Imeelezwa kuwa
katika kongamano la siku tisini watu mbalimbali waliokuwa na matatizo na shida
mbalimbali wamefunguliwa na kuwekwa huru na wengi wameshuhudia jinsi Mungu
alivyo wafungua katika taabu zao.
Akifundisha
katika kongamano hilo mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT City Center
Mchungaji Florian Katunzi alisema kuwa katika kongamano hilo kuna maombi ndani
mwa maombi ambao kuna vipengele
mbalimbali na kwa wiki hiii inahitimika na kiengele cha kumiliki na kutawala.
Aidha
alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanamilikuwa na matatizoa mbalimbali kama vile
magonjwa shida elimu jambo ambalo linawasasbabisha kushindwa kutekeleza
majukumu yao ya kila sai maana wamefungwa na kuwa chini ya vifungo hivyo.
Akinukuu
kitabu cha Isaya 26:11-14 ambapo alisema Bwana, mkono wako umeinuliwa, lakini
hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari;
naam, moto utawala adui zako. Bwana,
utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote. Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine
zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina
lako. Wao wamekufa, hawataishi;
wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza,
na kuupoteza ukumbusho wao.
Alisema kuwa
kama vile wana wa israeli walivyokuwa wakimilikiwa na farao siku ya kutoka
alipigwa kwa mapigo kumi na kuachia sasa na sasa kuna watu wanamilikiwa na
umaskini ,roho za ukahaba, roho za kutokuolewa, kutokuoa na pia kuna roho za ushoga
na usagali na ukiangalia utayaona kuwa hata katika ukoo wao kulikuwepo na
tatizo kama hilo ndani ya ukoo wao.
"maombi
ndani mwa maombi itakuwa ni maombi ambayo watu wataenda kukomesha matatizo na
shida mbalimbali ambazo zilikuwa zinakukabili na kukutesa,maana wale wote
waliokutesa kukuonea na kukutesa hwataishi",alisema mchungaji Katunzi.
Zaburi
107:13-14
ukishaokolewa
na kuokoka na kuacha dhambi sasa unahamishwa na kuanza kumilikishwa katika
maisha yako na utakuwa ukitawala katika maisha yako na hautateseka tena na alinukuu kitabu cha warumi 5:17 Kwa maana ikiwa kwa
kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao
wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa
yule mmoja, Yesu Kristo.
Alisema
kuwa huwezi kumiliki kama Bwana Yesu hayupo ndani ya maisha yako inatakiwa
kusimama kataika yeye na kumtegemea maana ndiye mwenye uwezo wa kukupa mamlaka
ya kuondoa matatizo na kukemea mapepo na matatizo mbali mbali na yanaondoka.
Baada
ya maombi haya ya kongamano watu wengi
wataanza kukushangaa na wengine watashangaa kukuona kuwa unaenda kuinuliwa na
kuacha umaskini katika maisha yako yote maana pale utakapookoka Mungu anaenda
kukubariki na kukufanikisha katika maisha yako na utakuwa mfano katika maisha
yako.
ukisoma
kitabu cha kutoka 11:1-3 inasema Bwana akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao
na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa
ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa. Basi nena wewe masikioni mwa watu hawa, na kila
mtu mume na atake kwa jirani yake, na kila mwanamke atake kwa jirani yake,
vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu. Bwana akawapa watu hao kibali machoni pa
Wamisri. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri,
machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake.
Hata hivyo aameongeza kuwa inachotakiwa ni kuhakikisha
unafuata taratizi za Mungu na pia inatakiwa ujifunze juu ya suala la uchumi
katika maisha yako unapoendelea na maombi na maombezi ili ufanikiwe na
kufanikiwa.
Kanisa la
eagt City Center limeanza kongamano la la siku tisini kuanzia april tatu hadi julai 3 mwaka huu na wangi
wameanza kufunguliwa na kuwekwa huru bila kuangalia dini dhehebu kanisa na
kabila mbalimbali.
unaweza
kuwasiliana na kanisa la EAGT City center na namba 0784367826,0754367826 na 0718267171 pia
tembelea www.pastorkatunzi.blogspot.com
au tovuti ya www.eagtcc.org
0 comments:
Post a Comment