Friday 12 December 2014

Kwa Takribani miezi SITA sasa WANAWAKE WA KANISA LA EAGT CITY CENTRE walikuwa wakiendelea na changizo kwaajili ya ununuzi wa gari aina ya LANDCRUZER V8 ikiwa ni katika kutimiza makusudi la tatu kati ya matano ya wanawake wainjilisti ( WWI)  ndani ya kanisa.

Zoezi hili lilifanikiwa kwa asilimi 100 ambapo wanawake hawa walifanikiwa kununua GARI hili ambalo lilikabidhiwa kwa Mchungaji wa kanisa hili Florian Katunzi  na aliyekuwa mgeni rasmi wa sherehe hiyo ambaye ni   Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda.


Picha za gari kabla ya kukabidhiwa.















Hakika haikuwa kazi nyepesi kulifanikisha hili kwa nguvu ya maombi kutoka wanawake hawa na kanisa kwa ujumla jambo hili lilifanikiwa.

Viongozi wa WWI ambao ndio walianzisha wazo hili na kulitekeleza kwa kusimamia, kuhamasisha changizo mpaka kukamilika kwa jambo hili
Makamu mwenyekiti  Grace Masebo akijadiliana jambo na Katibu Imani Mbaga.  

Mhazini wa chama Ester Mpepo wa tatu kushoto akiwa na baadhi ya viongozi na wanakamati wa sherehe.

Safu ya viongozi wa WWI jimbo wakiwana mwenyeji wao Mama Katunzi wa kwanza kulia,  nao walihudhuria ili kuwasindikiza wanawake wenzao katika kufanikisha hili.


Picha zinazoonesha wanawake hawa wakimkaribisha kwa shangwe mgeni rasmi Mama Tunu Pinda.

Mwenyekiti WWI  city center Christina Mgaya  akimlaki mgeni rasmi.

Mhazini wa WWI  Estha Mpepo akisalimiana na mgeni rasmi.

Mchungaji Flrian Katunzi akiongozana na viongozi katika kumlaki mgeni rasmi.


Mchungaji Florian Katunzi na mkewe wakiwa wameambatana na mgeni rasmi

Wanawake na mabinti waliovalia sare maridadi wakimpokea mgemi rasmi.


Mwenyekiti Christina Mgaya akisoma risala mara baada ya kumkaribisha mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akiwa na Mama Mchungaji Katunzi wakisikiliza risala kwa makini.


Mchungaji Katunzi akiwa na meza kuu huku akiwa ameambatana na  Mzee Kiongozi Bw. Mbaga wa kwanza kushoto.
Mwenyekiti akimkabidhi mgeni rasmi risala
Mwenyekiti akipena mkono na Mchungaji Katunzi  maara baada ya kukabidhi risala.
Mwimbaji wa nyimbo za injili Bahati Bukuku akiimba mara baada ya mwenyekiti kumaliza kusoma risala.
Mgeni rasmi akielekea mahali lilipo gari tayari kwa kumkabidhi Mchungaji Katunzi.
Mgeni rasmi akikata utepe

Mgeni rasmi akiwa ameshikwa funguo za gari
Mgeni rasmi tayari kufungua gari
Mchungaji Katunzi na mkewe wakitoa ahadi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yao .

Mchungaji Katunzi akielekezwa jambo la mgeni rasmi
Mchungaji Katunzi ndani ya LANDCRUZER V8 mara baada ya kukabidhiwa..
Mgeni rasmi akielekezwa jambo na Mc kabla ya kuanza kuzungumza.
Mgeni rasmi akihotubia pambani yake ni mama Katunzi. Mara baada ya hotuba hiyo moja kwa moja alienda kwenye zoezi la changizo kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya mchungaji ambayo inatarajia kugharimu kiasi cha Mil.250.
Mzee Kiongozi Bw. Mbaga akiwa na mkewe wakati wa kutoa ahadi yao.
Mwenyekiti mstaafu wa WWI na mzee wa kanisa Mama Kuchu akiahidi.
Katibu wa kanisa Bwa. Gideon akiahidi.
Mzee wa Kanisa na pia mlezi wa kwaya ya Majestic Bw. Zegezege akipeana mkono na mgeni rasmi mara baada ya kutoa ahadi yake.
Mwenyekiti akiahidi
Katibu Grace Masebo akiwa na mumewe nao pia waliahidi.

Waumini mbalimbali waliojitokeza na kuahaidi.

















Pamoja kufanya zoezi hili la changizo kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya Mchungaji bado WWI  waliona si vema wakamtegemeza Mchungaji peke yake kwani wapo viongozi wengine ambao huambatana nae  madhabahuni ambao nao walipewa zawadi ya shamba la eka moja kwa kila mmoja






Mgeni rasmi akipokea zawadi iliyoandaiwa maalumu kwa ajili yake.
 Mara baada ya zoezi hilo kuisha mgeni rasmi aliomba kuondoka kutokana na kuwa na majukumu mengi ya kikazi lakini kabla hajaondoka mchungaji alimfanyia maombi.
Sherehe hii haikuishia hapo kwani baada ya shughuli zote hizi mchungaji pamoja na wageni waalikwa waliungana kwaajili ya chakula cha jioni.


Bufee ya watu  ya 3000 waliohudhuria sherehe hiyo..

Na huu ndio ukumbi wa V.I.P



Mchungaji akiwana wageni waalikwa katika chakula cha pamoja

















0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Eagt City Centre Blog 2013. Powered by Blogger.

About Me

My photo
Jicho langu latoka machozi lisokome,wala haliachi;Hata BWANA atakapoangalia. Nakutazama toka mbinguni Maombolezo 3:49-50

Followers

Featured Posts

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget