Friday 28 November 2014

WANAWAKE wa injili (WWI) wa kanisa la EAGT City Centre lililopo
chini ya Mtumishi wa Mungu Mchungaji Florian Katunzi na mama yetu mlezi Rachel Katunzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jimbo la Temeke, katika kutimiza makusudi matano ya mwanawake ndani ya       kanisa,tumejipanga kumtegemeza Mchungaji wa kanisa hili FLORIAN KATUNZI  kwa kununua GARI aina ya LANDCRUZER V8 pamoja na kuandaa chakula cha hisani ambacho kinalenga kutumika kukusanya fedha ambazo zitatumika katika ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Mungu.

Tukio hili la kihistoria na lililojaa baraka ndani yake linatarajiwa kufanyika siku  tarehe 7 Desemba Mwaka huu  katika viwanja vya maonesho sabasaba na mgeni rasmi atakuwa Mh. Tunu Pinda.

Wazo hili limetokana na makubaliano ya wanawake wapatao 360 ambao ni wanachama wa kurugenzi ya ndani ya kanisa letu

Unaweza jiuliza wanawezaje kufanikisha hili!

Ukweli ni kwamba wanawake hawa walishirikiana katika kutoa ahadi mbalimbali pamoja na kadi za michango  ambazo zililenga ukusanyaji wa fedha ambazo ndizo zitakazotumika kununua gari hii, pia kuandaa chakula hiki cha hisani.

Lakini wanawake hawa hawakutaka kuchukua baraka hii peke yao bali walishirikisha kanisa kwa ujumla na michango hii bado inaendelea kukusanywa na tutazidi kujulishana kadri siku zinavyokwenda…

Najua unatamani kujua makudi haya matano ya mwanamke ndani ya kanisa ambayo yanatoa msingi na wazo madhubuti la kumtegemeza mtumishi wa Mungu.

KUSUDI LA KWANZA.
 -  KULETEA NYUMBA BARAKA.

* Kuombea Mungu aibariki na wote waliomo waokoke na wale waliokoka waendelee kukua kiroho.
* Kuwa mfano mzuri nyumbani.
* Kuwaleta wote na jamaa zake kwa Yesu
* Kuhudhuria ibada na mikutano yote ya WWI ili ajifunze.
* Kutekeleza nyumbani yote aliyojifunza kwemye ibada na mikutano ya WWI
* Kusimamia ibada za nyumbani.

KUSUDI LA PILI.
  -   KULILETEA KANISA BARAKA.

*Kuombea likue kiroho na mafanikio katika mahitaji yake.
* Kulitegemeza kwa sadaka zetu za pesa na uhusika katika shughuli za kanisa na kueneza injili.
*  Kulisaidia kununua viti, mikeka,meza n.k. kuwa walimu wa shule za Jumapili na kushuhudia.
* Kuhudhuria kwa uaminifu tutakuwa tunaliletea Baraka kanisa letu.

KUSUDI LA TATU
 - KUMLETEA MCHUNGAJI BARAKA.

* Kumwombea mchungaji na mke wake katika huduma
* Kuombea familia ya mchungaji kwa ajili ya mahitaji.
* KUMTEGEMEZA
- KWA CHAKULA AMBACHO HAKIJAPIKWA NA VITU MBALIMBALI       WALAO MARA MOJA KWA MWEZI
-KWA MAVAZI YA MCHUNGAJI NA FAMILIA YAKE WATOTO NA MKE
-KWA KUTOA FUNGU LA KUMI KWA UAMINIFU KANISANI.
* KUMSAIDIA
- KWA KUMPA NAULI ANAPIKWENDA KWENYE MIKUTANO YA  WACHUNGAJI INAPOWEZEKANA NA MAHITAJI MENGINE.

-KUMHESHIMU
-  kumheshimu mchungaji kama mtumishi wa Mungu anayesimamia kundi. Wathesalonike 5:12-13

KUSUDI LA NNE

*Kuuletea mji Baraka
* kuwaombea watu wa mji ili waokolewe
*Kuishi maisha matakatifu ambayo kwayo watu wanaweza kuvutwa kwa Yesu Kristo  bila hata neon au bila kuhubiriwa.
* Kwa kuwashuhudia watu na kuwakaribisha kanisani.

KUSUDI LA TANO

*Kukiletea chuo cha biblia Baraka
* Kwa kukiombea kwa ajili ya mahitaji yake
*kuwaombea walimu na wanafunzi
*Kukitegemeza kwa chakula na vitu vingine kama vyombo n.k
*Kukisaidia au kumsaidia mwanafunzi wa chuo cha Biblia kama ada na nauli yake.

Mpenzi wa blog hii, ni matumaini yangu ya kuwa mara baada ya kusoma makusudi hayo utatambua wanawake hawa wapo makini na wanafuata matakwa na makudi yao katika kanisa.

Lakini napenda utambue ya kuwa chama hiki cha WWI ni chama huru ambacho kinakaribisha wanawake wote waliompokea Yesu kuwa BWANA  na mwokozi wa maisha yao sanjari na kuabudu katika kanisa la mahala pamoja.

Naamini ya kuwa umeelewa chanzo na dhima halisi la wazo hili  na tunaamini utaungana nasi katika kufanikisha hili kwa fedha na maombi pia.

Mwisho napenda uwajue viongozi wetu ambao pia kama utaguswa unaweza kutuma mchango wako kupitia mitandao ya simu.

M/KITI- CHRISTINA MGAYA
MAKAMU M/KITI- GRACE MASEBO- 0717 332922
KATIBU- IMANI MBAGA
MTUNZA HAZINA- ESTER MPEPO

Je! Utapenda kujua ni gharama kiasi gani zitatumika katika ununuzi wa gari sanjari na ujenzi wa nyumba????????????

ENDELEA KUFUATA NAMI KATIKA BLOGU YETU PENDWA.
MUNGU AWABARIKI.



.


0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Eagt City Centre Blog 2013. Powered by Blogger.

About Me

My photo
Jicho langu latoka machozi lisokome,wala haliachi;Hata BWANA atakapoangalia. Nakutazama toka mbinguni Maombolezo 3:49-50

Followers

Featured Posts

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget