWANA  atakufungulia milango, na hakuna malango yatakayofungwa mbele yako tena. Neno la Mungu linatuambia:

 “Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafame; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.”  (Isaya 45:1-3)

Kipindi hiki wana wa Israeli walikuwa uhamishoni Babeli, kumbuka walitekwa na kuchuliwa uteka mpaka nchi ya Babeli na Jemadari Nebukadreza, mnamo mwaka 605 KK, baada ya kuwashinda wamisri  katika vita ya Karkameshi. Wakati huo kulikuwa na makundi mawili yaliyopelekwa uhamishoni Babeli, kundi la pili lilikuwa ni lile lililochukuliwa mwaka 586 KK.

Huyu Nebukadneza, ni mtoto wa kiume wa Nabopolasa, aliyemridhi baba yake kuwa mtawala wa dola ya Wakaldayo mwaka 605 KK. Hii ni kwa mujibu wa kitabu cha  The Cambridge Acient history  III Uk. 212.  Nebukadireza alikuwa  jemadari kijana aliyekuwa ana misuli ya vita na tena shujaa na mwerevu wa mapigano, hivyo alikuwa na sifa zote za kurithi kiti cha baba yake.

Wachambuzi wa mambo ya kale wanamuelezea kuwa alikuwa ni askari na mwanasiasa aliye heshimiwa sana kutokana na uwezo wake wa kuongoza mapigano na kujenga hoja katika uwanja wa kisiasa.

Baada ya kutwaa madaraka, mfalme huyu mpya alihusika kujenga  vyema himaya na alama za Babeli katika maeneo mbali mbali ya dunia, tena alijiongezea sifa kwa kumuoa Malkia wa Media  Amyhiya, binti wa Cyaxareas, aliyekuwa na utawala wa Kaskazini.

Neno la Mungu katika kitabu cha Daniel 2:36-43, linatuonyesha kuwa baada ya Nebukadreza aliyekuwa kiongozi wa dola yenye nguvu sana ya Ukaldayo kiasi cha  ufalme wake unafananishwa na kichwa cha dhahabu kwa  thamani yake, hata hivyo, alipojiinua kiasi cha kutaka kuabudiwa, ufalme wake, ulikomeshwa na Dola ya Ukaldayo iliingia hatua ya mwisho pamoja na kuchaguliwa kwa Nabondus mnamo mwaka 556 KK.

Baada ya kufa kwa Nebukadreza kinafuata kipindi kifupi cha kupinduana na kuchinjana kwa watawala na mwisho kabisa utawala wa Dola ya Ukaldayo unafutika kabisa na unaibuka utawala wa Wamedio, Umedi na Uajemi (Medionapersia) chini ya Mfalme Koreshi Mwajemi na Dario wa wamedi, walioungana pamoja na kuangusha Dola ya Ukaldayo mwaka 538. Utawala wa wabanabe ulidumu kwa kipindi cha miakamia mbili (200), mpaka 331 KK.  Ndani ya kipindi hiki cha utawala wa Wamedi na Wajemi, tunamuona Koreshi, tuliyemsoma katika andiko letu la msingi akitimiza unabii uliotolewa kwa kinywa cha Nabii Isaya miaka mia moja hamsini (150) kabla ya kutimizwa kwake  katika mwaka 538.

Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya wakaldayo. Katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Daniel, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka ambayo Neno la BWANA lilimjia Yeremia Nabii, kutimiza ukiwa wa Yerusalem, yaani, miaka sabini. nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwake maombi na dua, pamoja na kufunga na kuvaa nguo za magunia na majivu.” (Daniel 9:1-3).

Mungu anamuita Koreshi Masihi (mpakwa mafuta), kabla ya kuzaliwa kwake, kwani alizaliwa kwa makusudi ya Mungu, japo hakuwa akimwabudu (Mungu) wala hakuwa mwana wa Israeli, lakini anatumiwa na Mungu kuyatimiza mapenzi yake, kwa kuwaweka huru  Wayahudi kutoka uhamishoni Babeli.

Koreshi na mshirika wake Dario walianzisha dola ya Wamedi na Wajemi iliyodumu kwa karne mbili yaani miaka mia mbili, kama Neno la Mungu linavyosema:

“Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi Mfalme wa Uajemi, ili kwamba Neno la Bwana alilosema kwa kinywa cha Nabii Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake Koreshi, Mfalme wa Waajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaandika pia akisema Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; BWANA, Mungu wa mbingu, amenipa falme zote duniani; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi, kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, BWANA, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akajenge nyumba ya Bwana, Mungu wa Israeli, (Yeye ndiye Mungu, aliyoko Yerusalemu).  Na mtu awaye ye yote aliyesalia mahali popote akaapo hali ya ugeni, na asaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali,  na wanyama, zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiayari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu.” Ezra 1:1-4

Kudhihirisha upekee wa Koreshi, anatoa vyombo vya meza ya BWANA ambavyo Nebukadreza alivitwaa na kuvitia kwenye himaya ya miungu yake. “Tena Koreshi, mfalme, alivitoa vyombo vya nyumba ya BWANA, alivyokuwa amevileta Nebukadreza toka Yerusalemu na kuvitia katika nyumba haya miungu yake” Ezra 1:7







Total Pageviews

Eagt City Centre Blog 2013. Powered by Blogger.

About Me

My photo
Jicho langu latoka machozi lisokome,wala haliachi;Hata BWANA atakapoangalia. Nakutazama toka mbinguni Maombolezo 3:49-50

Followers

Featured Posts

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget