Friday 14 November 2014


BWANA asifiwe mtu wa Mungu, ni matumaini u mzima wa afya na unaendelea vema na shughuli zako za kila siku.

Ni jambo la baraka mbele zangu na mbele za Mungu kwa kuwa umepata nafasi ya kuweza kupitia habari mbalimbali katika blog hii.


Hivyo basi napenda nikukumbushe jambo moja la msingi sana katika maisha hasa wakati huu ambao tunajiandaa na safari ya kwenda mbinguni.


Jambo hilo ni juu ya maombi ya Utakaso, ni wazi kuwa wengi wetu tunajisahau sana au kujiona ni WAKAMILIFU mbele za Mungu na kusahau ya kuwa yapo mambo madogo madogo ambayo huwa yanatufarakanisha na Mungu wetu.


Ebu chukua hatua na kutafakari ni sehemu zipi au maeneo mangapi ambayo huwa unamkosea Mungu na yawezekana ikiwa ni kwa mawazo, matendo,maneno hata kutazama.


Bado hujachelewa Mungu wetu ni wa neema na huruma, na fanya wiki hii ikawe ni wiki yako ya kutengeneza na Mungu katika kila nyanja na eneo la maisha yako maana  Mungu wetu anasema, “Tazama mkono wa Bwana haukupunguka hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”Isaya 59:1-2


Je! unajisikia faraja gani kukosana na Mungu akupaye pumzi ya uhai kila inapoitwa LEO na ahangalii ni kwa namna gani umemkosea??


Lakini kumbuka, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Warumi 6:23


Hivyo, “Msidanganyike Mungu hadhihakiwi kwa kuwa cho chote apandacho mtu ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake katika mwili wake atavuna uharibifu bali yeye apandaye kwa Roho katika Roho atavuna uzima wa milele.” Wagalatia 6:7-8


Sasa basi huu ni wakati muafaka wa kuamua kwa dhati kabisa kuachana na yale yote mabaya na kulitii NENO la Mungu maana hata yeye anasema,“Kwa maana atakaye kupenda maisha na kuona siku njema auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila. Na aache mabaya atende mema  atafute amani, aifuate sana. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.” 1Petro 3:10-12


Ni matumaini yangu  vifungu hivi vya maneno vitakupeka katika tafakari ya juu ya njia zako maana Mungu anasema wazi ya kuwa, “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.” Mithali 28:13.


Basi chukua hatua ya kuingia katika maombi ya utakaso sasa,  TUBU kwa kila dhambi unayoikumbuka na usiyoikumbuka, achilia moyo wako mbele za Mungu., mimina machozi yako madhabahuni pake na kwa kuwa Mungu wetu ni wa rehema hakika atakusamehe.


Endapo utahitaji msaada zaidi basi wasiliana nami kupitia mawaaliano ambayo yanapatikana katika blog hii.


MUNGU WA MBINGUNI NA AKUBARIKI.

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Eagt City Centre Blog 2013. Powered by Blogger.

About Me

My photo
Jicho langu latoka machozi lisokome,wala haliachi;Hata BWANA atakapoangalia. Nakutazama toka mbinguni Maombolezo 3:49-50

Followers

Featured Posts

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget