SILAHA
NANE ZA KUFUNGUA MILANGO NA MALANGO YALIYOFUNGWA MBELE YAKO;
SILAHA
YA NNE
INUKA
KWA IMANI
Malango ya Israeli yalifungwa muda wa
miaka ishirini, Mashujaa walikoma, Watu walionewa kwa nguvu za Sisera muda wa
miaka ishirini, lakini Sisera alikomeshwa na mwanamke wa Imani Debora
aliyeinuka akaongoza vita dhidi ya Sisera Wana wa Israeli wakamlilia BWANA; kwa kuwa
Sisera alikuwa na magari ya chuma mia kenda, naye akawaonea wana wa Israeli kwa
nguvu muda wa miaka ishirini. Katika
siku za Shamgari, mwana wa Anathi, siku za Yaeli, njia kuu zilikuwa hazina
watu; Nao wenye kusafiri walipita kwa njia za kando. Maliwali walikoma katika
Israel, walikoma, Hata mimi Debora nilipoinuka, Nilipoinuka mimi, mama katika
Israeli.
hakika kwa mkono wa BWANA Sisera
alianguka. Maandiko matakatifu yanathibitisha waziwazi na kusema;
“Hata alipokufa Ehudi wana wa Israeli wakafanya
yaliyo maovu tena mbele za macho ya Bwana. Bwana akawauza na kuwatia katika
mkono wa Yabin Mfalme wa Kaanani aliyetawala huko Hazori na sisera aliyekaa
katika harosheth wa mataifa, alikuwa amiri wa jeshi lake. Wana wa Israel
wakamlilia Bwana kwakuwa sisera alikuwa na magari ya chuma mia kenda, naye
akawaonea wana wa Israeli kwa nguvu muda miaka ishirini. Basi Debora nabii mke
mkwewe Lapidoth ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule. Naye alikaa
chini ya mtende wa Debora kati ya Rama na Bethel katika nchi ya vilima vilima
ya Efreaim, Wana wa Israeli wakakwea kwake awaamue. Huyo akatuma mtu akamwita
Baraka wa Abinoam toka Kedeshi naftari akamwambia je! Bwana Mungu wa Israel
hakutoa amri? Akisema enenda ukawavute kwako huko katika mlima wa Tabora, watu
elfu kumi wa wana wa Naftari na wana wa Zabron. Nami nitakuvutia Sisera amiri
wa jeshi lake Yabin hata mto wa kishon pamoja na magari yake na wingi wa watu
wake nami nitamtia mkononi mwako. Baraka akamwambia, kama utakwenda pamoja nami
ndipo nitakwenda bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi. Basi akasema,
hakika nitakwenda pamoja nawe lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima
wewe maana Bwana atamuuza Sisera katika mkono wa mwanamke Debora, akainuka
akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedesh. Baraka akawakutanisha Ftari na Zabron
waende Kedesh wakakwea watu elfu kumi wakimfuata Debora, naye akaenda pamoja
naye. Basi heberi, mkeni alikua amejitenga na wake yaani na wana wa Hobab
Shemeji yake Musa, akaipiga hema yake mbali penye mualoni uliopo saa na imu
karibu na Kedesh. Watu wakamwambia Sisera yakwamba Baraka mwana wa Abinoam
amekwea kwenda mlima wa Tabora. Sisera akayakusanya magari yake yote, naam
magari ya chuma ni ya kenda na watu wote waliokuwa pamoja naye toka herosheth
wamataifa mpaka mto wa kishon. Debora akamwambia Baraka, haya? Inuka maana siku
hii ndiyo siku ambayo Bwana amemtia Sisera katika mkono wako, Je! Bwana
hakutoka atangukie mbele yako? Basi Baraka akashuka katika mlima wa Tabora na
watu elfu kumi wakamfuata. Bwana akamfadhaisha Sisera na magari yake yote, na
jeshi lake lote, kwa makali ya upanga, mbele ya Baraka; basi Sisera akashuka
katika gari lake, akakimbiakwa miguu. Lakini Baraka akayafuatia magari, na
jeshi, hata Haroshethi wa Mataifa, na hilo jeshi lote la Sisera likaanguka kwa
makali ya upanga; hakusalia hata mtu mmoja.lakini Sisera akakimbia kwa miguu,
akaifikilia hema ya Yaeli mkewe Heberi, Mkeni; kwa maana palikuwa na amani kati
ya Yabini, mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi, Mkeni. Yaeli akatoka kwenda
kumlaki Sisera, akamwambia, Karibu Bwana wangu, usiogope. Akakaribia
kwake hemani, naye akamfunika kwa
bushuti. Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe; maana nina kiu,
Akafungua chupa ya maziwa, akampa kunywa, akamfunika. Naye akamwambia, Simama
mlangoni pa hema; kasha itakuwa mtu awaye yeyote akija na kukuuliza, akisema,
Je! Yupo mtu hapa, basi, mjibu, La, hapana. Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa
kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia
kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa
maana usingizi mzito ulikuwa umemshika, basi akazimia, akafa. Na tazama, Baraka
alipokuwa akimfuatia Sisera; Yaeli akatoka ili kumlaki, akamwambia, Njoo, nami
nitakuonyesha yule mtu unayemfuata. Basi akamwendea, na tazama, Sisera amelala
humo, amekufa, na hicho kigingi kilikuwa kipajini mwake. Basi hivyo Mungu
akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani mbele ya wana wa Israeli siku hiyo. Mkono
wa wana wa Israeli ukazidi kupata nguvu juu ya Yabini, mfalme wa Kanaani, hata walipokuwa
wamemuangamiza Yabini, mfalme wa Kanaani.” Waamuzi 4:1-24
“Debora akamwambia Baraka, Haya!
Inuka; maana siku hii ndiyo siku ambayo
BWANA amemtia Sisera katika mkono wako. Je! BWANA hakutoka atangulie mbele
yako? Basi Baraka akashuka katika mlima wa Tabora, na mtu elfu kumi
wakamfuata.” Waamuzi 4:14
Malango na milango itakufungukia pale
utakapoinuka kwa silaha ya imani “
KUINUKA KWA IMANI.” Neno Inuka lina maana kubwa sana, angalia miaka nenda
rudi Mwanamke huyu amekuwa tasa na kila mwaka alikwenda Hekaluni kusali na
kutoa sadaka mbele za Mungu aliye hai lakini aliendelea kuwa tasa, mlango wake
wa uzazi ulifungwa. Wako watu watu wengi wanasali, wanatoa sadaka lakini
Malango na Milango imefungwa mpaka wachukue hatua ya “Kuinuka wenyewe wa
imani” Hana akainuka toka kwenye Utasa na Ugumba, akamwendea BWANA kwa
Maombi mazito. Yenye kufungua milango na malango, na alipoinuka alikutana
na BWANA, hakika ukawa ndio mwisho wa huzuni zake. Tunasoma maandiko yanasema; “Palikuwa
na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake
akiitwa Elkana, mwana wa yerohamu, mwana wa Sufu, Mwefraimu, naye alikuwa na
wake wawili, jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina,
naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto. Na mtu huyo
alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea
BWANA wa majeshi dhabihu katika Shilo, Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na
Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwako huko. Hata siku ile ilipofika Elkana alipotoa dhabihu, kumpa mkewe Penina sehemu,
akawapa na watoto wake wote, waume kwa wake, sehemu zao; lakini Hana humpa
sehemu mara mbili; maana alimpenda hana, ingawa BWANA alikuwa amemfunga tumbo.
Ila mwenzake humchokoza sana, hata kumsikitisha, kwa sababu BWANA alikuwa
amemfunga tumbo. Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke
alipokwea kwenda nyumbani kwa BWANA, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa
hiyo, yeye akalia, asile chakula. Elkana mumewe akamwambia, Hana, unalilia
nini? Kwani huli chakula? Kwa nini moyo una huzuni? Je! Mimi si bora kwako
kuliko watoto kumi? Ndipo Hana akainuka, walipokwisha kula na kunywa huko
Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake penye mwimo wa hekalu la
BWANA. Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA wa
majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala
usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo
mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe
hautamfikilia kichwani kamwe. Ikawa, hapo alipodumu kuomba mbele za BWANA, Eli
akamwangalia kinywa chake. Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake
tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo eli alimdhania kuwa
amelewa. Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai
yako. Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho
ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za
Bwana. Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa kitu; kwa kuwa katika
wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo nilivyonena hata sasa. Ndipo
Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako
uliyomwomba. Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo
mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena.
Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za BWANA, kisha wakarejea na
kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka.
Ikawa wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume;
akamwita jina lake Samweli, akisema, kwa kuwa Nimemwomba kwa BWANA. Kisha yule mtu, Elkana, na watu wote wa nyumbani mwake, wakakwea kwenda
kumtolea BWANA dhabihu ya mwaka, na nadhiri yake. Bali Hana hakukwea; maana
alimwambia mumewe, Sitakwea mimi hata mtoto wangu atakapoachishwa maziwa, hapo
ndipo nitakapomleta, ili ahudhurie mbele za BWANA, akae huko daima. Elkana,
mumewe, akamwambia, Haya, fanya uonavyo vema; ngoja hata utakapomwachisha
maziwa; BWANA na alithibitishe neno lake tu. Basi yule mwanamke akangoja,
akamnyonyesha mtoto wake, hata akamwachisha maziwa. Naye alipokuwa amekwisha
kumwachisha maziwa, akamchukua pamoja naye, na ng’ombe watatu, na efa moja ya
unga, na chupa ya divai, akamleta nyumbani kwa BWANA, huko Shilo; na yule mtoto
alikuwa mtoto mdogo. Nao wakamchinja huyo ng’ombe, wakamleta mtoto kwa Eli.
Akasema Ee bwana wangu, kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mimi ndimi yule
mwanamke aliyesimama karibu nawe hapa, nikimwomba BWANA. Naliomba nipewe mtoto
huyu; BWANA akanipa dua yangu niliyomwomba; kwa sababu hiyo mimi name nimempa
BWANA mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa BWANA. Naye akamwabudu
BWANA huko.” 1Samweli 1:1-28
Ikawa hapo alipoendelea kuomba mbele za
BWANA, Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamuomba BWANA
akalia sana. Kuhani Heri akamwendea na kumtamkia neno la kumfungua
tumbo lake, naye akaenda nyumbani mwake, majira yalipotimia akampata mtoto
akamwita Samweli. Lazima uchukue hatua ya Kuinuka kuyaendea Malango na Milango
iliyofungwa mbele yako nayo itafunguka. Maana kila hatua unayoipitia na kila
hatua unayoichukuwa, BWANA ataifanikisha. Mtu wa Mungu usipoinuka utabaki vivyo
hivyo japo umeokoka. Kwa Imani lazima Uinuke umwendee Mungu naye atafanya njia
mbele yako ambayo wewe kwa macho ya kawaida huioni. Angalia watu hawa
wanne wenye ukoma, walichukua hatua ya KUINUKA KWA IMANI, na Mungu
akawasikizisha mbele ya maadui zao wakawa lango la ukombozi kwa taifa zima la
Israeli. Neno la Mungu linasema; “Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma,
penye lango la mji, wakasemezana, mbona tunakaa hapa hata tufe? Tukisema,
tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasdi tutakufa humo, nasi tukikaa hapa,
tutakufa vile vile. Haya twende tukaliendee jeshi la Washami, wakituhifadhi hai
tutishi, wakituua tutakufa tu. Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende
mpaka kituo cha Washami, na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe!
Hapana mtu. Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo
ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa, wakaambiana,
tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri,
waje wapigane nasi. Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado,
wakaziacha hema zao, na farasi zao na punda zao, na kimo chao vile vile kama
kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. Basi wale wenye ukoma
walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala na kunywa,
wakachukua fedha, na dhahabu na mavazi,
wakaenda wakavificha, wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile
wakachukua vitu, wakaenda wakavificha. Ndipo wakaambiana, mambo haya tufanyayo
si mema, leo ni siku ya habari njema nasisi tunanyamaza, tukingoja hata
kutakapopambazuka, madhara yatatupata, basdi twende tukawaambie watu wa nyumba
ya mfalme. Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji, wakawaambia, tulifika
kituo cha Washami, na tazama hapana mtu yeyote huko, wala sauti ya mtu ila
farasi wamefungwa, na punda wamefungwa na hema zao kama walivyoziacha. Na
mabawabu wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme. Mfalme akaondoka usiku,
akawaambia watumishi wake, sasa nitawaonyesha ninyi walivyotutendea Washami.
Wanajua yakuwa tuna njaa, basi wametoka kituoni ili kujificha kondeni, wakisema
watakapotoka mjini, tutawakamata hai, tena tutapata kuingia mjini, na mmoja
wapo wa watumishi wake akajibu, akasema, kunradhi, baadhi ya watu na watwae
farasi watano katika hao waliosalia, waliobaki ndani ya mji (tazama wamekuwa
kama mkutano wote wa Israeli waliobaki ndani yake; tazama wamekuwa kama mkutano
wote wa Israeli walioangamia), tukawapeleka tukaone. Basi wakatwaa magari
mawili na farasi zake, mfalme akawatuma kuwafuata Washami, akasema, Enendeni,
mkaangalie. Wakawafuata mpaka Yordani na kumbe! Njia yote ilikuwa imejaa
mavazi na vyombo, walivyovitupaWashami,
wapate kukimbia upesi. Watu wale waliotumwa wakarudi, wakamwambia mfalme, basi
watu wakatoka, wakaziteka nyara hema za Washami. Ikawa kipimo cha unga mzuri
kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekel, sawasawa na
nenola BWANA. Naye mfalme akamweka yule akida, ambaye alitegemea mkono wa ke,
awasimamie watu langoni; na watu wakamkanyaga langoni, akafa, kama alivyosema
yule mtu wa Mungu, aliyenena hapo mfalme alipomshukia.ikatukia kama vile yule
mtu wa Mungu alivyomwambia mfalme, vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, na
kipimo cha unga mzuri kwa shekeli ndivyo vitakavyokuwa kesho, panapo saa hii,
katika lango la Samaria, na yule akida akamjibu mtu wa Mungu akasema, sasa
tazama kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana?
Akasema, angalia wewe utaliona kwa macho yako lakini hutakula.” 2 Wafalme 7:3-19
Watu hawa walitupwa nje ya lango la mji
wafe na njaa. “Wakaasemezana wao kwa wao;
mbona tunakaa hapa hata tufe?” Ili wasife ni lazima wachukue hatua ya
KUINUKA KIIMANI kutoka kwenye “Kifo”
Kwa sababu kwenye lango la Samaria mpaka ndani ya mji wa Samaria kulikuwamo
vifo vilivyotokana na njaa kali kiasi cha watu walikula watoto wao. Nje ya
Samaria kulikuwa na chakula, lakini kilikuwa mikononi mwa maadaui wa wana wa
Israeli. Ndipo wakoma hawa wakachukua hatua ya kukiendea kituo cha Washami kwa
Imani, wakainuka wakasema; “Haya twende tukaliendee jeshi la Washami,
wakituhifadhi hai, tutaishi na wakituua, tutakufa tuu.”
Wakainuka kwa Imani kungali bado
mapambazuko ili waende mpaka kituo cha Washami, lakini walipofika mwanzo wa
kituo cha Washami kumbe hamna mtu, Maadui wamekimbia mbele ya watu wenye
Ukoma, walioamua KUINUKA KWA IMANI. Angalia Mungu anapenda mtu anayechukua
hatua ya “KUINUKA KWA IMANI.”
Washami
walikimbia kwasababu; BWANA alikuwa amewasikizisha Washami
kishindo cha miendo ya magari na kishindo cha farasi kama kishindo cha jeshi
kubwa, Wakaambiana, tazama mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti na
wafalme wa Wamori waje wapigane nasi. “Kishindo” cha Mungu,
lazima kiambatane na mtu aliyekubali kuinuka kwa Imani. Nasi tukikubali kuinuka kwa Imani, kipo kishindo cha Mungu aliye
hai, kitawakimbiza maadui zetu wataacha Malango yetu na Malango ya Baraka
yakitufungukia.
Lazima kuinuka Kimaombi ndipo utasonga
mbele, naye Mungu atakushika mkono wako na kukuinua. “Bwana huzikomboa nafsi za watumishi
wake, Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao.” Zaburi 34:22
Tunapoendelea kuinuka kwa Imani
tunayafungua Malango na milango. “Maskini huyu aliita, BWANA akasikia,
akamuokoa na taabu zake zote. Malaika wa BWANA hufanya kituo pale aketipo,
akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.” Zaburi 34:6-7
Kuinuka na Kumwita Mungu kunafungua
Malango. Huu ni wakati wa Kuinuka tena Kiimani. Na kushika kazi za mikono ili
tupate kumilikishwa katika BWANA, ndiyo maana BWANA anatoa wito wa kuinuka na
kushika kazi sawasawa na neno lake; “Ya dhahabu, ya fedha, naya shaba naya
chuma, hapana hesabu, basi inuka ushike kazi, naye BWANA na awe pamoja nawe.”
1Mambo ya Nyakati 22:16
Mungu anatafuta mtu atakayeinuka na
kusimama mbele zake ili kuyafungua Malango na Milango iliyofungwa. Naye BWANA
atageuza ishara za waongo na wachawi zisitende kazi. Maandiko matakatifu
yabasema; “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na
kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi nisije nikaiharibu,
lakini sikuona mtu.” Ezekieli 22:30
Yatupasa kuinua watoto wetu, ndoa zetu,
biashara zetu, maisha yatu kwa ujumla mbele za Mungu aliye hai. Maana hayo
mateso hayatainuka tena mara ya pili. Inua Misingi yako ya uchumi iliyobomoka.
Pembe ya mwenye haki itainuka daima pale
atakapoiinua ndani mwa maombi. Maandiko yanasema; “Inueni vichwa vyenu, enyi
malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.”
Zaburi 24:9
Usikubali nafsi yako kuinama kwa huzuni,
bali Inuka uyafungue Malango yako nayo yatafunguliwa. “Pembe zote za wasio haki
nitazikata, Na pembe za mwenye haki zitainuka.” Zaburi 75:10
Daudi, anaomba anasema; “Amka,
utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, nitaamka alfajiri.” Zaburi 57:8
Vita vyote unavyopitia, utavishinda pale
utakapochukua hatua ya Imani ya kuyaendea malango ya adui katika Maombi na
kuyafisha.
Na
waangamie vivyo maadui zako, kama Sisera alivyoangamia mbele ya BWANA. Kwa mkono wa
Debora, mateso yalikomeshwa dhidi ya Israeli. Kwa muda wa miaka arobaini,
Israeli alistareheshhwa na BWANA. Heshima ya Israeli ilirejea tena kwa Imani
walipokubali kuinuka.
0 comments:
Post a Comment