Friday 26 May 2017

 kila mmoja sasa ni zamu ya kuombewa kwa kuwekewa mikono na mchungaji Florian Josephat katunzi ndani ya kanisa ambapo alifundisha neno la nguzo ya urejesho.

 mchungaji Florian Katunzi akifundisha neno la Mungu ndani ya Kanisa la EAGT lilopo mtoni mtongani.
 Mchungaji Florian katunzi akiwaombea baadhi ya watu waliodondoka wakati wa ibada ya maombezi ndani ya kanisa la EAGT City Center.

sasa ni wakati wa kila mmoja kuombewa na mchungaji katunzi ambapo watu mbalimbali walifika na kuanza kupita madhabahuni kuombewa
 mchungaji Florian Katunzi wa EAGT City Center  akiwa na mchungaji msaidizi  Sospeter Mgema wakati wa kuanza ibada ya maombi na maombezi.
 ni wakati wa maombi na maombezi sasa ni zamu ya kila mmoja kujiombea wakati ibada ya maombezi na maombi haijaanza.

Kila mmoja kujiombea ndani ya kanisa la EAGT chini ya mchungaji Florian Katunzi
Na Stelius Sane,
Imebainika kuwa asilimia kuwa ya waumini wamekuwa wakipitia katika mapito magumu ya kukatisha tama na kushindwa kuinuliwa na kufanikiwa kutokana na mafungo mbalimbali yaliyowafunga na kuwafanya kushindwa kustawishwa.
Hayo yalisemwa na mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT City Center lilopo mtoni mtongani jijini Dar es salaam,mchungaji Florian Katunzi ambapo alisema kuwa kuna mafungo ambayo imewakwamisha katika njia zao ya ustawisho.
Aidha mchungaji Katunzi alisema kuwa katika taifa la Tanzania kuna makaburi ambayo ni kukosekana kwa mvua hakuna kustawishwa wala kuinuliwa ila sasa Mungu anaende kutenda na kufufua kazi ya mikono ya kila mtanzania ambaye atasimama katika nafasi yake na kumtafuta Mungu wa kweli kwa bidii bila kujali kuwa umezikwa kwa muda gani.
Mchungaji katunzi aliongeza kuwa akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la Bwana. Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi.Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. 
Aidha aliendelea kunukuu na kusema kuwa Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake. Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi. 

Hata hivyo aliendelea kuwa Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa.Basi tabiri, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli. 
Pamoja na hayo alifafanua kwa kunukuu kuwa  Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu.Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimesema hayo, na kuyatimiza, asema Bwana. 
Akifafanua kwa undani juu ya nguzo hiyo ya pili ambayo ni imani alisema kuwa ni njia ya kupokea kutoka kwa Mungu ambayo ni kule kumtumainia Mungu katika hali zote na kuishi katika neon maana chanzo cha nguzo hii ni nguzo ya kwananza ambayo ni neno la Mungu.
Kuomba kwa imani inasababisha jambo kutendeka kama vile neno linavyosema maana ukitumia nguzo hii unafanikiwa na kuwa katika viwango vingine sawa na kitabu cha Waebrania 11:1-2  Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana,Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. 
Katika kitabu cha Ezekieli alipokuwa akizungumzia mifupa mikafu ikimaanisha ni hali ya ukame ambayo inaweza kuwa ni ukame katika huduma yako,elimu yako,maisha yako na pia inawezekana ni ukame katika kila unachofanya kwa mikono yako.
Kutabiri ikiashiria ni kuomba kwa imani juu ya hali yako unayopitia na kusababisha kukata tamaa na kuona kama haiwezekani sasa ni wakati wako kusimama na kutabiria maisha yako ili ufanikiwa na kuinuliwa katika kila jambo unalofanya  Mchungaji katunzi akinukuu kitabu cha Warumi 10:17 alisema kuwa Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. 
Katika maisha ya kina mwanadamu inawezekana kuna vitu vimekukandamiza na kukumiza na kukufanya ushindwe kufanikiwa sasa ni zamu ya kuinuliwa bila kujali walikuzika na kukufunga kwa njia gani.

“Yakobo 1:22 inasema kuwa Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”alinukuu mchungaji katunzi
Aliongeza kuwa kuna baadhi ya watu wanasikiliza neno la Mungu lakini hawalifanyii kazi badala yake wanabaki tu maana cha cha imani ni kusikia,neno la Mungu na ukiwa msikiaji na hutendei kazi matokeo yake unabaki kudumaa katika maisha.
Inawezekana umezikwa katika makaburi ya babu zenu na ukoo zetu kwa kuchukua nywele na kucha zenu na kuzika unaonekakna unaishi lakini maisha yako yamezikwa katika makaburi sasa ni wakati wa kuwekwa huru.
Hata kama umezikwa kiasi kwamba hata huwezi kufanikiwa katika kila unachokifanya Mungu wa kweli kwa jina la Yesu unafunguliwa hata kama wamekupa majina kutokana na tatizo unalopitia unawekwa huru na kufanikiwa .


“Katika taifa la Tanzania kuna makaburi ambayo ni kukosekana kwa mvua hakuna kustawishwa wala kuinuliwa ila sasa Mungu anaende kutenda na kufufua kazi ya mikono ya kila mtanzania ambaye atasimama katika nafasi yake na kumtafuta Mungu wa kweli kwa bidii bila kujali kuwa umezikwa kwa muda gani”alisema mchungaji katunzi.
Katika taifa kama ikikosekana Mvua ama mafanikio biblia inasema kuwa waumini waliomtambua Bwana Yesu kama mwokozi wa maisha yao kuomba kwa bidii na Mungu anatenda maana yeye anatenda anyefahamu maisha ya kila mwanadamu.
Akinukuu kitabu cha Zekaria 10:1 inasema kuwa Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni. 
“Ni wakati wako kusimama na kumwomba Mungu alete mafanikio na kleta mvua ya Baraka itakayoleta ustawisho na mafanikio na sio mvua zenye madhara”, alisema mchungaji Katunzi.
Ni wakati wa kusimama na kutenda kwa imani maana ni nguzoo ya pili ya urejesho itakayokusaidia kutekeleza na kufanikiwa kiuchumi na katika kazi ya mikono yako.
Msomaji unaweza kufuatilia kipindi cha saa ya ushindi na kufunguliwa kupitia runinga ya chanel Tena kuanzia saa mbili na nusu usiku na kurudiwa jumatano saa kumi na moja jioni na kusikiliza wapo redio kila jumapili saa nne kamili hadi saa tano na kurudiwa jumatatu saa sita mchana
Ama tembelea pastorkatunzi.blogspot.com
Kwa mawasiliano 0784367826,0754367826
Na 0718267171



0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Eagt City Centre Blog 2013. Powered by Blogger.

About Me

My photo
Jicho langu latoka machozi lisokome,wala haliachi;Hata BWANA atakapoangalia. Nakutazama toka mbinguni Maombolezo 3:49-50

Followers

Featured Posts

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget