Imeelezwa kuwa katika kongamano la siku tisini watu
mbalimbali waliokuwa na matatizo na shida mbalimbali wamefunguliwa na kuwekwa
huru na wengi wameshuhudia jinsi Mungu alivyo wafungua katika taabu zao.
Akifundisha katika kongamano hilo mchungaji kiongozi wa
kanisa la EAGT City Center Mchungaji Florian Katunzi alisema kuwa katika
kongamano hilo kuna maombi ndani mwa maombi ambao kuna vipengele mbalimbali na kwa wiki hiii
inahitimika na kiengele cha kumiliki na kutawala.
Aidha alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanamilikuwa na
matatizoa mbalimbali kama vile magonjwa shida elimu jambo ambalo
linawasasbabisha kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kila sai maana wamefungwa
na kuwa chini ya vifungo hivyo.
Akinukuu kitabu cha Isaya
26:11-14 ambapo alisema Bwana, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini
watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala
adui zako. Bwana, utatuamuria
amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote. Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine
zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina
lako. Wao wamekufa, hawataishi;
wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza,
na kuupoteza ukumbusho wao.
Alisema kuwa kama vile wana wa israeli walivyokuwa
wakimilikiwa na farao siku ya kutoka alipigwa kwa mapigo kumi na kuachia sasa
na sasa kuna watu wanamilikiwa na umaskini ,roho za ukahaba, roho za kutokuolewa,
kutokuoa na pia kuna roho za ushoga na usagali na ukiangalia utayaona kuwa hata
katika ukoo wao kulikuwepo na tatizo kama hilo ndani ya ukoo wao.
"maombi ndani mwa maombi itakuwa ni maombi ambayo watu
wataenda kukomesha matatizo na shida mbalimbali ambazo zilikuwa zinakukabili na
kukutesa,maana wale wote waliokutesa kukuonea na kukutesa hwataishi",alisema
mchungaji Katunzi.
Zaburi 107:13-14
ukishaokolewa na kuokoka na kuacha dhambi sasa unahamishwa
na kuanza kumilikishwa katika maisha yako na utakuwa ukitawala katika maisha
yako na hautateseka tena na alinukuu
kitabu cha warumi 5:17 Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa
sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa
cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.
Alisema kuwa huwezi kumiliki kama
Bwana Yesu hayupo ndani ya maisha yako inatakiwa kusimama kataika yeye na
kumtegemea maana ndiye mwenye uwezo wa kukupa mamlaka ya kuondoa matatizo na
kukemea mapepo na matatizo mbali mbali na yanaondoka.
Baada ya maombi haya ya kongamano watu wengi wataanza kukushangaa na wengine
watashangaa kukuona kuwa unaenda kuinuliwa na kuacha umaskini katika maisha
yako yote maana pale utakapookoka Mungu anaenda kukubariki na kukufanikisha
katika maisha yako na utakuwa mfano katika maisha yako.
ukisoma
kitabu cha kutoka 11:1-3 inasema Bwana akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao
na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa
ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa. Basi nena wewe masikioni mwa watu hawa, na kila
mtu mume na atake kwa jirani yake, na kila mwanamke atake kwa jirani yake,
vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu. Bwana akawapa watu hao kibali machoni pa
Wamisri. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri,
machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake.
Hata hivyo aameongeza kuwa inachotakiwa ni kuhakikisha
unafuata taratizi za Mungu na pia inatakiwa ujifunze juu ya suala la uchumi
katika maisha yako unapoendelea na maombi na maombezi ili ufanikiwe na
kufanikiwa.
Kanisa la
eagt City Center limeanza kongamano la la siku tisini kuanzia april tatu hadi julai 3 mwaka huu na wangi
wameanza kufunguliwa na kuwekwa huru bila kuangalia dini dhehebu kanisa na
kabila mbalimbali.
unaweza kuwasiliana na kanisa la EAGT City
center na namba 0784367826,0754367826 na
0718267171 pia tembelea www.pastorkatunzi.blogspot.com
au tovuti ya www.eagtcc.org
0 comments:
Post a Comment