WANAWAKE wa injili (WWI) wa kanisa la EAGT City Centre lililopo
chini ya Mtumishi wa Mungu Mchungaji Florian Katunzi na mama yetu mlezi Rachel
Katunzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jimbo la Temeke, katika kutimiza makusudi matano ya mwanawake
ndani ya kanisa,tumejipanga kumtegemeza Mchungaji wa kanisa hili FLORIAN
KATUNZI kwa kununua GARI aina ya
LANDCRUZER V8 pamoja na kuandaa chakula cha hisani ambacho kinalenga kutumika
kukusanya fedha ambazo zitatumika katika ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Mungu.
Tukio hili la kihistoria na lililojaa baraka
ndani yake linatarajiwa kufanyika siku
tarehe 7 Desemba Mwaka huu katika
viwanja vya maonesho sabasaba na mgeni rasmi atakuwa Mh. Tunu Pinda.
Wazo hili limetokana
na makubaliano ya wanawake wapatao 360 ambao ni wanachama wa kurugenzi ya ndani
ya kanisa letu
Unaweza jiuliza
wanawezaje kufanikisha hili!
Ukweli ni
kwamba wanawake hawa walishirikiana katika kutoa ahadi mbalimbali pamoja na
kadi za michango ambazo zililenga
ukusanyaji wa fedha ambazo ndizo zitakazotumika kununua gari hii, pia kuandaa
chakula hiki cha hisani.
Lakini wanawake
hawa hawakutaka kuchukua baraka hii peke yao bali walishirikisha kanisa kwa
ujumla na michango hii bado inaendelea kukusanywa na tutazidi kujulishana kadri
siku zinavyokwenda…
Najua unatamani
kujua makudi haya matano ya mwanamke ndani ya kanisa ambayo yanatoa msingi na
wazo madhubuti la kumtegemeza mtumishi wa Mungu.
KUSUDI LA
KWANZA.
- KULETEA
NYUMBA BARAKA.
* Kuombea Mungu
aibariki na wote waliomo waokoke na wale waliokoka waendelee kukua kiroho.
* Kuwa mfano
mzuri nyumbani.
* Kuwaleta wote
na jamaa zake kwa Yesu
* Kuhudhuria
ibada na mikutano yote ya WWI ili ajifunze.
* Kutekeleza
nyumbani yote aliyojifunza kwemye ibada na mikutano ya WWI
* Kusimamia
ibada za nyumbani.
KUSUDI LA PILI.
- KULILETEA KANISA BARAKA.
*Kuombea likue kiroho na mafanikio katika mahitaji yake.
* Kulitegemeza kwa sadaka zetu za pesa na uhusika katika shughuli
za kanisa na kueneza injili.
* Kulisaidia kununua viti,
mikeka,meza n.k. kuwa walimu wa shule za Jumapili na kushuhudia.
* Kuhudhuria kwa uaminifu tutakuwa tunaliletea Baraka kanisa letu.
KUSUDI LA TATU
- KUMLETEA MCHUNGAJI BARAKA.
* Kumwombea mchungaji na mke wake katika huduma
* Kuombea familia ya mchungaji kwa ajili ya
mahitaji.
* KUMTEGEMEZA
- KWA
CHAKULA AMBACHO HAKIJAPIKWA NA VITU MBALIMBALI WALAO MARA MOJA KWA MWEZI
-KWA MAVAZI YA
MCHUNGAJI NA FAMILIA YAKE WATOTO NA MKE
-KWA KUTOA FUNGU
LA KUMI KWA UAMINIFU KANISANI.
* KUMSAIDIA
- KWA KUMPA
NAULI ANAPIKWENDA KWENYE MIKUTANO YA WACHUNGAJI INAPOWEZEKANA NA MAHITAJI
MENGINE.
-KUMHESHIMU
- kumheshimu mchungaji kama mtumishi wa Mungu
anayesimamia kundi. Wathesalonike 5:12-13
KUSUDI LA NNE
*Kuuletea mji
Baraka
* kuwaombea
watu wa mji ili waokolewe
*Kuishi maisha
matakatifu ambayo kwayo watu wanaweza kuvutwa kwa Yesu Kristo bila hata neon au bila kuhubiriwa.
* Kwa
kuwashuhudia watu na kuwakaribisha kanisani.
KUSUDI LA TANO
*Kukiletea chuo
cha biblia Baraka
* Kwa kukiombea
kwa ajili ya mahitaji yake
*kuwaombea
walimu na wanafunzi
*Kukitegemeza
kwa chakula na vitu vingine kama vyombo n.k
*Kukisaidia au
kumsaidia mwanafunzi wa chuo cha Biblia kama ada na nauli yake.
Mpenzi wa blog hii, ni matumaini yangu ya kuwa
mara baada ya kusoma makusudi hayo utatambua wanawake hawa wapo makini na
wanafuata matakwa na makudi yao katika kanisa.
Lakini napenda
utambue ya kuwa chama hiki cha WWI ni chama huru ambacho kinakaribisha wanawake
wote waliompokea Yesu kuwa BWANA na
mwokozi wa maisha yao sanjari na kuabudu katika kanisa la mahala pamoja.
Naamini ya kuwa
umeelewa chanzo na dhima halisi la wazo hili
na tunaamini utaungana nasi katika kufanikisha hili kwa fedha na maombi
pia.
Mwisho napenda
uwajue viongozi wetu ambao pia kama utaguswa unaweza kutuma mchango wako
kupitia mitandao ya simu.
M/KITI-
CHRISTINA MGAYA
MAKAMU M/KITI-
GRACE MASEBO- 0717 332922
KATIBU- IMANI
MBAGA
MTUNZA HAZINA-
ESTER MPEPO
Je! Utapenda
kujua ni gharama kiasi gani zitatumika katika ununuzi wa gari sanjari na
ujenzi wa nyumba????????????
ENDELEA KUFUATA
NAMI KATIKA BLOGU YETU PENDWA.
MUNGU AWABARIKI.
.
0 comments:
Post a Comment