Thursday 29 December 2016

Mtu aliyebebelewa ni mgonjwa ambaye ameletwa kanisani akiombewa na mchungaji Florian Katunzi katika ibada iliyofanyika ndani kanisa hapo hivi karibuni.
 
 mchungaji Katunzi akishangaa moja ya vitendea kazi vya kichawi ambazo Hassan alivikabidhi Kwake baada ya maombi ya nguvu za Mungu kanisani hapo



 Hassani akionesha baadhi ya vitendea kazi vya kichawi  ndani ya kanisa hilo.




Ndugu Hassa akionesha Pembe ya Kolongo Ndani ya kanisa la EAGT City Center.

vifaa vinavyodaiwa kuwa ni vya kichawi mali ya mtu mmoja aliyejulikana nkwa jina moja la hassan mkazi wa mbagala akivikabidhi kwa mchungaji Katunzi baada ya kusikia injili kupitia Wapo redio siku ya jumamosi.

 mchungaji Katunzi akimwongoza sala ya toba Hassan baada ya kukabidhi vifaa vya kichawi kanisani hapo baada ya maombi alifunguliwa na sasa yupo huru

 mchungaji Katunzi akishangaa moja ya vitendea kazi vya kichawi ambazo Hassan alivikabidhi Kwake baada ya maombi ya nguvu za Mungu kanisani hapo.


 mchungaji Florian katunzi akiwa katika picha ya pamoja na waumini walifunguliwa kutoka katika mateso na mafungo mbalimbali.
 Kutokana na baadhi ya changamoto za maisha wanazokumbana nazo watu wa Mungu na kupitia vipindi vigumu vya maisha  imeelezwa kuwa haijalishili unaishi katika maisha magumu kiasi cha kukata  tamaa bado Mungu anawapenda na yupo tayari kuwasaidia na kuwatoa katika matatizo ambayo wanalipitia.
kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na mchungaji kiongozi Floriani Katuniz  wa kanisa la EAGT City center lililpo Mtoni mtongani jijini Dar es salaam ambapo alisema kuwa mambo ya msingi ya kiimani yanatakiwa kusimamiwa na kufuata taratibu za Mungu kulingana na kitabu cha marko 5:21-24 , Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng'ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake,akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi.Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa. 
"Inawezekana maisha yako hayaendelei kila unachokigusa hakuna mafanikia jambo ambalo linatakiwa kumlilia Mungu ili afungue milango ya baraka na kufanikiwa sawa sawa na kitabu cha Zaburi 107:13-14,   Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.Aliwatoa katika giza na uvuli wa mauti, Akayavunja mafungo yao. sasa inawezekana unapitia katika mapito magumu umekata tamaa umeona kuwa haiwezekani ila utakapo amua kumlilia Mungu katika mapito yako atakuonekania na kukusaidia na kukufungua katika mateso ya pepo wachafu"Alisema Katunzi.
Aliongeza kuwa kuna watu ambao biashara zao zinakufa na kuzaa mapooza jambo ambalo adui ameamua kuwavuruga na kuangamiza hivyo siku ya tarehe nane mwezi wa nane  itakuwa ibada ya kuwaombea wafanya biashara na wafanya kazi ambao kazi na biashara zao zimekuwa zikizaa mapooza zinaenda kuinuliwa na Mungu wa kweli anaaenda kukubariki na kukuinua.
"tukisoma kitabu cha 2 wafalme 2:19-22 inasema kuwa  Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena sasa Mungu anaenda kukutendea sawa sawa na neno lake. inawezekana kuwa biashara ,kazi yako na afya yako imefukiwa sasa ni wakati wa kuinuliwa na kuanza kuzaa matunda".alisema Katunzi.
Alinukuu kitabu cha mwanzo  26:1-22 Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari. Bwana akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia. Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako. Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia. Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu Isaka akakaa katika Gerari. Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso. Ikawa alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, akachungulia dirishani, akamwona Isaka anacheza-cheza na Rebeka mkewe.Abimeleki akamwita Isaka, akasema, Yakini huyu ni mkeo, mbona ulisema, Ni ndugu yangu huyu? Isaka akamwambia, Kwa sababu nalisema, Nisife kwa ajili yake Abimeleki akasema, Ni nini hii uliyotutendea? Labda mtu mmojawapo angalilala na mkeo bila kufikiri, nawe ungalitutia hatiani. Basi Abimeleki akawaamuru watu wote, akisema, Amgusaye mtu huyu au mkewe lazima atauawa.Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, Bwana akambariki.Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana. Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng'ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu. Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Ibrahimu babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza kifusi. Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi. Basi Isaka akatoka huko akapiga kambi katika bonde la Gerari, akakaa huko. Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye. Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika. Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye.Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna. Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi. 
maombi ya kuvunja mafungo kipengele cha kuvunja mauti ndiyo somo ambalo mtumishi wa Mungu mchungaji Katunzi alifundisha ndani ya kanisa la EAGT City Center kwa wiki mfululizo
mchungaji Katunzi alinukuu kitabu cha Mathayo 9:18-26 ambayo inasema kuwa alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi. Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake.Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake. Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile. Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo, akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana. Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule kijana akasimama. Zikaenea habari hizi katika nchi ile yote. 
Mmoja wa mtu ambaye amefahamika kwa jin a moja la Hasani mkaazi wa mbagala ametoa ushuhuda jinsi alivyokuwa akisikiliza redio wapo na Mungu akamtembelea kwa namna ya kipekee na akaamua kusalimisha vifaa vya uchawi ambayo ni pembe kubwa ya faru mdogo na ya swala pia mkuki ambayo wao kichawi wanita mshale kwa ajili ya kupambana nayo kwenye vita kichawi hirizi sita ambazo zimepotea na dawa ya kujipaka na kuruka akitaka kuruka na alikiwa na uwezo wa kujibadilisha.
Mara baada ya kuombewa sala ya toba bibi yake ambaye ni mrehemu alimtembelea usiku na kumwambiakwa nini ameamua kufanya mkaamuzi hayo magumi bila kumshirikisha sasa kutokana na hayo alimpa pembe ndogo ambayo itamsaidia pale atakapotumiwa wanyama wakati anaweza kujigeuza a kuwa mnyama mkali kuliko wote na kupambana nao na ndiyo kilichomtokea usiku wa kuamkia jumamosi alipambana na wanyama wakali ila yeye alijigeuza na kuwa chui na kupambana nao na kuwaua wengine.
Pia unaweza kuwasiliana na kanisa la EAGT City center na namba  0784367826,0754367826 na 0718267171 pia tembelea  www.pastorkatunzi.blogspot.com au tovuti ya www.eagtcc.org


0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Eagt City Centre Blog 2013. Powered by Blogger.

About Me

My photo
Jicho langu latoka machozi lisokome,wala haliachi;Hata BWANA atakapoangalia. Nakutazama toka mbinguni Maombolezo 3:49-50

Followers

Featured Posts

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget