Waumini wametakiwa kusimamia utakatifu ambayo ndiyo njia pekee inayoweza kumasaidia mwananadamu kumwona Mungu katika maisha yako ya kila siku na hakuna anayeweza kumwona Mungu pasipo utakatifu.
Hayo yalisemwa na askofu wa kanisa la EAGT City Center iliyopo
jijini Dar es salaam askofu Florian Josephat Katunzi wakati akifundisha somo
la utakaso kanisani hapo ambapo alisema kuwa utakaso ndiyo njia pekee ya
kufanya mambo mema na kumwona Mungu na ukuu wake katika maisha yako yako ya
kila siku.
Aidha alisema kuwa utakaso ni tendo la kiimani la
kujitenga na vitu ambavyo ni viovu au kilicho kiovu jambo linalokupelekea utengwe na dhambi na mauti na hata
na biashara na maisha yako yanakuwa salama na bora.
"waumini wakishatengwa na dhambi watakuwa wametengwa
na matatizo na magonjwa maana kupigwa kwake Yesu wanadamu wamewekwa huru na
kufunguliwa maana wanadamu wengi wamekuwa wakiteseka kateseka bila kufahamu
kuwa kwa nini wanapitia katika matesso hayo"alisema askofu Katunzi.
Aidha alisema kuwa ni vyema waumini wakaaamu kuwa makini
kuepuka kuwa sehemu ya kuhifadhia majini
na mapepo bila wewe kufahamu maana mwisho wake utakuwa ni mbaya kuliko hapo
awali maana Mungu akishamsamehe mtu
dhambi kinafuata ni kuondolewa magonjwa na matataizo zote zinazokuandama
katijka maisha yako na katika ukoo jamii na familia yako.
Akinukuu kitabu cha Isaya 38:1-6 alisema kuwa Hezekia
aligua,akawa katika hatari ya kufa lakini Mungu alimtuma Samweli kupeleka
ujumbe kwake kuwa atengeneze mambo ya nyumba yake maaana anaenda kufa hakika.
AkitoA mfano w akijana ambaye aliletwa na mama yake
kanisani alisema kuwa mume wake alikufa kwa ugonjw wa kuumwa kichwa na mtoto
wake wa kiume pia alikufa kwa kuumwa kichwa na alipougua na mwingine aliamua
kumleta kanisani na kuanza kumwombea na mwisha wake mama alidondoka na kuanza
kupagwa na mapepo badala ya mgonjwa na kuanza kusema kuwa tumeifunga familia
hii.
Akielezea juu ya suala la utakaso alisema kuwa kuna
utakaso wa roho na wa nafsi hayo yote mwamini lazima afunguliwe katika tatizo
hilo na kuwekwa huru na hapo ndipo mkambo yake yatakuwa salama maana kupitia Damu ya Yesu ndiyo inayotakasa
na kuweka huru kila mmoja ambaye amemkubali Yesu kama Bwana na mwokozi wa
maisha yake.
"kila mmoja ambaye anapitia katika mapito magumu ni
vyema afunguliwe na kuwekwa huru mbali na dhambi na magonjw a ambayo yamekuwa
yakikitesa kwa muda mrefu.Ni vyema akaamua kujiuliza maswali kuwa ni kwanini
unakubali kiteseka na kupitia katika mapito magumu huku Yesu amekuweka huru"
alisema Askofu katunzi kwa kusisitiza.
Aliongeza kuwa Mungu aliye mweka huru ndugu Bonifasi
asiliwe nyama na wachawi ndiye ambaye anaenda kukuokoa na matatizo na masumbuko
ya adui shetani na kukuweka huru mbali na magonjwa na matatizo na taabu mbalimbali
ambazo yamekuwa kikwazo katika maisha yako ya kila siku ambayo imekupelekea
kukata tamaa.
Uovu ulioko ndani ya familia yako,jamii yako na hata
katika ukoo wako wewe unaweza kuondoa kwa kuomba na kufunga huku ukitolea
sadaka na kukombolewa na upoenda kanisani tarajia kukutana naMungu sio askofu
Katunizi.
Askofu katunzi pia alisema kuwa siku ya tarehe 26 April
2016 kutakuwepo na ibada maalum ya familia ambayo itaanza kuanzia saa mbili
asubuhi hadi saa saba kwa lengo la kuomba kutengwa na uovu
Ambapo alinukuu kitabu cha Ayubu 1:11 kwa muda mwingi
ayubu alikuwa akimpendeza Mungu katika misha yake hapo shetani akasema kuwa ni
kwa vile kulikuwepo na ulinzi wa Mungu juu yake na ndipo alisposema gusa mali
yake naye atakuwacha.
"ibada hii itakuwa wa kuowambea na kuwakomboa kwa
kuwaombea na kuwatolea sadaka ya ukombozi maana hata Ayubu hakuwaacha watoto
wake nyuma ila aliwapeleka katika nyumba ya ibada pamoja na kutolea sadaka na
kuwaombea rehema maaana inawezekana kuwa walitenda dhambi"alisema askofu
katunzi.
Kuna madhehebu ya dini ambayo hawaachi watoto wao nyuma wanaenda
anao katika nyumba ya ibaada ila waumini
wengine wanaacha watoto wao manyumbani hata neno la Mungu hawafundishi ndani ya
akili zao zimejaa masomo ya dunia na mambo yaasiompendeza Mungu .
Hata hivyo alisema kuwa Inatakiwa watoto wako wafundishwe
neno la Mungu jumapili jioni na jumamosi jioni ili watoto wafundishwe na
kukumbushwa masuala ya Mungu ili aweze kusimama katika nafasi yake wenyewe.
Amen
ReplyDelete