Wednesday 10 June 2015

" Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio ; Bali sasa jicho langu linakuona ." Ayubu 42:5

Kama ambavyo mtumishi wa Mungu Ayubu alivyosema hivyo ndivyo wana EAGT CITY CENTRE TUNASEMA LEO!!!

Ama kwa hakika tumemuona Mungu akifanya na ataendelea kufanya maana tulikotoka ni mbali kuliko tunakokwenda...!!!

Kwa takribani miaka mitano sasa tumekuwa tukiabudu katika Viwanja vya Maonesho vya Mwl Julius Kambarage Nyerere ( Sabababa) huku tukiwa na shauku ya kutaka kumiliki eneo letu ambapo tutajenga nyumba ya kumuabudu Mungu wetu pasipo bughudha.

Hakika Mungu amejibu maombi yetu kwa kutupa eneo katika eneo la MTONI MTONGANII karibu kabisa na Daraja la  Reli ya Tazara .....

Eneo hili  jipya lina  uwezo wa kuchukua takriban waumini 2,500 , na kuna mpango  endelevu ambao utawezesha upanuzi wa eneo hili hata kuweza  kuchukua jumla ya waumini 7,200.  Na hapo ndipo EAGT City Centre itadumu

Kikosi cha Bendi ya Jeshi la Polisi Tanzania kikiongoza maandamano kuelekea katika kanisa jipya .. 


Umati mkubwa wa waumini wa kanisa la EAGT CITY CENTER ukiongozwa na Mchungaji Florian Katunzi.



MChungaji Katunzi akiongoza msafara kuelekea lilipo kanisa jipya eneo la MTONI MTONGANI  jirani na reli ya Tazara.




Mwandishi na mtangazaji wa Radio WAPO Angelina Lukindo akifanya kazi yake wakati wa masafara..








Viongozi wa kanisa wakiwa wametangulia mbele  ili kuhakikisha mambo yanakwenda kwa utaratibu.


Waumini wakiwa wamebeba viti ambavyo watatumia katika kanisa hili jipya.



Mbeba maono na Mchungaji wa kanisa hili akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kanisa hili.

Viongozi mbalimbali waliokuwepo katika zoezi hilo

Umati wa waumini wakiwa ndani ya kanisa.

Unaweza pia kuwa sehemu ya baraka hizi kwa kutoa mchango wako utakaofanikisha kufikia lengo la ujazo wa watu 7,200 ndani ya miaka mitatu, kwa kuwasiliana na kutuma mchango wako moja kwa moja na Mchungaji Florian Josephat Katunzi kupitia namba 0754367826 ,  0784367826  au  0718267171.

Thursday 28 May 2015

SILAHA NANE ZA KUFUNGUA MILANGO NA MALANGO YALIYOFUNGWA MBELE YAKO;

SILAHA YA NANE

UWE MVUMILIVU;

“Uvumilivu” (Greek makrothumia) means patience without reaction (by implication without reaction, long suffering) ikiwa na maana ya ustahimivu; si mwepesi wa hasira wala kukata tamaa. Maandiko matakatifu yanatuelekeza tumwendee BWANA kwa wito wetu. Tukiwa tumejivika uvumulivu. “Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumulivu, mkichukuliana katika upendo.” Waefeso 4:2

Maisha ya mwanadamu yana mapito mengi sharti avumilie katika BWANA. Pasipo Uvumilivu, hauwezi kupokea jibu toka kwa BWANA kwa kuwa yeye hachelewi wala hawai isipokuwa anajibu kwa wakati wake. Hivyo maisha ya Imani yanahitaji Uvumilivu. “Kwa hiyo ndugu, vumilieni hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza naya mwisho. Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake BWANA kunakaribia. Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango. Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la BWANA, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa BWANA ya kwamba BWANA ni mwingi wa rehema, mwenye huruma. Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape wala kwa mbingu wala kwa nchi, wala kwa kiapo kinginecho chote, bali ndiyo yenu iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.” Yakobo  5:7-12

Mmesikia habari ya uvumulivu wa Ayubu, inasemekana zaidi ya miaka kumi na saba Ayubu alikuwa kwenye hali ya dhiki nzito yenye msiba na magonjwa lakini katika mambo yote hakumkufulu Mungu wala kuwaza kwa upumbavu. Maandiko yanathibitisha; “Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.” Ayubu 1:22
Kutokana na uvumilivu basi hivyo BWANA akaubarikia mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake. Akawa na mali mengi kondoo kumi na nne elfu, ngamia elfu sita na jozi ya ng’ombe elfu na punda wake elfu pia BWANA alimbariki Ayubu kwa kumwinulia uzao tena akawa wana waume saba na binti watatu. Wana wa Mungu yatupasa tusizimie roho bali tumtumaini BWANA kwa uvumilivu, “Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki bali njia ya wasio haki itapotea.” Zaburi 1:6

Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. Akaomba tena mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake. Maombi ni lazima yaambatane na Uvumilivu. Bwana anaposema atatenda ni lazima atende kwa wakati. “Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu.” Waebrania 10:23

Hivyo Mungu wetu hana kigeugeu, yeye akisema itakuwa lazima iwe tu. Ibrahimu alivumilia miaka ishirini na mitano kabla ya kumpata Isaka kwa Sara mkewe. “Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema. Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu. Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia. Ibrahimu akamtahiri Isaka mwanawe alipokuwa mwenye siku nane, kama Mungu alivyomwamuru. Naye Ibrahimu alikuwa mtu wa miaka mia, alipozaliwa mwana wake Isaka. Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami. akasema, n’nani  angemwambia Ibrahimu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.” Mwanzo  21:1-7

BWANA alimpa ahadi lakini ilipita miaka ishirini na mitano ya uvumilivu wa Kiimani. BWANA akageuza huzuni ya Sara kuwa kicheko, akazaliwa Isaka. Nawe Vumilia katika BWANA, Isaka wako atazaliwa pale lango lako  litakapo funguliwa.  “BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwahiyo nafsi imtafutayo.” Maombolezo  3:25

Umkabidhi BWANA njia zako pia umtumaini yeye naye atafanya. Ukae kimya mbele za BWANA nawe umngojee kwa saburi naye atakutendea pale usipozimia roho.

ISAKA naye alivumilia katika BWANA miaka ishirini akiomba kwa ajili ya mke wake Rebeka alikuwa tasa, mwisho wakazaliwa watoto mapacha. Isaka alioa Rebeka akiwa na umri wa miaka arobaini na mke wake alizaa Isaka alipokuwa ametimiza miaka sitini. “Na hivi ndivyo vizazi vya Isaka, mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka. Isaka akawa mwenye miaka arobaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake. Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba, watoto wakashindana tumboni  mwake. Naye akasema, ikiwa ni hivi, kuishi kwa nifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA. BWANA akamwambia, Mataifa mawili yako tumboni mwako, na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la
pili, na mkubwa atamtumikia mdogo. Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake. Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau. Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake unamshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa.” Mwanzo 25:19-26

Yusufu alivumilia mbele za BWANA muda wa miaka kumi na mitatu kabla ya ndoto zake zikatimizwa. “Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake, naye alikuwa kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari mbaya.” Mwanzo  37:2

Yusufu aliyekuwa na miaka kumi na saba alikuwa akichunga kondoo, akaota ndoto akawajulisha ndugu zake, wakazidi kumchukia wakasema tumuue tuone ndoto zake zitakuwaje. Lengo la ndugu zake Yusufu ilikuwa ni kuua maono na ndoto zisitimie, maadamu mbeba hayo maono alikuwa ni Yusufu ilibidi wapange kumuua na hayo maono. Maandiko yanathibitisha yakisema; “Wakamwona toka mbali na kabla hajawakaribia wakafanya shauri juu yake ili wamwue. Wakasemezana wao kwa wao, tazama, Yule bwana ndoto anakuja. Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema mnyama mkali amemla; KISHA TUTONA ZITAKUWAJE NDOTO ZAKE.” Mwanzo 37:18-19

Atukuzwe Mungu asiyeshindwa na jambo lolote, anayetuwazia mema, anayetamka mwisho wetu kabla ya mwanzo. Maana yake kwa imani lazima uuone mwisho wako kabla ya mwanzo ndipo utaweza kuvumilia. Maana; “Mungu si mtu aseme uongo; wala si mwanadamu, ajute; iwapo amesema hatalitenda? Iwapo amenena hatafikiliza?” Hesabu 23:19
Sifa ya Mungu ni thabiti katika kauli zake. Mungu si yule ambaye haaminiki, mwenye kigeugeu au mwenye kubadilika lakini kwa asili yake ni mwaminifu katika ahadi zake na kauli zake. Pamoja na kuuzwa ili ndoto za Yusufu zisitimie, Mungu alimfungulia Milango na Malango baada ya kukaa ndani ya gereza miaka miwili mizima ikiwa inahitimisha miaka kumi na tatu ya kusubilia jibu na wakati wa Mungu kuyatimiza aliyosema kwake. Tunajifunza uvumilivu wa Yusufu na mapito yake maana kila alikopita BWANA alikuwa pamoja naye, ndio maana hata kwa mke wa Potifa alionyesha kumjali Mungu na kumtumainia kuliko ahadi za muda kitambo tu. Akasema; “Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu chochote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe NIFANYEJE UBAYA HUU MKUBWA NIMKOSE MUNGU?” Mwanzo 39:9
Uaminifu wa Yusufu kwa Mungu ulimfanya ashinde jaribu la kuanguka katika tanzi ya uzinzi na uasherati. Tunajifunza kwa Yusufu alivyokimbia dhambi hii nasi yatupasa kuiga mfano huu kwa kukimbia dhambi ya uzinzi. Dhambi hii imewaangusha wengi na wamepoteza mwelekeo wa kiimani na uwepo wa Mungu. Vijana kwa wazee wanaanguka katika dhambi hii. Na wengi wao wameponzwa na ushawishi wa wenye dhambi kama mke wa Potifa,  badala ya kukimbia kama Yusufu wameingia katika majadiliano mwisho wake wameanguka. “Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, wewe usikubali. Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.” Mithali 1:10, 15
Baada ya uvumilivu na ushindi wa Yusufu, BWANA alimwinua, tunaona katika maandiko matakatifu jinsi Mungu alivyomkamata Farao kukawa ndio mwanzo wa kuinuliwa Yusufu na wana wa Israeli. “Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake. Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri. Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri. Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, kuwa mkewe Yusufu akaenda huko na huko katika nchi yote ya Misri. Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akapita katika nchi nyote ya Misri.” Mwanzo 41:41-46

Pia tunajifunza kwa Musa  alipokataa kuitwa mtoto wa binti Farao, alikuwa na umri wa miaka AROBAINI. Lakini alivumilia miaka arobaini akichunga mifugo ya Yethro na akavumilia safari ya miaka arobaini jangwani na wana wa Israeli kuelekea Kanani. Maandiko matakatifu yanathibitisha; “Umri wake ulipopata kama miaka arobaini akaazimu moyoni mwake kwenda kuwatazama ndugu zake Waisraeli. Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamtetea, akamlipia kisasi yule aliyekuwa akionewa, akampiga huyo Mmisri. Alidhani kwamba ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokovu kwa mkono wake, lakini hawakufahamu. Siku ya pili yake akawatokea walipokuwa wakishindana, akataka kuwapatanisha, akasema, Enyi bwana zangu, ninyi ni ndugu. Mbona mnadhulumiana? Lakini yeye aliyemdhulumu mwenziwe akamsukumia mbali, akisema, ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri jana? Musa akakimbia kwa neno hilo, akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Midiani, akazaa wana wawili huko. Hata miaka arobaini ilipotimia, malaika wa Bwana akamtokea katika jangwa la mlima wa Sinai katika mwali wa moto, kijitini. Musa alipouona akastaajabia maono yale, na alipokaribia ili atazame, sauti ya Bwana ikamjia, Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akatetemka asithubutu kutazama. Bwana akamwambia, vua viatu miguuni mwako, kwa maana mahali hapa unaposimama ni nchi takatifu. Yakini nimeona mateso ya watu wangu waliomo Misri, nimesikia kuugua kwao, nami nimeshuka niwatoe. Basi sasa, nitakutuma mpaka Misri. Musa huyo waliyemkataa, wakisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu na mwamuzi? Ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mkuu na mkombozi, kwa mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kijiti. Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arobaini. Musa huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi, msikieni yeye. Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi. Mtu huyo baba zetu hawakutaka kumtii, bali wakamsukumia mbali, na kwa mioyo yao wakarejea Misri, wakamwambia Haruni, Tufanyie miungu, watakaotutangulia; maana huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui lililompata. Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi za mikono yao. Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka, Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli? Nanyi mlichukua hema ya Moleki, na nyota za mungu wenu Refani, Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu; nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli.” Matendo 1:23-43


Pasipo Uvumilivu tutapishana na kalenda ya Mungu, lakini tukivumilia katika BWANA tutavuna mema. “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kishinda, kwa yeye aliyetupenda.” Warumi  8:37

Tutashinda yote tusipovunjika moyo; bali tujinyenyekeze kwa Mungu atatukweza kwa wakati wake. “Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.” Zaburi 55:22

DAUDI alivumilia miaka kumi na tatu. Na wakati ulipofika alipokuwa na umri wa miaka thelathini akawa mfalme wa Israeli. Amenusulika kuuawa na Sauli mfalme mara ishirini na tano; lakini Daudi daima aliomba akisema; “Ee Mungu, uniokoe, Ee BWANA, unisaidie hima. Warudishwe nyuma , watahayarishwe, wapendezwao na shari yangu. Warudi nyuma na iwe aibu yao, wanaosema Ewe! Ewe! Washangilie, wakufurahie, wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako waseme daima, Atukuzwe Mungu. Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee BWANA, usikawie.” Zaburi  70:1-5

Maombi haya yanafungua Malango na Milango ndani mwa Uvumilivu  wa Kiimani. Mtu mwenye Imani sharti avumilie akidumu katika maombi, maana yuko Jehova aliye hai atasimama. Maandiko matakatifu yanasema; “Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.” Ayubu 19:25

Mtetezi wetu hatimaye atasimama juu ya nchi atafuta kila chozi.
“Heri wakaao nyumbani mwako, Wanakuhimidi daima. Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake. Wakipita kati ya bonde la Vilio, hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulivika Baraka.” Zaburi  84:4-6

Yesu atawalipa watu wake wala hatawaacha bali katika taabu atawatoa. Mateso ya mwenye haki ni mengi sana lakini BWANA humponya nayo yote.









SILAHA NANE ZA KUFUNGUA MILANGO NA MALANGO YALIYOFUNGWA MBELE YAKO;

SILAHA YA SABA

UTOAJI WA DHABIHU
Kutoa Dhabihu au Sadaka sio kununua kitu kwa Mungu bali ni ishara ya unyenyekevu mbele za Mungu na ni tendo kamili la Kiibada. Kristo Yesu amefanyika Dhabihu ya dhambi ili sisi tupate ukombozi. Mungu amemtoa Sadaka ili kupitia yeye tufunguliwe mlango na milango ya mbinguni.

Utoaji  wa dhabihu au sadaka ni wa muhimu sana kwake yeye aaminiye maana tangu mwanzo dhabihu zilitolewa. Tunaona hata Adamu na Hawa walipotenda dhambi, BWANA Mungu aliwafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi akawavika. Lakini baada ya Mungu kumwinulia Adamu uzao walizaliwa Kaini na Habili. kutokana na kazi zao walipewa nafasi sawa ya kumtumikia Mungu kwa kazi za mikono yao. Kaini alikuwa mkulima na Habili alikuwa mfugaji. Tunajifunnza kwa watu hawa wawili walikwenda kumtolea Bwana Mungu dhabihu (sadaka ya hiari) mbele za BWANA. Maandiko yanathibitisha; “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabari Habili na sadaka yake; bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akagadhibika sana, uso wake ukakunjamana. BWANA akamwambia Kaini, kwanini unaghadhabu? Na kwanini uso wako umekunjamana?. KAMA UKITENDA VEMA, HUTAPATA KIBALI? Usipotenda vema dhambi iko inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.” Mwanzo 4:3-6
Mungu alimuumba mwanadamu kwa ajili yake. Ili amwabudu yeye, awe furaha yake iko nafasi moja tu katika moyo wa mwanadamu ya ibada. Na hii ni kwa ajili ya Mungu pekee. Mungu ni mwenye wivu asiyetaka kamwe kuchanganywa na miungu mingine. Ndiyo maana Mungu aliweka amri katika amri kumi “Mimi ni Bwana Mungu wako niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa usiwe na miungu mingine ila mimi.” Kutoka 20:1-2

Suala la kumwabudu Mungu linaambatana na kumtolea Mungu sadaka. Sadaka za wana wa Adamu, Kaini na Habili inaonyesha kielelezo cha kumkaribia Mungu kwa ibada. Tendo la kukubaliwa sadaka ya Habili ni kielelezo cha kukubaliwa mtoa sadaka. Hii ndiyo sababu iliyomfanya Kaini akamgadhibikia ndugu yake kwa sababu Mungu alizikataa sadaka za Kaini kwa sababu moyo wake haukuwa mkamilifu. Maana BWANA anasema, “Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA bali maombi ya mtu mnyoofu ni furaha. Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA. Bali humpenda mtu afuatie wema.” Mithali 15:8-9

Ndiyo maana hoja ya Mungu kwa Kaini inasema; KAMA UKITENDA VEMA, HUTAPATA KIBALI? (If you do what is right, will you not be accepted?) Ili mtu wa Mungu dhabihu yake ikubalike mbele za Mungu sharti awe na moyo mnyoofu. Habili anatajwa na maandiko matakatifu ya kuwa ni shujaa wa imani aliyetoa sadaka iliyo bora ambayo inanena mbele za Mungu. “Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo ijapo amekufa angali akinena.” Waebrania 11:4
Mungu aliikubali dhabihu ya Habili kwa sababu alikuwa mwenye haki na mtiifu. Nuhu alipokwisha kuokolewa na Mungu yeye na jamaa yake toka kwenye gharika tunaona anamjengea BWANA madhabahu na kutoa dhabihu. “Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, sitalaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.” Mwanzo 8:20-21

Baada ya kuokolewa lazima tumkaribie Mungu kwa maombi na sadaka. Tunajifunza katika utumishi wa Nuhu wa utoaji sadaka uliosababisha BWANA atoe tamko la kutokuangamiza tena baada ya kusikia harufu nzuri ya sadaka nzuri zilizotolewa na Nuhu. Kwa sadaka waweza kuikoa familia yako na maangamizi ufanyavyo hivyo ndani mwa maombi. Mungu hakutoa tamko la kutokuangamiza tena kabla ya sadaka bali ni baada ya sadaka kutolewa. Hivyo Mungu akambarikia Nuhu na wanae. Na akafanya agano nao la kutofuta kizazi chao tena kwa gharika. “Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya ghalika; wala hakutakuwa tena ghalika, baada ya hayo kuiharibu nchi.” Mwanzo 9:11

Tunajifunza pia kwa Ibrahimu baba yetu wa imani alimwabudu Mungu katika roho na kweli na kutoa dhabihu juu ya madhababu. “BWANA akamtokea Abram, akasema, uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhababu BWANA aliyemtokea. Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhababhu huko, kaliitia jina la BWANA.” Mwanzo 12:7-8

Ibrahimu aliitwa rafiki wa Mungu kwa sababu alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora, hata alipokuwa amepewa mtoto Isaka, alipotakiwa kumtoa mwanawe mpendwa wa pekee aliyempata katika uzee hakumzuilia Mungu. Tunasoma hivyo katika maandiko matakatifu “… Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko katika mlima mmoja wapo nitakao kwambia… wakafika mahali pale walipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhababu huko akaziweka tayari kuni kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe… kwa maana sasa najua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee… kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwano, mwanao wapekee, katika kukubariki nitakubariki, na katika kukuzidisha nitakuzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao na katika uzao wako mataifa yote duniani watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.” Mwanzo 22:1-18

Kwa tendo hili Ibrahimu alihesabiwa kuwa mwenye haki pale alipomtoa mwanawe juu ya madhabahu. Imani ya Ibrahimu ilijidhihirisha katika utii wa kweli kwa Mungu. Yeyote atakaye kutembea na Mungu kwa karibu yampasa kuwa tayari kumtoa “Isaka” wake madhabahuni. Ibrahim aliitwa rafiki wa Mungu kwa sababu ya kukubali kutoa Isaka wake. Wakristo wengi wanatoa ili mradi wanatoa, hawatoi kilicho bora bali wanatoa bora sadaka. Lakini tujifunze kwa watu hawa wawili Habili na Ibrahimu tunaona utoaji wao ni utoaji ulio bora, walitoa sadaka zinazowagusa wao wenyewe, maana Isaka anatolewa mzima-mzima madhabahuni pa BWANA. Hivyo hakuna kuabudu kuliko kamili kusiko ambatana na utoaji. Kila mtu katika biblia aliyetoa sadaka bora ilidhihirisha ubora wa maisha ya mcha Mungu. Maandiko yanathibitisha katika kitabu cha 1Nyakati “Mpeni BWANA utukufu wa jina lake, leteni sadaka mje mbele zake; mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.” 1Nyakati 16:29
Kipindi hiki cha nabii Eliya mtishibi alipotaka kukomesha imani potofu za miungu katika Taifa la Israeli, zilizoanzishwa na mfalme Ahabu mwana wa Omri na mke wake Yezebeli binti Ethbaali mfalme Wasidoni. Mfalme huyu na mke wake walimjengea Baali madhabahu huko Samaria na wakamsujudia. Katika biblia mfalme Ahabu anahesabika kuwa mfalme mwovu sana miongoni mwa wafalme wa Israeli. BWANA alipokuwa amemwinua Eliya mtishibi kipindi hiki Ahabu alikuwa amewaua manabii wengi mno wa Mungu aliye hai. Ilibidi afanye maombi ya kufunga malango na milango juu ya Israeli, akaifunga mvua isinyeshe katika nchi miaka mitatu na nusu (3½) maandiko yanasema; “Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja nasisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu yanchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. Akaomba tena mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda.” Yakobo 5:17-18
Maombi ya mwenye haki sharti yaambatane na kutoa dhabihu mbele za Mungu aliye hai, tunajifunza kwa Eliya nabii.“Kisha Eliya akamwambia watu wote, Nikaribieni mimi. Watu wote wakamkaribia. Akaitengeneza madhahabu ya BWANA iliyovunjika. Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya kabila za wana wa Yakobo, aliyejiliwa na neno la BWANA na kuambiwa, jina lako litakuwa Israeli. Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la BWANA; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu. Kisha akazipanga zile kuni, akamkata-kata yule ng’ombe vipande vipande, akaviweka juu ya kuni. Akasema, Jazeni mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya kuni. Akasema fanyeni mara ya pili, wakafanya mara ya pili. Akasema fanyeni mara ya tatu, wakafanya mara ya tatu. Yale maji yakaizunguka madhabahu, akaujaza mfereji maji. Ikawa wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. Unisikie, Ee BWANA unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, BWANA, ndiwe Mungu, na ya kuwa wew umewageuza moyo wakurudie. Ndipo moto wa BWANA ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, yaliyokuwamo katika mfereji. Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, BWANA ndiye Mungu. Eliya akawaambia, Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja, wakawakamata, na Eliya akawachukua mpaka kijito cha Kishoni, akawaua huko.” 1Wafalme  18:30-46

Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya kabila za wana wa Yakobo, akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la BWANA; tunajifunza tendo la imani kwa mtumishi wa Mungu nabii Eliya jinsi alivyobeba watu wake kwa kabila zao na kuwainua mbele za BWANA kwa njia ya maombi, kisha akazipanga zile kuni, akamkata-kata yule ng’ombe vipande vipande, akaviweka juu ya kuni. Tunajifunza kuwa maombi na dhabihu vinakwenda pamoja madhabahuni pa BWANA. Ikawa wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, Ndipo moto wa BWANA ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, yaliyokuwamo katika mfereji. Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, BWANA ndiye Mungu.

Moto wa BWANA unawakilisha uwepo wa Mungu na nguvu zake. Maombi haya ya kufungua Malango na Milango sharti yaambatane na Kutoa Dhabihu mbele za Mungu aliye hai. Eliya Mtishibi ili akomeshe taabu, dhiki na mateso kwa Israeli vilivyotekwa na mfalme Ahabu na mkewe Yezebeli kwa kuungamanisha taifa kwa miungu ya Wasidoni mungu aitwaye Baari na Ashtoleth; Eliya alisimama mahali palipo bomoka, akajenga Madhabahu ya BWANA tena iliyokuwa imevunjika. Kwa mawe kumi na mawili sawasawa na kabila kumi na mbili za Israeli.

Hata Mungu mwenyewe, ili amwokoe mwanadamu na dhambi, alimtoa mwanawe wa pekee Yesu kristo, ili awe kuhani mkuu atakaye wapatanisha kwa njia ya kifo cha msalaba. Ili kwa damu yake Kristo Yesu wanadamu wapate ukombozi maana pasipo damu hakuna ondoleo la dhambi. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana  3:16

Vitu vyote tulivyo navyo vyatoka kwake na viko kwa uweza wake, hivyo tunapotoa Dhabihu zetu mbele zake yeye Mungu aliye hai ni tendo la Kiimani la Kujiungamanisha naye kwa neno na kwa tendo.
“Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.” Warumi  11:35-36

Maombi yetu ya kufungua malango sharti yatubebe Sisi, Watoto wetu na Mali zetu. “Na tumwinulie Mungu aliye mbinguni, Mioyo yetu na mikono.” Maombolezo  3:41

Maana yake; Wewe binafsi ufunguliwe Malango na Milango, Watoto wako wafunguliwe Malango na Milango, Mali zako, Kazi yako, Biashara yako, Elimu yako na Vyote Uvitendavyo vistawishwe katika BWANA visizae Kufa-kufa wala Mapooza. “Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote, Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.” Mithali  3:9-10


Bwana yeye ndiye atupaye Baraka na Ustawi si vinginevyo, Lazima tujinyenyekeze kwa Maombi yeu na Sadaka zetu zilizo bora. “Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, UTAJIRI na HESHIMA katika mkono wake wa kushoto. NJIA zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani. Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana, Ana heri kila mtu ashikamanaye naye.” Mithali  3:16-18

Baraka za Mungu zipo kwao waliotayari kuzifuata na kushikamana nazo. Unapo mwomba Mungu na kutoa Dhabihu zako Madhabahuni pake, Yeye hushuka kwa nguvu zake na atakupa Baraka zifuatazo:-

(i) WINGI WA SIKU; maana yake Maisha marefu.
      BWANA anasema; “Utafika kaburini  mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.” Ayubu  5:26

(ii) UTAJIRI na HESHIMA;
     Vinaambatana na USTAWI katika kazi yako yote ya mikono. “Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, Tena nipate kuzijaza hazina zao.” Mithali  8:20-21

Jambo la msingi lazima kila mmoja wetu anayeitwa kwa jina la BWANA, sharti ajenge Madhabahu ya BWANA kwa ajili yake na familia yake. Maana yake ni Kumrejesha Mungu wa kweli katika familia. Panahitajika mtu atakaye batilisha hiyo miungu ya ukoo, miungu ya kichifu, isitende kazi kwa kuivua madhabahuni kwa njia ya maombi na dhabihu ili maandiko yatimie ya Mtunga Zaburi. “Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu. Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.” Zaburi  20:7-8
Baada ya kuokoka na kuvishwa uwezo wa ki-Mungu kwa njia ya imani yatupasa kuchukua hatua za kiimani ndani mwa maombi ili KUBATILISHA na KUTENGUA ibada za miungu na matoleo yake (makafara), yaliyotolewa kabla. Ibada za miungu hufanyika kwa njia ya maombi na dhabihu japo hazitolewi kwa mungu wa kweli lakini mfumo unaweza kufanana na wa ibada za kweli, ndiyo maana manabii wa Baali walijenga madhabahu na kutoa sadaka. Tunaona katika maandiko; “Eliya akawaambia manabii wa Baali, jichagulieni ng’ombe mmoja, mkamtengeneza kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu wal msitie moto chini… wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri wakisema Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliye jibu. Nao wakrukaruka juu ya madhabahu aliyoifanya… ikawa wakati wa adhuhuri ulipopita, walitabiri hata wakati wa kutoa dhabihu ya jioni; lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu, wala aliyeangalia.” 1Wafalme 18:25-29 

Tunajifunza kwa mtumishi wa Mungu Ayubu jinsi alivyoomba na kutoa dhabihu kwa Mungu aliye hai; Ayubu alikuwa anawaombea daima watoto wake na kuwatolea dhabihu mbele za BWANA, kila mmoja alimtolea Maombi na Sadaka. Hata Shetani alipowatamani watoto wa Ayubu na akatamani kumfilisi Ayubu, alishindwa mpaka alipomwendea Mungu kuomba apewe ruhusa.

Maisha ya Ayubu na familia yake yalijulikana daima mbele za BWANA. Tunasoma katika maandiko matakatifu yanasema; “Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi namapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu siku zote. Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao. BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Kisha BWANA akamwuliza Shetani, je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure? Wewe hukumzingira kwa ukingo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake umeiongezeka katika nchi.” Ayubu 1:5-10

Ayubu hakuwaacha watoto wake nyuma katika Ibada, bali aliwabeba daima na kuwaombea. Mungu alimzingira pande zote yeye na familia yake pamoja na mali zake zote, BWANA aliwawekea UKINGO, shetani akashindwa kuwanasa.

Tunapata siri ya ki-Mungu ya kwamba tumwombapo Mungu na kutoa dhabihu zinazokubalika mbele zake, Yeye hutuwekea ukingo pande zote. Ukingo maana yake ni ukuta, boma, ngome, jabali, mwamba. Na BWANA anasema; “Kwa maana mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.” Zekaria 2:5

Lazima uchukue hatua ya Kiimani kumwendea Mungu Madhabahuni pake. Omba, Ombea, Watiishe watoto wako kwenye Maombi na Sadaka popote walipo na adui hatawanasa kamwe. “Wewe hukumzingira kwa ukingo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake umeiongeza katika nchi.” Ayubu  1:10

Inua Biashara yako mbele za BWANA, Inua kazi yako mbele za BWANA, Inua Elimu yako mbele za BWANA kwa maombi na sadaka. “Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.” 1 Mambo ya nyakati  16:29

Leteni Sadaka, mje mbele zake, Inua mikono mje mbele zake kwa Maombi ili BWANA aweke Ukingo kwako, Mabaya yasikupate na Ulinzi wake ukufunike.

Tunaona mtumishi wa Mungu mfalme Daudi alipokuwa na msiba uliotokana na pigo la ugonjwa wa tauni toka kwa BWANA. Maelfu ya watu yamekwishakufa katika nchi yake, wakati Daudi hajui cha kufanya ili kuondoa mauti juu ya nchi ndipo anaambiwa na Mungu ajenge Madhabahu na atoe Dhabihu. “Siku hiyo Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Haya! Kwea wewe, ukamwinulie BWANA madhabahu penye kiwanja cha Arauna, Myebusi. Basi Daudi akakwea sawasawa na neno la Gadi, kama BWANA alivyoamuru. Huyo Arauna akatazama, akamwona mfalme na watumishi wake wakimjia, Arauna akatoka, akasujudu mbele ya mfalme kifulifuli hata nchi. Arauna akasema, Bwana wangu mfalme amemjia mtumwa wake kwa kusudi gani? Naye Daudi akasema, Makusudi ninunue kwako kiwanja hiki, ili nimjengee BWANA madhabahu, ili kwamba tauni ipate kuzuiliwa katika watu. Arauna akamwambia Daudi, Bwana wangu mfalme na akitwae, akatolee yaliyo mema machoni pake, tazama ng’ombe hawa kwa sadaka ya kuteketezwa, tena vyombo vya kupuria, na vyombo vya ng’ombe, viko kwa kuni. Vitu hivi vyote, Ee mfalme, mimi Arauna nakupa wewe mfalme. Kisha Arauna akamwambia mfalme, BWANA Mungu wako, na akukubali. Lakini mfalme akamwambia Arauna, La, sivyo lakini kweli nitavinunua kwako kwa thamani yake, wala sitamtolea BWANA, Mungu wangu, sadaka za kuteketezwa nisizo zigharamia. Hivyo Daudi akakinunua hicho kiwanja cha kupuria na wale ng’ombe kwa shekel hamsini za fedha. Naye Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Basi BWANA aliidhiria nchi, na tauni ikazuiliwa katika Israeli.” 2 Samweli  24:18-25

Tunajifunza kwa mtumishi wa Mungu Daudi jinsi alivyotoa Sadaka yenye gharama na bora aliyo gharamikia yeye mwenyewe. Matokeo yake tunayaona baada ya Daudi kutoa dhabihu kifo kilizuiliwa kwa watu wake. Tukio hili ni la kiimani na la kuigwa kwa watu wa Mungu. Tunayaona Maombi ya kufungua Malango na Milango ni sharti tumwendee Mungu madhabahuni, Tumjengee madhabahu na Tutoe Sadaka; naye atashuka Kuzuia Magonjwa, Mateso, Misiba na kila aina ya Vifungo. Hivyo Usiogope; Jenga Madhabau yako, Toa Sadaka, hayo yaliyokupata yataondolewa na kuzuiliwa yasije kwako tena. Dhabihu yako, Igeuze Msiba wako kuwa Uzima, na kwa wale unao waombea na kuwainua mbele za Mungu aliye hai.

“Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.” Zaburi  50:23

Lazima nasi tunapofunguliwa Malango na Milango; fahamu wako wengi watupingao watatufuata-fuata  kwa ubaya, Nawe usimamapo katika maombi nyosha mkono wako juu yao, kinyume, warudishie mabaya yao, yawalambe, wavishwe fedheha yao. “Bwana akamwambia Musa, nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao. Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na BWANA akawakukutia mbali hao Wasmisri kati ya bahari. Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.” Kutoka 14:26-28

Usiudharau Mkono wako, Musa aliponyoosha mkono wake juu ya bahari, BWANA alifungua njia na mlango kwa wana wa Israel wakapita, Bahari ikawa nchi kavu. Nasi tukinyosha mikono yetu kwa Jina la Yesu Kristo yatafanyika na Malango yatafunguka. “Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake.” Mithali  5:22



SILAHA NANE ZA KUFUNGUA MILANGO NA MALANGO YALIYOFUNGWA MBELE YAKO;

SILAHA YA SITA

GEUZA UTEKA WAKO
Maombi yetu ni ya kufungua Malango na Milango, sasa tunaingia hatua ya sita ya Kuvaa Silaha; Silaha ni lazima Ugeuze kwa Maombi; uteka, taabu zako, Dhiki zako kuwa Baraka. Hali uliyopitia au unayopitia haiwezi kugeuzwa kama  wewe hutaigeuza kwa Imani. Hakuna neno gumu la kumshinda kristo Yesu. Angalia mfano wa Ayubu; “Basi ikawa, baada ya BWANA kumwambia Ayubu maneno hayo, BWANA akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili, kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu kwani ninyi hamkunena maneno yaliyonyoka katka habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. Basi Elifazi, Mtemani na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda wakafanya kama vile BWANA alivyowaamuru, naye BWANA akamridhia Ayubu. Kasha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza. Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake, nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote BWANA aliouleta juu yake; kila mtu akam,pa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja. Basi hivyo BWANA akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu, na punda wake elfu. Tena alikuwa na wana waume saba, na binti watatu. Akamwita huyo wa kwanza jina lake Yemima, na wa pili akamwita jina lake Kesia, na wa tatu akamwita jina lake Keren-hapuhu. Katika nchi hiyo yote hawakuwapo wanawake waliokuwa wazuri kama hao wana wa Ayubu; na baba yao akawapa urithi kati ya ndugu zao wana waume. Kasha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia na arobaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hata vizazi vinne. Basi Ayubu akafa, mzee sana mwenye kujawana siku.” Ayubu 42:7-17

Pia tunajifunza kwa Yabesi katika Biblia jinsi alivyofanya maombi ya kufungua milango na malango. Alipaza sauti yake kwa Mungu wa Israeli ni kielelezo cha wenye haki, ni kweli kwamba Mungu huwabariki wale ambao humuita kwa uaminifu. Yatupasa tuzingatie kwamba heshima na baraka zitatujia na kutupata pale tutakapomwomba Mungu ndani mwa maombi ya kufungua milango na malango. Yabesi anaonyesha waziwazi kwamba Baraka za Mungu na Ulinzi wake havishuki kwetu hivihivi bali hutokea baada ya sisi kujitoa kwake na kwa mpango wake hapa duniani na baadaya maombi yetu. Maombi ya Yabesi yaligeuza historia ya maisha yake tena ya kuzaliwa nayo badala ya kuwa na maisha ya huzuni alikuwa na maisha ya furaha. Maandiko yanathibitisha kielelezo cha maisha ya Yabesi kama ifuatavyo; “Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamamye akamwita jina lake Yabesi, akisema, ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kwelikweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo alioyaomba” 1Nyak 4:9-11

YABESI kwa lugha ya kiebrania inasikia kama uchungu.
Tukimwomba Mungu kwa moyo wa dhati pasipo shaka yeye ni mwaminifu kwa wote wamtafutao na kwake hakuna jambo lililo gumu la kumshinda.“Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili, je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?”  Yeremia  32:27

Malango na Milango, Inafunguliwa kwa sisi Kuomba kwa kugeuza kimaombi kilicho kufa kipate kuwa hai. Ndani mwa maombi haya BWANA anasema waziwazi; “Watakuja kwa kulia na kwa maombi nitawaongoza, nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyooka, katika njia hiyo hawatajikwaa maana mimi ni baba wa Israeli…” Yeremia 31:9

Maombi yanageuza hali, Maombi yanafungua Malango yaliyofungwa. Bwana anasema Maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha; nami nitawafanya waache huzuni zao. Nasi tukiomba kwa Imani, Kristo Yesu atageuza uteka wetu kuwa Baraka. BWANA aligeuza taabu ya Ayubu kuwa Baraka pia aligeuza msiba wa Ayubu kuwa baba wa watoto wengi. Kwa kuwa Ayubu hakuteteleka katika imani bali aliomba na kukiri akisema, “Lakini mimi najua ya kuwa mteteaji wangu yu hai, na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, lakini pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; nami nitamwona mimi nafsi yangu, na macho yangu yatamtazama wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu!” Ayubu 19:25-27  


Wako maadui zako wanakutaja kwa ubaya; wanasema mabaya juu yako, juu ya ndoa yako, wanasema mabaya juu ya kizazi chako;
Lakini Mungu atageuza tutakapodumu katika maombi ile laana na hayo matamko yao yatakuwa Baraka. “Kwa sababu hawakuwalaki wana wa Israeli kwa chakula na maji, bali walimwajiri Balaamu juu yao ili awalaani; lakini Mungu aliigeuza ile laana kuwa Baraka.” Nehemia 13:2

Malango yalipofungwa mbele ya wana wa Israeli, mtumishi wa Mungu Nehemia aliitisha maombi ya kufungua Malango na milango muda wa miezi minne mfululizo. “Hata ikawa niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadha wa kadha; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni.” Nehemia 1:4

Hapa tunajifunza jinsi watakatifu wa zamani walivyomwishia Mungu kwa imani. Kwa njia ya maombi na kujinyenyekeza kwa kufunga, hatuoni mahali popote kimaandiko wakijihangaisha kutafuta mbinu mbadala za kuwafungulia malango na milango katika maisha yao. Bali tunaona silaha ya maombi ndiyo iliyotumika, tofauti na wakristo wa leo walio wengi wameacha maombi, wameacha kufunga na kutafuta uso wa Mungu aliye hai, wamegeukia imani nyingine za kutegemea vitu viitwavyo vya upako kama vile mafuta ya upako, maji ya upako, chumvi ya upako, udongo wa upako, picha za hao wajiitao manabii na mitume, vitambaa vya upako, sabuni za upako na vingine vingi vifananavyo na hivyo. Vitu hivi haviwezi kamwe kuleta suluhisho la kiroho katika maisha ya mkristo maana ni vitu vilivyobuniwa kwa akili za wanadamu sio kwa akili za Mungu. Mkristo jifunze na ujiepushe na hizi imani potofu zinazoenea kwa kasi zikionyesha zitafungua malango na milango ya watu wa Mungu kumbe sivyo. Msingi wetu wa wokovu upo katika maneno haya; “Basi, kwakuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili  za wanadamu.” Mdo 17: 29
Pia Mungu ni Roho na wale wanaomwabudu Yeye sharti kumwabudu katika roho na kweli sio kwa mitazamo ya watu wanaopinga maombi na kuwauzia watu vitu vya kiibada za kishetani ili viwalinde. “Basi wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu msijemkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu. Lakini kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na mwokozi Yesu Kristo, utukufu unayeye sasa na hata milele.” 2Petro 3:17-18
Maana wengi walipotea kwa kufuata uhalifu wa mioyo, maana kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwetu watakavyo kuwepo waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza. Na wengi watafuata ufisadi wao, na wao watajipatia faida ya mali kwa tamaa zao wenyewe wakitumia maneno yaliyotungwa ili kuwanasa yamkini wateule. BWANA anasema, “Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliowekewa.” 2Petro 2:17 
Wapenzi msiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetoka kwa Mungu kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea. Wenye kudanganya wanamfano wa utaua lakini wanazikana nguvu za Mungu. Mkristo usidanganyike hakuna Mungu wa kweli anayepatikana ndani ya chupa bali ndani mwa Maombi. Kristo Yesu alisema waziwazi; “Ombeni, nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.” Mathayo 7:7
Ndugu zangu tangu zamani mafuta yalikuwepo lakini hayakutumiwa kiholelaholela kama yanavyotumika sasa, ingekuwa ni hivyo, Yesu Kristo asingewaagiza wanafunzi wake wasiondoke Yerusalemu mpaka wajazwe nguvu za Roho mtakatifu. “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” Mdo 1:8  Kama mafuta yanaleta upaku au uwepo wa Mungu angeweza kuwapaka mafuta akawaacha waende kutumika, lakini Kristo hakufanya hivyo bali aliwaambia wakae mpaka siku ya Pentekoste (siku ya hamsini baada ya kufufuka kwa Yesu) wakae kwenye maombi. “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto ulio wakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajaalia kutamka.” Mdo 2:1-4

Hivyo tukimwamini Mungu na nguvu zake, yeye anazo nguvu na uweza mkuu wa kugeuza uteka wetu kuwa Baraka. Kila hali unayoipitia iliyo ngumu hata kama ina historia tata kwa Mungu yote yawezekana kwake yeye aaminiye. Simama katika zamu yako geuza uteka. Maandiko yanasema; “Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, ukanivika furaha.” Zaburi  30:11

Nyumba yako ifunike ndani mwa maombi ili isiwe ni nyumba ya misiba, huzuni, umaskini, magonjwa, dhiki na vilio vya uchungu. Bali zigeuza hali zote zisikaribie mlango wako. Usiogope, bali wewe fanya Maombi upate kugeuza, Maana Mkono wake Kristo ni Mkono wenye Nguvu na Uwezo mkuu wa kufungua malango na milango iliyofungwa. Tunajifunza kwa Mfalme Yehoshafati aliwashinda wana wa Moabu na wana wa Amoni kwa Maombi ya kugeuza ubaya wao uwapate wao wenyewe. “Ikawa baadaye, wana wa Moabu, na wana wa Amoni, na pamoja nao baadhi ya Wameuni, wakaja juu ya Yehoshafati vitani. Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng’ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio En-gedi) Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute BWANA; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote.” 2Nyakati 20:1-3

Wana wa Israeli walipokuwa ndani mwa maombi ya kugeuza uteka; BWANA alilibatilisha shauri la maadui zao. Hata sisi tukiomba kwa uaminifu na kwa juhudi, hakika maadui zetu wa kiroho na kimwili wataanguka mbele yetu. Maana Mungu ni yeye yule jana, leo na hata milele.
“Nao walipoanza kuimba na kusifu, BWANA akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa. Kwani wana wa Amoni na wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu mwenziwe. Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia wa jangwani, wakalitazama hilo jeshi; nao angalia, walikuwa maiti walioanguka nchi, wala hapana aliyeokoka.” 2Nyakati  20:22-24
Katika hili tunajifunza nguvu iliyomo ndani mwa maombi maana tunauona mkono wa BWANA ambavyo unawaangusha maadui wa Israeli walipokuwa kwenye maombi. Tuonapo vita katika ulimwengu wa roho au mwili, hatua ya kwanza ni kumtafuta Mungu aliye hai kwa njia ya maombi. Ndipo maadui zako wataanguka kwa ajili yako. Watu wa Moabu, Amoni na Seiri walipatana kinyume juu ya Israeli lakini BWANA aligeuza shauri lao, panga zao na mikuki yao, ikawachoma wenyewe ili yathibitike maneno ya Mungu yaliyonenwa na kinywa cha nabii Isaya; “Utathibitika katika haki, utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa, na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia. Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako. Tazama nimemuumba mhunzi avukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemuumba mharibu ili aharibu. Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.” Isaya  54:14-17

Usiogope kwa sababu ya hayo bali yageuze yawageukie wao wenyewe, maana wamechimba shimo lazima watumbukie wao. Geuza kwa Maombi yako na kwa Dhabihu zako. Maana BWANA amekukumbuka tena na atakubarikia tena. BWANA anasema; “Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe, usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako. Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, usiogope; mimi nitakusaidia.” Isaya  41:10-13
Hakika tukiomba na tukaa ndani mwa maombi; Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.





SILAHA NANE ZA KUFUNGUA MILANGO NA MALANGO YALIYOFUNGWA MBELE YAKO;

SILAHA YA TANO

REJESHA KILA KILICHOKUWA KIMECHUKULIWA;

Katika hatua hii ya tano, ni hatua ya urejesho maana baada ya kuokolewa Kristo Yesu amekusudia kuturejeshea Baraka na Ustawi. Maandiko matakatifu yanathibitisha kwa kinywa cha nabii Isaya;  “BWANA akapendezwa, kwaajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha. Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa, wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza, wamekuwa mawindo wala hapana aokoaye, wamekuwa mateka wala hapana asemaye rudisha. Ni nani miongoni mwenu atakaye tega sikio lake kuyasikia hayo? Atakayesikiliza na kusikia kwa wakati ujao? Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang’anyi? Si yeye, BWANA? Yeye tuliyemkosa, ambaye hakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake.” Isaya 42:21-25

BWANA anasema wazi wazi yakuwa wako watu walioibiwa Baraka zao na ustawi, wengine wameibiwa ufaulu na uelewa wao katika masomo,wengine wameibiwa uchumi na utajiri wao, wengine wameibiwa ndoa zao na mengine mengi yanayofanana na haya. Lazima tusimame ndani mwa maombi  na kurejesha kila kilichoibiwa na adui shetani. Maombi ugeuza hali pale watu wa Mungu wanapoomba kwa nia moja na moyo mmoja, hakika Mungu atafungua. Tunajifunza kwa wana wa Israeli kipindi cha nabii Samweli jinsi walivyoinuka, wakamlilia BWANA naye akawaitikia. Nakuwafadhaisha maadui zao. Maandiko yanathibitisha katika kitabu cha Samweli; “Samweli akasema, Wakusanyeni Israel wote Mispa, name nitawaombea ninyi kwa BWANA. Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji na kuyamimina mbele za BWANA; wakafunga siku ile, wakasema huko, tumemfanyia BWANA dhambi. Samweli akawaamua wana wa Israeli huko Mispa. Hata Wafilisti waliposikia ya kuwa wana wa Israeli wamekusanyika huko Mispa, mashehe wa Wafilisti walipanda juu ili kupigana na Israeli. Nao wana wa Israeli waliposikia, wakawaogopa Wafilisti. Wana wa Israeli wakamwambia Samweli, Usiache kumlilia BWANA, Mungu wetu kwa ajili yetu, kwamba atuokoe na mikono ya Wafilisti. Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo mchanga, akamtolea BWANA sadaka ya kuteketezwa nzima, Samweli akamlilia BWANA kwa ajili ya Israeli, BWANA akamwitikia. Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; walakini BWANA akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, juu ya Wafilisti siku ile, akawafadhaisha, nao wakaangamizwa mbele ya Israeli. Nao watu wa Israeli wakatoka Mispa, wakawafuatia Wafilisti, wakawapiga hat walipofika chini  ya Beth-kari. Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya mispa na Sheni, akaliita jina lake Eben-ezeri, akasema, Hata sasa BWANA ametusaidia.hivyo Wafilisti walishindwa, wasiingie tena ndani ya mipaka ya Israeli; na mkono wa BWNA ulikuwa juu ya Wafilisti siku zote za Samweli. Nayo miji ile Wafilisti waliyokuwa wamewapokonya Waisraeli ilirudishwa tena kwa Israeli, tokea Ekroni mpaka Gathi, na Waisraeliwakaukoa mpaka wake mikononi mwa Wafilisti. Tena kulikuwa na amani kati ya Israeli na Waamori. Naye huyo Samweli akawaamua Israeli siku zote za maisha yake.” 1 Samweli  7:5-14

Israeli chini ya Nabii Samweli, BWANA aliwashindia vita katika kusanyiko la Maombi ya kufunga. Maana wakati Samweli anatoa sadaka na dhabihu ya jioni madhabahuni pa BWANA; ikapigwa ngurumo na mshindo mkuu toka kwa BWANA ambao uliwafadhaisha Wafilisti ndipo Israeli wakashinda vita, baada ya kushinda ndipo wakarejesha yote yaliyokuwa yametekwa na Wafilisti. Nasi ndani mwa Maombi haya lazima turejeshe kila kilichochukuliwa na adui. Kama ni afya yako sharti uombe kwa Imani ukirejesha. Maana BWANA anasema, nitakurudishia afya, nitakuponya jeraha zako… Hata kama umeumwa sana lazima Uombe urejeshewe afya yako. “Naye atakurejezea uhai wako, na kukuangalia katika uzee wako, kwa maana mkweo ambaye akupenda, naye anakufaa kuliko watoto saba, ndiye aliyemzaa.” Ruthu  4:15

BWANA kabla ya kuwaokoa wana Israeli toka utumwani Misri, alipiga miungu ya Farao kwa mapigo kumi lakini kabla ya pigo ya mwisho, alimwambia Musa awaambie wana wa Israeli watake mali, toka kwa Wamisri naye BWANA atashusha nguvu ya kuwafanya Wamisri warejeshe mali mengi na utajiri kwa wana wa Israeli. “Basi nena wewe masikioni mwa watu hawa, na kila mtu mume na atake kwa jirani yake, na kila mwanamke atake kwa jirani yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu.” Kutoka  11:2

Malango ya Uchumi yatafunguliwa pale tu Mwombaji sharti kwanza atake mbele za Mungu kwa Imani. Lipo sikio linalosikia Maombi, Lazima Mali zilizofichwa na adui gizani, tuzitoe na turejeshe katika milki yetu.“Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.” Isaya  45:2-3

BWANA anasema atakufungulia Malango na Milango mbele yako, naye atakupa hazina, utajiri usio pimika, wewe na uzao wako maana wote walio kuonea watafadhaishwa naam wametahayarika mbele yako. Chukua hatua ya kuamini, Mali zako, Utajiri wako uje mikononi mwako maana Mungu aliyeziumba Mbingu na Nchi, yeye ndiye Mungu wako ataufanya Imara Uchumi wako, Hakutakuwa tena ndani mwako kufa-kufa na kuzaa mapooza.“kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.” Isaya  45:23

Ayubu anasema nimeomba BWANA, amesikia, nimemlilia yeye kwa sababu hiyo Mungu atamfanya mjane na yatima wabarikiwe na wataimba nyimbo za furaha badala ya maombolezo. Usiogope, Lango lako limefunguliwa, Rejesha Ustawi wako. Usikae kimya, Omba urejesho kwa nguvu. Mtumishi wa Mungu Ayubu, anaomba Mungu baada ya kufilisika, hana kitu, lakini anaomba tena Ustawi wa Mali zake.“Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia; Na jicho liliponiona, likanishuhudia. Kwa sababu nalimuokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia. Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia, nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.” Ayubu  29:11-13
Lazima Mali zetu zitapikwe na wachawi walio tumeza lazima tuwakanyage matumbo yao kwa nguvu, tuwatapishe UTAJIRI wetu na HESHIMA. Baada ya Maombi haya, tutang’aa kama dhahabu mbele ya maadui zetu; maana BWANA anaugeuza uteka wako kuwa Baraka na Ustawi; ustawishwe na Uinuliwe na Urejeshewe Heshima. “Utukufu wangu utakuwa mpya, Na uta wangu hurejezwa upya mkononi mwangu.” Ayubu  29:20

Yeye aliyemeza mali ataitapika, maana BWANA ataitoa tumboni mwake. “Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake.” Ayubu 20:15

HESHIMA AU CHEO

Esta  3:13-15
“Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja yaani siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa Adari, na kuyachukuamali yao kuwa nyara. Nakili ya andiko, ya kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa yote wawe tayari siku ile ile. Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai, bali mji wa Shushani ukafadhaika.”

Esta na Modekai wanachukua hatua ya Kufunga na Kuomba. wakachukua hatua ya kuifuata Heshima yao kwa mfalme Ausuwelo. Esta akaingia kwa mfalme, ndipo Heshima ya Wayahudi ikarejeshwa, Aibu zao, Huzuni zao zikatenguliwa. “Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, name na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kasha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia na niangamie.” Esta 4:16

Ombea Uzao wako

“Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu moyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu siku zote.” Ayubu  1:5

Esta; alisimama na kweli, Mungu akatenda



Total Pageviews

Eagt City Centre Blog 2013. Powered by Blogger.

About Me

My photo
Jicho langu latoka machozi lisokome,wala haliachi;Hata BWANA atakapoangalia. Nakutazama toka mbinguni Maombolezo 3:49-50

Followers

Featured Posts

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget