SILAHA
NANE ZA KUFUNGUA MILANGO NA MALANGO YALIYOFUNGWA MBELE YAKO;
SILAHA
YA TANO
REJESHA
KILA KILICHOKUWA KIMECHUKULIWA;
Katika
hatua hii ya tano, ni hatua ya urejesho maana baada ya kuokolewa Kristo Yesu
amekusudia kuturejeshea Baraka na Ustawi. Maandiko matakatifu
yanathibitisha kwa kinywa cha nabii Isaya; “BWANA
akapendezwa, kwaajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha. Lakini
watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa, wote wamenaswa katika mashimo,
wamefichwa katika magereza, wamekuwa mawindo wala hapana aokoaye, wamekuwa
mateka wala hapana asemaye rudisha. Ni nani miongoni mwenu atakaye tega sikio
lake kuyasikia hayo? Atakayesikiliza na kusikia kwa wakati ujao? Ni nani
aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang’anyi?
Si yeye, BWANA? Yeye tuliyemkosa, ambaye hakutaka kwenda katika njia zake, wala
hawakuitii sheria yake.” Isaya 42:21-25
BWANA anasema wazi wazi yakuwa wako watu
walioibiwa Baraka zao na ustawi, wengine wameibiwa ufaulu na uelewa wao katika
masomo,wengine wameibiwa uchumi na utajiri wao, wengine wameibiwa ndoa zao na
mengine mengi yanayofanana na haya. Lazima tusimame ndani mwa maombi na kurejesha kila kilichoibiwa na adui
shetani. Maombi ugeuza hali pale watu wa Mungu wanapoomba kwa nia moja na moyo
mmoja, hakika Mungu atafungua. Tunajifunza kwa wana wa Israeli kipindi cha
nabii Samweli jinsi walivyoinuka, wakamlilia BWANA naye akawaitikia. Nakuwafadhaisha
maadui zao. Maandiko yanathibitisha katika kitabu cha Samweli; “Samweli
akasema, Wakusanyeni Israel wote Mispa, name nitawaombea ninyi kwa BWANA.
Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji na kuyamimina mbele za BWANA; wakafunga
siku ile, wakasema huko, tumemfanyia BWANA dhambi. Samweli akawaamua wana wa
Israeli huko Mispa. Hata Wafilisti waliposikia ya kuwa wana wa Israeli
wamekusanyika huko Mispa, mashehe wa Wafilisti walipanda juu ili kupigana na
Israeli. Nao wana wa Israeli waliposikia, wakawaogopa Wafilisti. Wana wa
Israeli wakamwambia Samweli, Usiache kumlilia BWANA, Mungu wetu kwa ajili yetu,
kwamba atuokoe na mikono ya Wafilisti. Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo
mchanga, akamtolea BWANA sadaka ya kuteketezwa nzima, Samweli akamlilia BWANA kwa
ajili ya Israeli, BWANA akamwitikia. Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka
ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; walakini BWANA
akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, juu ya Wafilisti siku ile,
akawafadhaisha, nao wakaangamizwa mbele ya Israeli. Nao watu wa Israeli
wakatoka Mispa, wakawafuatia Wafilisti, wakawapiga hat walipofika chini ya Beth-kari. Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha
kati ya mispa na Sheni, akaliita jina lake Eben-ezeri, akasema, Hata sasa BWANA
ametusaidia.hivyo Wafilisti walishindwa, wasiingie tena ndani ya mipaka ya
Israeli; na mkono wa BWNA ulikuwa juu ya Wafilisti siku zote za Samweli. Nayo
miji ile Wafilisti waliyokuwa wamewapokonya Waisraeli ilirudishwa tena kwa
Israeli, tokea Ekroni mpaka Gathi, na Waisraeliwakaukoa mpaka wake mikononi mwa
Wafilisti. Tena kulikuwa na amani kati ya Israeli na Waamori. Naye huyo Samweli
akawaamua Israeli siku zote za maisha yake.” 1 Samweli 7:5-14
Israeli chini ya Nabii Samweli, BWANA
aliwashindia vita katika kusanyiko la Maombi ya kufunga. Maana wakati Samweli
anatoa sadaka na dhabihu ya jioni madhabahuni pa BWANA; ikapigwa ngurumo na
mshindo mkuu toka kwa BWANA ambao uliwafadhaisha Wafilisti ndipo Israeli
wakashinda vita, baada ya kushinda ndipo wakarejesha yote yaliyokuwa yametekwa
na Wafilisti. Nasi ndani mwa Maombi haya lazima turejeshe kila kilichochukuliwa
na adui. Kama ni afya yako sharti uombe kwa Imani ukirejesha. Maana BWANA
anasema, nitakurudishia afya, nitakuponya jeraha zako… Hata kama umeumwa sana
lazima Uombe urejeshewe afya yako. “Naye atakurejezea uhai wako, na kukuangalia
katika uzee wako, kwa maana mkweo ambaye akupenda, naye anakufaa kuliko watoto
saba, ndiye aliyemzaa.” Ruthu
4:15
BWANA kabla ya kuwaokoa wana Israeli
toka utumwani Misri, alipiga miungu ya Farao kwa mapigo kumi lakini kabla ya
pigo ya mwisho, alimwambia Musa awaambie wana wa Israeli watake mali, toka kwa
Wamisri naye BWANA atashusha nguvu ya kuwafanya Wamisri warejeshe mali mengi na
utajiri kwa wana wa Israeli. “Basi nena wewe masikioni mwa watu hawa, na
kila mtu mume na atake kwa jirani yake, na kila mwanamke atake kwa jirani yake,
vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu.” Kutoka 11:2
Malango ya Uchumi yatafunguliwa pale tu
Mwombaji sharti kwanza atake mbele za Mungu kwa Imani. Lipo sikio linalosikia
Maombi, Lazima Mali zilizofichwa na adui gizani, tuzitoe na turejeshe katika
milki yetu.“Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja
vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; nami
nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua
ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.” Isaya 45:2-3
BWANA anasema atakufungulia Malango na
Milango mbele yako, naye atakupa hazina, utajiri usio pimika, wewe na uzao wako
maana wote walio kuonea watafadhaishwa naam wametahayarika mbele yako. Chukua
hatua ya kuamini, Mali zako, Utajiri wako uje mikononi mwako maana Mungu
aliyeziumba Mbingu na Nchi, yeye ndiye Mungu wako ataufanya Imara Uchumi wako,
Hakutakuwa tena ndani mwako kufa-kufa na kuzaa mapooza.“kwa nafsi yangu nimeapa, neno
hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele
zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.” Isaya 45:23
Ayubu anasema nimeomba BWANA, amesikia,
nimemlilia yeye kwa sababu hiyo Mungu atamfanya mjane na yatima wabarikiwe na
wataimba nyimbo za furaha badala ya maombolezo. Usiogope, Lango lako
limefunguliwa, Rejesha Ustawi wako. Usikae kimya, Omba urejesho kwa nguvu.
Mtumishi wa Mungu Ayubu, anaomba Mungu baada ya kufilisika, hana kitu, lakini
anaomba tena Ustawi wa Mali zake.“Maana sikio liliponisikia, ndipo
likanibarikia; Na jicho liliponiona, likanishuhudia. Kwa sababu nalimuokoa
maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.
Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia, nikaufanya moyo wa mjane
kuimba kwa furaha.” Ayubu
29:11-13
Lazima Mali zetu zitapikwe na wachawi
walio tumeza lazima tuwakanyage matumbo yao kwa nguvu, tuwatapishe UTAJIRI wetu
na HESHIMA. Baada ya Maombi haya, tutang’aa kama dhahabu mbele ya maadui zetu;
maana BWANA anaugeuza uteka wako kuwa Baraka na Ustawi; ustawishwe na Uinuliwe
na Urejeshewe Heshima. “Utukufu wangu utakuwa mpya, Na uta wangu
hurejezwa upya mkononi mwangu.” Ayubu
29:20
Yeye aliyemeza mali ataitapika, maana
BWANA ataitoa tumboni mwake. “Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu
atayatoa tumboni mwake.” Ayubu
20:15
HESHIMA
AU CHEO
Esta 3:13-15
“Barua
zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza
Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na
wanawake pia, siku moja yaani siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili
ndio mwezi wa Adari, na kuyachukuamali yao kuwa nyara. Nakili ya andiko, ya
kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa yote wawe tayari siku
ile ile. Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa
mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai, bali
mji wa Shushani ukafadhaika.”
Esta na Modekai wanachukua hatua ya
Kufunga na Kuomba. wakachukua hatua ya kuifuata Heshima yao kwa mfalme
Ausuwelo. Esta akaingia kwa mfalme, ndipo Heshima ya Wayahudi ikarejeshwa, Aibu
zao, Huzuni zao zikatenguliwa. “Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo
Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku
wala mchana, name na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kasha nitaingia kwa
mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia na niangamie.” Esta 4:16
Ombea
Uzao wako
“Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu
zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi
na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa;
kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu
wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu moyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu siku
zote.” Ayubu 1:5
Esta; alisimama na kweli, Mungu akatenda
0 comments:
Post a Comment